Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Naona 0019 Ethiopian airlines waeioder kwa maana hiyo nao wameamua kuchukua hiyo terribe teens,je wao wamenunu kwa USD ngapi je ni USD 99 au? Wamepigwa kama sisi


Ukisoma taarifa mbalimbali ikiwemo Boeing wenyewe ndege hizi zimewekewa price listing ya $224 , lakini bei zake halisi zimepunguzwa ili kuvutia wateja. Katika msingi kama huu kuna uwezekano kuwa Boeing na serikali ya Tanzania walikubaliana bei ya chini tofauti na bei ya Tangazo lakini pia wakaamua wasipublish bei hiyo ya makubaliano ili kulinda heshima ya ndege kibiashara.
Sina hakika sana na hili ila ni mawazo na mtazamo wangu binafsi kuwa kama ukiuza au ukanunua bidhaa kwa nusu bei ya thamani yake kuna uwezekano mkubwa ukashusha heshima ya bidhaa hiyo na pengine kuwapa watu walakini wa usalama wa matumizi yake na hivyo kushindwa kupata abiria, na pengine hata kwa kampuni nzima na hivyo kuathiri hata ndege nyingine za brand nyingine ulizonazo katika fleet.

Katika mtazamo huo hiki kinachotokea sasa hakikutarajiwa na pengine damage yake huenda ikawa sawasawa au zaidi ya kile kampuni/serikali ilichojaribu kukilinda...

Haya ni mawazo na mtazamo wangu tu binafsi, sio facts!
 
Hujaelewa nini hapo shabiki wa Bashite, au umeazima akili za Bashite?
Kifupi mmetupigisha watanzania kwa ujuaji wenu, wewe kila kitu anafanya raisi wa nchi, mambo yakiharibika hakuna wakumtowa kafara.

Si usubiri tuone, unajua Raisi wetu mpendwa ana subira. Akikiwasha wanaojifanya wajanja wanamkoma.

Hapa kazi tu
 
Embu nifupishie kuwa nani ameitumia hiyo ndege na ilitumika kwa muda gani? Na pia hizo tarehe zote vipengele kwa kifupi vinaashiria nini hadi Dec 2016. macho yananiuma nimeshindwa kusoma yote vizuri.
Wewe kweli ni kichwa maji yaani bogas yaani pamoja na maelezo yote ya mleta uzi bado upo mweupe tu kichwani?
 
Ukisoma taarifa mbalimbali ikiwemo Boeing wenyewe ndege hizi zimewekewa price listing ya $224 , lakini bei zake halisi zimepunguzwa ili kuvutia wateja. Katika msingi kama huu kuna uwezekano kuwa Boeing na serikali ya Tanzania walikubaliana bei ya chini tofauti na bei ya Tangazo lakini pia wakaamua wasipublish bei hiyo ya makubaliano ili kulinda heshima ya ndege kibiashara.
Sina hakika sana na hili ila ni mawazo na mtazamo wangu binafsi kuwa kama ukiuza au ukanunua bidhaa kwa nusu bei ya thamani yake kuna uwezekano mkubwa ukashusha heshima ya bidhaa hiyo na pengine kuwapa watu walakini wa usalama wa matumizi yake na hivyo kushindwa kupata abiria, na pengine hata kwa kampuni nzima na hivyo kuathiri hata ndege nyingine za brand nyingine ulizonazo katika fleet.

Katika mtazamo huo hiki kinachotokea sasa hakikutarajiwa na pengine damage yake huenda ikawa sawasawa au zaidi ya kile kampuni/serikali ilichojaribu kukilinda...

Haya ni mawazo na mtazamo wangu tu binafsi, sio facts!
Tatizo ni usiri usio na maana na unaotia mashaka
 
s
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg


5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg


Boeing 787 Register - Welcome

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page
sawa
 
hapa ndopale mtu hajawai hata kununua baiskeli anataka kuelekeza namna ya kununua ndege!!! Tz bhana...
Kiufupi inaonesha tumeibiwa tena kutokana na kiherehere cha kununua ndege wanasema hakukuwa hata na business plan pale ATC..
sijui Ni kiherehere chanani hiki?
 
This whole thing regarding those planes is so terribly convoluted...

So much information...you don't know for sure who's telling the truth and who's not!

But oh well...nowadays anybody can be an expert on anything and everything.

Naomba unisaidie hiyo link aliyorusha yenye bei ya 99m ni ipi? Umeiona na mimi nikajisomee.
 
Back
Top Bottom