Mkuu Mimi Nakuonea Huruma Sana kwa kuwa umeuvika Ubongo wako Wingi la mafundsho ya Ellen Basi Ngoj nikuache maana Yohana Anasema Mwanamke Kahaba ni Mji ww unasema Ni Kanisa inabid watu wanaoptia uzi huu wang'amue tu wenyewe wAfuate unayosema ww au Yohana
UNGEANZA KUJIONEA HURUMA WEWE AMBAYE UMEPOTEA , MAANA INAONESHA BIBLIA HUSOMI ILA UNASOMEWA
BIBLIA IPO WAZI MWANAMKE HUYO NI NANI
FUNGU 1: “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;”
Mwanamke katika unabii huwakilisha kanisa (angalia Ufunuo 19:7; 21:2; na 2 Wakorinto 11:2). Katika kitabu cha Ufunuo sura ya 12 ametajwa mwanamke safi ambaye anawakilisha kanisa la kweli la Mungu, lakini mwanamke anayezungumziwa katika Ufunuo 17 ni mchafu na ametajawa kama Kahaba. Mwanamke huyu anawakilisha kanisa ambalo limeacha kumtii Mungu na amri zake, na likafanya uzinzi na shetani kwa kufuata maagizo yake.
Kahaba Mkuu: Hii wakati inapotumika katika unabii, ni mfano unaowakilisha kanisa ambalo limeachia kutii Neno la Mungu na badala yake linatii neno la shetani. Mfano huu siku zote hutumika kuwalenga watu ambao walikuwa kama jumuiya wakitumiwa na Mungu kufanya mapenzi yake, lakini wakaiacha njia yake na wakaachia kuisikiza sauti yake na kufuata uovu. Wayahudi katika historia yao katika Agano la Kale walitangazwa mara nyingi kuwa kahaba, kila walipoacha kufuata maagizo ya Mungu. Yeremia alisema: “Tena, Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi. 7 Nami nalisema baada ya yeye kuyatenda hayo yote, Atanirudia mimi, lakini hakurudi;. . . 8 Nami nikaona, wakati nilipokuwa nimemwacha Israeli mwenye kuasi, nikampa hati ya talaka kwa sababu hiyo ya kuzini, dada yake, Yuda mwenye hiana, hakufanya hofu; bali yeye naye akaenda akafanya mambo ya ukahaba. 9 Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.” (3:6-9; angalia pia Ezekieli 16,17 na Hosea 2).
Kwa hiyo mfumo wa kanisa kuitwa Kahaba, inaonyesha kuwa kama jumuiya wameasi kutoka katika uongozi wa Mungu, na wanafuata njia zao wenyewe wala hawasikilizi sauti ya Mungu wala kutii amri zake na maagizo yake. Na kwa kuwa malaika hapa anatumia neno “kahaba mkuu” hii inaonyesha wazi kwamba kuna makahaba wengine wengi ambao ni mifumo ya makanisa ya leo yaliyoasi kutoka kwenye ukweli wa neno la Mungu na kufuata mapokeo ya wanadamu. Hii imethibitishwa katika fungu la 5 ambapo huyu kahaba mkuu ametajwa kama “MAMA WA MAKAHABA”, hii inaweza pekee kumaanisha kwamba hawa makahaba wengine ambao ni binti zake wameanguka kutoka katika njia ya Mungu kwa sababu ya kufuata njia za kahaba huyu, na ndio maana ni mama yao na ni kahaba mkuu kwao.
Kanisa katoliki hujiita mama wamakanisa. Katika barua waliotumiwa maaskofu wote wa ulimwengu, Cardinal Joseph Ratzinger aliandika hivi: "Yapasa izidi kueleweka waziwazi ya kwamba kanisa moja lilio takatifu, la kikatoliki na la mitume linalozaa dunia nzima, hilo sio dada bali ni mama wa makanisa yote" (Daily telegraph, September 4, 2000).
Matangazo ya aina hii huchangia kuhakikisha ya kwamba kanisa katoliki ndilo linalo utimiza unabii wa Ufunuo 17:5.
NAKUSIHI JIONEE HURUMA WEWE , AMBAYE HUWEZI KUSOMA BIBLIA MWENYEWE MPAKA USOMEWE NA PADRI