Hapana hujajibu swali langu nililo kuuliza.
Naomba aya inayo watambulisha
Seventh Day Adventist kwenye biblia.
SDA IN THE BIBLE PROPHECY
"Ndipo yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana
yule mwanamke [Kanisa la Mungu], akaenda
zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia
- wale wanaozitii amri za Mungu na kuwa na
ushuhuda wa Yesu." - (Ufunuo 12:17).
UTANIAMBIA NI KANISA GANI LINATII AMRI ZOTE KUMI NA KUZIFUNDISHA NA LINA USHUHUDA(ROHO YA UNABII) KATIKA HIZI SIKU ZA MWISHO , KAMA SIO SDA TU, MAANA MAKANISA MENGINE YOTE YAMEREJEA KWA MAMA.YAO ROMAN CATHOLIC NA YANAZIDI KUMTUKUZA KWA KUKUMBATIA AMRI ZAKE FAKE NA MAPOKEO IKIWEPO IBADA YA JUMAPILI, IBADA ZA SANAMU N.K
Unabii huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani
amekasirika sana; anafanya vita dhidi ya wazao
wa mwanamke waliosalia" - yaani, dhidi ya watu
wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao
zinazowatambulisha:
(1)Waumini hao wa siku za mwisho wanao
"ushuhuda wa Yesu." Kwa uaminifu
wakiyang'ang'ania mafundisho safi ya Neno la
Mungu, wanamshuhudia Yesu kwa njia ya maisha
yao yenye nguvu nyingi ya Kikristo.
(2) Wakristo hao wa siku za mwisho ni watu wa
unabii. Kuupokea ule "ushuhuda wa Yesu Kristo"
kulimwezesha Yohana kukiandika kitabu kile cha
Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundi hilo la mwisho la
waumini linapokea karama ile ile: yaani, ushuhuda
wa moja kwa moja toka kwa Mungu kupitia kwa
mjumbe wa kibinadamu. Karama yao ya unabii
inalenga juu ya ufunuo wa Mungu kuhusu utume
wao na mwisho wao.
(3) Wakristo hao wa siku hizi za mwisho
wanatambulikana pia kama "wale wanaozitii Amri
[kumi] za Mungu." Hawatetei tu ukamilifu wa
hizo Amri Kumi, bali wanazitii pia. Upendo wa
Mugu ulio mioyoni mwao unawaletea utii
unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5;
13:8-10).
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata
kielelezo cha Kristo na cha kanisa lile la kwanza
kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilo
linamkasirisha vibaya sana yule Joka - yaani, yule
Ibilisi. Naye anapigana vita dhidi ya "wazao" wa
mwanamke "waliosalia" kwa sababu wanatoa
ushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu
unawafanya wafuasi wake hao kuwa watii. Kama
vile Kristo alivyoagiza, aliposema:
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana
14:15.
Maisha ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho
yanaonyesha kwamba uwezekano upo wa
kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na
kuwapenda wenzetu kama sisi tunavyojipenda
wenyewe. Kulingana na maneno ya Yesu, sifa hizo
za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo
kwa watu, hufanya muhtasari wa Amri kumi za
Mungu (Mathayo 22:35-40).
Ya nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza
Jumamosi, siku ya saba ya juma, kama Sabato.
Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani
ya mioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut.
20:3-17; Yak. 2:10-12], basi, Wakristo hao wa
siku hizi za mwisho ni Wasabato.
Sabato ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa
Mungu kwa watu wake katika kitabu cha Ufunuo,
sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbinguni
zinajipanga nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi
za mwisho walioelezwa katika sura hizo.
Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na
Roho Mtakatifu anafanya kazi yake "kuwafanya
imara kwa nguvu katika utu wao wa ndani."
Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani
"kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la
ushuhuda wao" (Ufunuo 12:11).
Je! unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa
siku hizi za mwisho ambao "wanazitii amri [kumi]
za Mungu" tena wa"na ushuhuda wa Yesu"? Kwa
nini usikate shauri sasa hivi?