Wewe jamaa toka day one niligundua una uhaba wa kulijua neno, halafu unataka mashindano, ukishindwa unaanza matusi
Hao wakristo unaosema walianzia Antiokia bado
Biblia inatuambia walifanya IBADA SIKU YA SABATO
IBADA YA JUMAPILI IMELETWA NA UPAPA
SASA MIMI NAKUPA UTHIBITISHO WA BIBLIA
Yakobo, kiongozi wa kwanza wa kanisa lile la mwanzo, aliandika maneno haya kuhusu zile Amri kumi:
"Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yule yule aliyesema: "USIZINI, "alisema pia" "USIUE." Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria" - (Yakobo 2:10, 11).
Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lile la kwanza, anatoa taarifa hii.
"Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi, tukiongea na wanawake waliokusanyika mahali hapo" - (Matendo 16:13).
Kitabu cha Matendo cha Agano Jipya kinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyo na wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwa zikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 pale Antiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 pale Thesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).
Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili, aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
"Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho" - (Ufunuo 1:10).
Kulingana na maneno ya Yesu, siku ya Bwana ni Sabato:
"Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato" - (Mathayo 12:8).
Uchunguzi wa ushahidi wa maandiko unaoonyesha wazi kwamba wale mitume hawakufanya jaribio lolote la kuibadili siku ya Mungu ya mapumziko kutoka siku ya saba kwenda ile siku ya kwanza ya juma. Agano jipya, linaitaja siku hiyo ya kwanza ya juma mara nane tu. Katika mifano hiyo yote hakuna ambapo siku ya kwanza ya juma inatajwa kuwa ni takatifu, wala hata kudokezwa kuwa tunapaswa kuitenga kama siku ya ibada. Uchunguzi uliofanywa kwa makini sana wa hayo mafungu manane yanayoitaja siku ya kwanza ya juma huonyesha matukio haya yaliyotokea Jumapili:
(1) Wanawake walikwenda kaburini siku ile ya kwanza ya juma (Mathayo 28:1).
(2) "Hata Sabato ilipokwisha" wanawake wakaanza tena kufanya shughuli zao za kidunia katika siku ile ya kwanza ya juma (Marko 16:1,2).
(3) Yesu alimtokea kwanza Mariamu Magdalena mapema siku ile kwanza ya juma (Marko 16:9).
(4) Wafuasi wa Yesu walianza tena kufanya shughuli zao katika ile siku ya kwanza juma (Luka 24:1).
(5) Mariamu alikwenda kwenye kaburi lile la Yesu na kulikuta kaburi liko tupu katika ile siku ya kwanza (Yohana 20:1).
(6) Wanafunzi wale walikusanyika mahali pamoja "kwa hofu ya Wayahudi" (si kwa ajili ya kuendesha ibada ) Katika ile siku ya kwanza ya juma (Yohana 20:19).
(7) Paulo aliwaomba washiriki wa kanisa kufanya mahesabu ya fedha zao walizopata katika ile siku ya kwanza ya juma, na "kuweka kando kiasi fulani cha fedha" kwa ajili ya maskini kule Yerusalemu (I Wakorintho 16:1,2). Kifungu hicho hakitaji mkutano wowote wa dini ambao ulifanyika.
(8) Katika Matendo 20:7 Luka anaongea habari za hotuba (mahubiri) ya Paulo aliyoitoa katika ile siku ya kwanza ya juma wakati wa mkutano ule wa kuagana ambao haukutazamiwa kufanyika. Kusema kweli, Paulo alihubiri kila siku, na mitume wale walimega mkate kila siku (Matendo 2:46).
Hakuna hata moja kati ya mafungu hayo linalodokeza ya kwamba wale mitume waliazimu kuacha kuitunza Sabato ya siku ya saba. Mitume wale hawakulitaja badiliko lolote la Sabato kutoka siku ya saba kwenda ile ya
kwanza ya juma.
View attachment 927881