Tanzania tumefikia sehemu kwenye siasa zetu mpaka tumesahau tofauti ya siasa, vyama na kuona kila kitu uadui.
Nilikuwa namwangalia leo CAG akisoma repoti na kusema mwenyewe. Je, hayo anayosoma yote angesoma mtu wa upinani kama Lema serikali ingechukulia kama ni mawazo au ingechukulia kama ni uchochezi ingawa ni ya kweli. Inaelekea ukosoaji unaruhusiwa tu kwa CAG mwananchi wa kawaida akisema yaleyale kuna hatari kubwa ya kufugwa.
Lakini hii inaonyesha ukweli kwamba tumefika wakati hatusikilizani tena. Ukimwona mtu au kuona jina la mtu unakuwa umeshaweka mawazo yako binafsi kichwani bila hata kusoma hoja au kusikiliza mawazo. Hata kwenye mitandao kuna watu wengi wana tabia hii yaani wakiona hoja ya mtu fulani wanakuwa wameshamweka kwenye box na kufikiria wanajua anafikiria nini.
Hebu jiulize kabisa; Je, hata yote yangesomwa na mpinzani na kusema ni uchunguzi wake angekuwa wapi leo. Na ukishajiuliza kwa nafsi yako binafsi utajua nchi yetu imefika wapi.