Ukweli kama hii report ya CAG ingesomwa na mpinzani kama Lema angeshikwa na kushitakiwa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,551
8,642
Tanzania tumefikia sehemu kwenye siasa zetu mpaka tumesahau tofauti ya siasa, vyama na kuona kila kitu uadui.

Nilikuwa namwangalia leo CAG akisoma repoti na kusema mwenyewe. Je, hayo anayosoma yote angesoma mtu wa upinani kama Lema serikali ingechukulia kama ni mawazo au ingechukulia kama ni uchochezi ingawa ni ya kweli. Inaelekea ukosoaji unaruhusiwa tu kwa CAG mwananchi wa kawaida akisema yaleyale kuna hatari kubwa ya kufugwa.

Lakini hii inaonyesha ukweli kwamba tumefika wakati hatusikilizani tena. Ukimwona mtu au kuona jina la mtu unakuwa umeshaweka mawazo yako binafsi kichwani bila hata kusoma hoja au kusikiliza mawazo. Hata kwenye mitandao kuna watu wengi wana tabia hii yaani wakiona hoja ya mtu fulani wanakuwa wameshamweka kwenye box na kufikiria wanajua anafikiria nini.

Hebu jiulize kabisa; Je, hata yote yangesomwa na mpinzani na kusema ni uchunguzi wake angekuwa wapi leo. Na ukishajiuliza kwa nafsi yako binafsi utajua nchi yetu imefika wapi.
 
Tatizo chadema wanaropoka tu ndio wanapo shindwa habari zao nyingi upotofu na takwimu za kupika mpinzani anae sema kweli Ni zito maalim sefu mbatia ila chadema hata wakisema haya ni maji kunywa usiamini unaweza kuta Ni mkojo wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakumbuka kuna wakati wanasiasa walikuwa hawampendi CAG ayepita mfano waziri wa mambo ya ndani alisema report yake ni ya wongo. Hivyo hata CAG inaelekea kuna ambao wanaangalia zaidi ni nani kasema kuliko ni nini kimesemwa. Huu ni utamaduni mbaya sana
 
No numbers don't lie. Hata ingesomwa na Lema asingeshikwa. Mbunge ana kinga ya kibunge.
Cha muhimu ni kuwa na facts.
Hata Lowassa baada ya kushindwa alisema haya

Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! - JamiiForums

Na hakushikwa.
P
CAG aliepita Prof Assad jee yeye hakua akisomAa namba kama huyu ? maana kwake yeye ilikua hapakaliki, kuanzia speaker wabunge wa CCM, mawaziri na hata makada wa chama walimjia juu kumbeua na kumdhihaki.

Mayalla hebu lielezee hili
 
Huyu kipenzi cha jamaa sioni hata kama ana weledi kama ule wa Assad, anajua kapewa hiyo nafasi kama zawadi, siku zote atatekeleza majukumu yake kumfurahisha bosi wake.

Ripoti ya Profesa Assad ilikuwa tamu zaidi, watu wanaulizana maswali majibu hawana, wakaona isiwe tabu tumuite tumuulize mbele ya kamera labda atatuonea huruma atakanusha, kweli akakanusha, ila ukweli ulibaki palepale, trillion 1.5 mpaka leo hazijulikani zilipokwenda, mwishowe wakaona wamuondoe tu Assad kwenye nafasi yake, badala ya kutafuta majibu ya maswali yake.

Halafu wanajiita wazalendo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo chadema wanaropoka tu ndio wanapo shindwa habari zao nyingi upotofu na takwimu za kupika mpinzani anae sema kweli Ni zito maalim sefu mbatia ila chadema hata wakisema haya ni maji kunywa usiamini unaweza kuta Ni mkojo wao

Sent using Jamii Forums mobile app
Inakuwaje basi, kama hivyo ndivyo, inapofika wakati wa uchaguzi, CCM ya Magufuli inapanic hivyo, na kupora kura au kuengua wapinzani? Na kisha kuwabambikia kesi viongozi wa upinzani? Hasa CHADEMA. Angalia chaguzi za marudio zilivyokuwa figisu. Ule wa serikali za mitaa ndio kabisaa wizi wa mchana kweupeee. WEZI WAKUBWA NYIE.
 
Tanzania tumefikia sehemu kwenye siasa zetu mpaka tumesahau tofauti ya siasa, vyama na kuona kila kitu uadui

Nilikuwa namwangalia leo CAG akisoma repoti na kusema mwenyewe Je hayo anayosoma yote angesoma mtu wa upinani kama Lema serikali ingechukulia kama ni mawazo au ingechukulia kama ni uchochezi ingawa ni ya kweli. Inaelekea ukosoaji unaruhusiwa tu kwa CAG mwananchi wa kawaida akisema yaleyale kuna hatari kubwa ya kufugwa.

Lakini hii inaonyesha ukweli kwamba tumefika wakati hatusikilizani tena. Ukimwona mtu au kuona jina la mtu unakuwa umeshaweka mawazo yako binafsi kichwani bila hata kusoma hoja au kusikiliza mawazo. Hata kwenye mitandao kuna watu wengi wana tabia hii yaani wakiona hoja ya mtu fulani wanakuwa wameshamweka kwenye box na kufikiria wanajua anafikiria nini.

Hebu jiulize kabisa je hata yote yangesomwa na mpinzani na kusema ni uchunguzi wake angekuwa wapi leo. Na ukishajiuliza kwa nafsi yako binafsi utajua nchi yetu imefika wapi.
Usihofu ndio maana ya kupewa mamlaka na hayo ndo mamlaka yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ripoti ya CAG nyepesi mno, Wala haina uzito wowote...ndio maana hata Magufuli amesema tutaipeleka bungeni bila kupunguza chochote .

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti Polisi wamelipa mil.193.12 kwa watumishi waliokufa au kufukuzwa kazi ndo iwe na uzito wa kutikisa mtu? Hata IGP mwenyewe amefurahi tu kwa sababu hakuna ubadhirifu wa fedha bali uzembe wa kuhasibu!

Leta hesabu za ununuzi wa ndege na ujenzi wa reli ilitoshindikana tukuone msafi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania tumefikia sehemu kwenye siasa zetu mpaka tumesahau tofauti ya siasa, vyama na kuona kila kitu uadui.

Nilikuwa namwangalia leo CAG akisoma repoti na kusema mwenyewe. Je, hayo anayosoma yote angesoma mtu wa upinani kama Lema serikali ingechukulia kama ni mawazo au ingechukulia kama ni uchochezi ingawa ni ya kweli. Inaelekea ukosoaji unaruhusiwa tu kwa CAG mwananchi wa kawaida akisema yaleyale kuna hatari kubwa ya kufugwa.

Lakini hii inaonyesha ukweli kwamba tumefika wakati hatusikilizani tena. Ukimwona mtu au kuona jina la mtu unakuwa umeshaweka mawazo yako binafsi kichwani bila hata kusoma hoja au kusikiliza mawazo. Hata kwenye mitandao kuna watu wengi wana tabia hii yaani wakiona hoja ya mtu fulani wanakuwa wameshamweka kwenye box na kufikiria wanajua anafikiria nini.

Hebu jiulize kabisa; Je, hata yote yangesomwa na mpinzani na kusema ni uchunguzi wake angekuwa wapi leo. Na ukishajiuliza kwa nafsi yako binafsi utajua nchi yetu imefika wapi.
Lema kawa CAG toka lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwel hii kinga ipo ktk awamu hii?ikiwa wabunge wanakamatwa mpka ndan ya bunge na kila kukicha wanafunguliwa mashtaka feki. Na hiyo facts unayosema ndyo ilisababisha mmoja wao kuwa mhanga mpk leo hayupo ktk nchi yake.
No numbers don't lie. Hata ingesomwa na Lema asingeshikwa. Mbunge ana kinga ya kibunge.
Cha muhimu ni kuwa na facts.

Hata Lowassa baada ya kushindwa alisema haya

Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu? Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! - JamiiForums

Na hakushikwa.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom