Ukweli juu ya freshley mwamburi wimbo wa stella ..

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,238
22,669
Wakuu
Kitambo Fulani pale Kenya ulihit sana wimbo kwa jina la Stella ..

Wimbo huo ulioimbwa na mtu aitwaye freshley mwamburi ni kisa cha msichana aliyeitwa Stella , ambaye alipelekwa japan na bwana mwamburi kusoma udaktari mpaka alipomaliza masomo yake Ili kurejea nyumbani Kenya na shida ikaanzia hapo.


Kisa kinaendelea pale Stella alipotoa taarifa kwa bwana freshley mwamburi kuwa ajisogeze airport kumpokea ..!

Then mzee wetu akajisogeza kumsubiri kwa ugwadu mkubwa sanaaa.

Stella aliposhuka ndani ya ndege, bwana mwamburi alipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kumuona Stella ameshuka na Mtoto kambeba na nyuma yake yupo mjapani ambaye ndiyo baba wa Mtoto , mwenye urefu wa futi NNE.!

Bwana mwamburi alipigwa butwaa sana inasemekana yeye ndiye aliyemsomesha Stella na huyo mjapan ndiye alikuwa mwalimu wa Stella na alimzalisha na kumuoa na hata kuja naye Kenya ..!

Ndipo kama wimbo unavyojieleza hapo chini je ni kisa cha kweli????


__________________________________
Freshley Mwamburi_Stella wangu

Nilikua na mchumba wangu
Tulipendana kama nyama choma,
Alibahatika kwenda ngambo
Chuo kikuu kwenda kusoma
Miaka mitatu kule Japani
Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilikua na mchumba wangu
Tulipendana kama nyama choma
Alibahatika kwenda ngambo
Chuo kikuu kwenda kusoma
Miaka mitatu kule Japani
Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilivyo mpenda Stella jamani
Kujitolea kwa roho moja
Nikauza shamba langu
Sababu yake yeye

Nikauza gari langu, sababu yake yeye
Nikauza Ng'ombe na mbuzi sababu yake yeye
Ili apate nauli yake
Na pesa nyngine za matumizi kule Japani

Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano
Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano
Ndiyo ilokua tarehe kamili ya Stella kurudi Kenya
Nilikwenda uwanja wa ndege kwenda kumlaki Stella

Nilikua na uncle Kilinda uwnaja wa ndege
Nilikua na baziri mwa Kolomba na mkewe na watoto wake
Nilikua na uncle Mshomba wa mdundonyike tuveluva
Nilikua na ndugu Afisi mtoto wa Mombasa

Ghafla ndege lipotua uwanajani tuliona vituko
Stella alishuka amebeba mtoto mkononi
Nyuma yake mchumba wake mfupi
Futii nne Mjapani

Nilisikitika ndani ya moyo
Nikakosa la kufanya
Nilitamani nilie Kikamba lakini sikijui
Ilibidii nilie Kijaluo" angatima ngo wachoa", Freshley

Nilitamani nilie Kihindi lakini sikijui
Ilinibidi nilie Kitaita lugha ya mama na baba
Ilinibidi nilie Kitaiata
"Beke mwana niponyebanda, Freshley"

Nilikua na mchumba wangu
Tulipendana kama nyama choma
Alibahatika kwenda ngambo
Chuo kikuu kwenda kusoma
Miaka mitatu kule Japani
Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilikua na mchumba wangu
Tulipendana kama nyama choma
Alibahatika kwenda ngambo
Chuo kikuu kwenda kusoma
Miaka mitatu kule Japani
Kusomea udakitari, Stella wangu eeeh

Nilivyo mpenda Stella jamani
Kujitolea kwa roho moja
Nikauza shamba langu
Sababu yake yeye

Nikauza gari langu, sababu yake yeye
Nikauza Ng'ombe na mbuzi sababu yake yeye
Ili apate nauli yake
Na pesa nyngine za matumizi kule Japani

Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano
Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano
Mwaka elfu moja mia tisa tisini na mbili
Ndiyo ilokua tarehe kamili ya Stella kurudi Kenya

Nilikwenda uwanja wa ndege kwenda kumlaki Stella
Nilikua na uncle Kilinda uwnaja wa ndege,
Nilikua na baziri mwa Kolomba na mkewe na watoto wake
Nilikua na uncle Mshomba wa mdundonyike tuveluva
Nilikua na ndugu Afisi mtoto wa Mombasa

Ghafla ndege lipotua uwanajani nliona vituko
Stella alishuka amebeba mtoto mikononi
Nyuma yake mchumba wake mfupi
Futii nneMjaipani

Nilisikitika ndani ya moyo nikakosa la kufanya
Nilitamani nilie Kikamba lakini si kijui
Ilibidii nilie Kijaluo "Angatima ngo wauchoa", Freshley

Nilitamani nilie Kiindi lakini si kijui
Ikanibidi nilie Kitaita lugha ya mama na baba
Ilinibidi nilie Kitaita, "beke mwana niponyebanda, Freshley"

Iyooo, yoo, yoo, yoo
I love you Stella mami
Iyooo, yoo, yoo, yoo
I love you Stella mami

Come back, come back Stella
I still need you baby
Nikwendetete nyama kuivivya
Stella kindu wakwa

Nikwendetete nyama kuvivya
Ya kuvulania na kachumbari
Ukava kuvi nakwa Stella, linda unguune kisi
Ukava kuvi nakwa Stella linda unguune kisi

Nakupenda kama choma Stella mpenzi wangu
Nakupenda kama nyama choma Stella mpenzi wakwa
Ukava kuvi nakwa Stella linda unguune kisi
Nikwendetete nyama kuvivya
Ya kuvulania na kachumbari

Come back, come back Stella
I still need you baby
Come back, come back Stella
I still need you baby

Kwanini kunichenga chenga hivyo
Stella kama mpira uwanjani
Kwanini kunichenga chenga hivyo
Stella kama mpira uwanjani
Kwanini kunichenga chenga hivyo
Stella kama mpira uwanjani

download.jpeg
 
Back
Top Bottom