Baada ya miaka 28 kupita, Freshley Mwamburi asema kumsamehe Stellah kwa kumuacha na kuolewa na Mjapani futi 4

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Freshley.JPG

Msanii wa Muziki Kenya, Freshley Mwamburi amesema kuwa amemsamehe Stellah wake ambaye alijitolea kwa ari na mali kumsomesha Udaktari miaka 5 nchini Japan.

Baada ya Stellah kuhitimu udaktari nchi Japan na kurejea Kenya, cha ajabu Freshley akiwa ameambatana na ndugu na jamaa zake wakienda kumpokea Stellah na kumpongeza kwa kisomo, Stellah alishuka kwenye ndege akiwa na mtoto, pia akiwa ameambatana na mchumba wake yule Mjapan.

Lilikuwa ni Pigo kubwa sana kwa Freshley na kuacha gumzo kwa waliokuwa wamemsindikiza. Freshley anasema alitamani kulia Kitaita, Kijaluo lakini ikabidi alie kikamba lugha ya baba na mama.

Kila ifikapo tarehe tarehe 17 Mei ya kila mwaka, Wakenya huonesha hisia zao kuhusu tukio hili ambalo lilitokea tarehe tajwa hapo.

Pia soma

- It’s 25 years since Stellah dumped Mwamburi

- Leo trh 17/05 ni siku ambayo Stellah alirudi kutoka Japan na mchumba wake mwenye urefu wa futi 4

Sikiliza wimbo wa ''Stellah Wangu'' wenye kisa cha kusisimua
 
Kumsomesha mwanamke ili umuoe afadhali ubet mkeka utachanika leo kesho utaotea.
Ni mtazamo , katika maisha tunafanya mambo mengi kwa hope. Maana yake hatujui result ya tunachofanya. Kuna watu wamesomesha wana wake, wamekuja kuwa msaada mkubwa sana katika maisha yao, na pia wapo waliosome na ikawa virse versa.
 
Huu wimbo ulitamba sana enzi hizo, hata mm nilizani ni wimbo tu kumbe jamaa ilimtokea kweri, kama ingekua tz gunia 2 za mkaa zingehusika mapema tu.
Mapenzi yana maumivu makali sana, na kama utadhindwa handle hisia zako vizuri. Waweza jikuta unafanya mambo yatayo gharimu hata tegemezi wako.
 
Mwaka juzi nilipomuona ktn ama citizen tv ya Kenya akifanya mahojiano ndio nikajua kumbe ilikua hadithi ya kweli.

Mshikaji aliumia sana aisee, nilijaribu kuvaa viatu vya mshikaji nilimsikitikia sana. Mbaya zaidi jamaa alibeba wapambe, ndugu na jamaa kwenda kumpokea Stella uwanja wa ndege halafu akaisha kupata aibu kubwa ya mwaka.

Hua najiulizakama Stella alijua alikua na mume mwingine ilikuaje akamjulisha mashikaji ratiba ya tarehe yake kurudi Kenya, si bora angemficha. Ila wanawake wako hivyo siku wakikuaibisha wanakuaibisha kweli.
 
Ni mtazamo , katika maisha tunafanya mambo mengi kwa hope. Maana yake hatujui result ya tunachofanya. Kuna watu wamesomesha wana wake, wamekuja kuwa msaada mkubwa sana katika maisha yao, na pia wapo waliosome na ikawa virse versa.
Jibu lako linaonesha unasomesha mkuu..

Hauna ndugu,.?? Wadogo zako, binamu, wasio na uwezo kijijini unapotokea hadi usomeshe mwanamke.???

Pole in advance...
 
Msanii wa Muziki Kenya, Freshley Mwamburi amesema kuwa amemsamehe Stellah wake ambaye alijitolea kwa ari na mali kumsomesha Udaktari miaka 5 nchini Japan.

Baada ya Stellah kuhitimu udaktari nchi Japan na kurejea Kenya, cha ajabu Freshley akiwa ameambatana na ndugu na jamaa zake wakienda kumpokea Stellah na kumpongeza kwa kisomo, Stellah alishuka kwenye ndege akiwa na mtoto, pia akiwa ameambatana na mchumba wake yule Mjapan.

Lilikuwa ni Pigo kubwa sana kwa Freshley na kuacha gumzo kwa waliokuwa wamemsindikiza. Freshley anasema alitamani kulia Kitaita, Kijaluo lakini ikabidi alie kikamba lugha ya baba na mama.

Kila ifikapo tarehe tarehe 17 Mei ya kila mwaka, Wakenya huonesha hisia zao kuhusu tukio hili ambalo lilitokea tarehe tajwa hapo.

Pia soma

- It’s 25 years since Stellah dumped Mwamburi

- Leo trh 17/05 ni siku ambayo Stellah alirudi kutoka Japan na mchumba wake mwenye urefu wa futi 4

Sikiliza wimbo wa ''Stellah Wangu'' wenye kisa cha kusisimua
View attachment 1695476
Stella kamkondesha mpaka leo 😆😆😆😆
 
Jibu lako linaonesha unasomesha mkuu..

Hauna ndugu,.?? Wadogo zako, binamu, wasio na uwezo kijijini unapotokea hadi usomeshe mwanamke.???

Pole in advance...
Tenda wema nenda zako. Sio kwamba ukimsomesha ndio awe wako. Swala la mtu kuishi na mtu flani, ni swala nyeti sana. Hapana mie sisomeshi ila kama akitokea wa kumsomesha na uwezo ukiwepo namsomesha
 
Back
Top Bottom