Ukweli hasa ni upi?

kikwakwa

Senior Member
Dec 20, 2011
105
12
Habari wana jf,kuna jambo natatizwa nalo khs mahari,wengine wanasema mahari huwezi kulipa yote unapolipa lazima ubakishe na wengine husema mahari unaweza kulipa yote uliyopangiwa na hakuna tatizo,nipo njia panda katika hili naombeni ukweli kutoka kwenu wana jf.
 
Na unaweza usilipe kabisa...masharti ya mahari yametofautiana, ni vizuri kuuliza huko unakotaka kulipa wana taratibu gani....!uzifuate!
 
Na unaweza usilipe kabisa...masharti ya mahari yametofautiana, ni vizuri kuuliza huko unakotaka kulipa wana taratibu gani....!uzifuate!
nimeshapangiwa tayari sasa nilipe yote au nilipe nusu?
 
Kulipa au kutolipa yote kunategemea na huyo anayetakiwa kulipa hiyo mahari km ana huo uwezo kwa wakati huo. Km mahari siyo kubwa( una uwezo wa kulipa) lipa yote .

Kuna kisa cha bwana mmoja alifiwa na mkewe wazazi/wakwe wakataka mahari imalizwe kwanza ndipo marehemu azikwe au wakazike kwao. Usingoje yakukute.
 
nimeshapangiwa tayari sasa nilipe yote au nilipe nusu?

Kwetu sisi, mahari hulipwa yote kama mhusika anaweza na kwa awamu kama hawezi kulipwa yote kwa pamoja,ila kuna makabila hii wanaona si sawa (ya kulipa kwa pamoja), wanaona kama kujionyesha fulani na visababu vingine vingi....!

Ndo maana nimekushauri uulize zaidi namna ambayo inakubalika,mbona rahisi tu mwambie mchumba wako aulize shangazi zake... au baba wadogo/wakubwa!
 
Kulipa au kutolipa yote kunategemea na huyo anayetakiwa kulipa hiyo mahari km ana huo uwezo kwa wakati huo. Km mahari siyo kubwa( una uwezo wa kulipa) lipa yote .

Kuna kisa cha bwana mmoja alifiwa na mkewe wazazi/wakwe wakataka mahari imalizwe kwanza ndipo marehemu azikwe au wakazike kwao. Usingoje yakukute.

asante lee kwa ushaur ntaufanyia kazi
 
Kwetu sisi, mahari hulipwa yote kama mhusika anaweza na kwa awamu kama hawezi kulipwa yote kwa pamoja,ila kuna makabila hii wanaona si sawa (ya kulipa kwa pamoja), wanaona kama kujionyesha fulani na visababu vingine vingi....!

Ndo maana nimekushauri uulize zaidi namna ambayo inakubalika,mbona rahisi tu mwambie mchumba wako aulize shangazi zake... au baba wadogo/wakubwa!

sister Michelle asante maana umenipa mwanga
 
wengine hawalipi yote,hawa wapo wengi sana
wachache huamua kulipa yote
ila nazani inategemea wapi unapoenda kuoa
 
Mtoa mada, kwanza uliza wazee wa ukoo wenu watakuwa washauri wazuri.

Pili hiyo inategemea na makabila, kuna mengine ni sifa kumaliza yote si unaoa mke kwa kuunga unga mahari.
 
Kwetu sie umang'atini mahari haumalizi ili uwe na heshima kwa wakwe zako. Na siku ukimkorofisha mke (kupiga ni taboo kabisaaa) unakuja na mahari kidogo ya kupunguza deni, baba mkwe akiona tu mbuzi hakuna hata kesi. Binti anaitwa anakimbizwa aondoke zake. So ina faida pande zote. Usimalizie banaa!
 
Habari wana jf,kuna jambo natatizwa nalo khs mahari,wengine wanasema mahari huwezi kulipa yote unapolipa lazima ubakishe na wengine husema mahari unaweza kulipa yote uliyopangiwa na hakuna tatizo,nipo njia panda katika hili naombeni ukweli kutoka kwenu wana jf.

Mkuu kwa ujumla Tanzania mahari haishi unaweza kwenda kumalizia ukiwa tayari mkeo keshapata mtoto.
 
haaaaa
inategemea, kwetu mahari huwa hailipwi yote
ukilipa yote ni dalili ya dharau majivuno na kujifanya unazo

muulize mkeo mtarajiwa utaratibu wa kwao uko vipi
 
Cna uhakika na dini yako wala kabila lakini kama uwezo unao bora kulipa yote wala sio dharau tena hiyo ndio nzuri zaidi
 
ulipe yote kwani ushaingiza chombo ndani????lipa robo tu,hiyo iliyobaki unaimalizia baadae,uchmba ukivunjika je???
 
Kwetu USKUMANI niheshima ya mwanaume kulipa mahari zote lakini sio lazima na inategemea na familia. sijui kwingine.
Lakini mimi ningeshauri ulipe mahari yote kama unauwezo wa kulipa.
Huwa ni vizuri kulipa mahari zote na hiyo hufungua baraka katika familia yako.
Jitahidi kwa namna yoyote ile ulipe yote.
 
Back
Top Bottom