Ukuaji wa mziki wa Afrika. Hakika tunakua na kusonga mbele

LUKAMA

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,081
1,271
Habari za kazi wa kuu katika jukwaa langu pendwa, kwanza natoa pole kwa member wote kwa kuondokewa na mtu muhimu katika jukwaa hili warumi simfaham sura ila kwa taarifa nilizo pata ni home boy kabisa.😭😢
Mimi nimdau wa mziki wa Afrika wa kizazi kipya kwa kitambo kirefu toka miaka ya 90 mwishoni hadi sasa, sana napenda hiphop ila leo naomba tushili kuzungumzia mziki wa afrika wa kizazi cha sasa kwa mjumla.
Kwa kipindi hicho ukisiliza mziki wa kizazi kipya unaoneka muhuni ila sasa unasikilizwa na kila lika, kabla ya sasa ilikuwa ukisiliza mziki toka amerika sana hiphop ulikuwa unaonekana mjanja sana katika kumbukumbuza zangu kukiwa na matukio kama mwaka mpya au chrismas mimi na vijana wezangu tulikuwa tunatoa radio kaseti nje tuna bang usiku kucha kusikiliza na kucheza nyimbo za kina 50 cent, dmx (R.I.P) n.k
Ila Mungu mkubwa leo hii Africa to the world kweli mambo yanaenda kasi sana naamini miaka 5 ijayo billboard itachafukwa na wasanii kutoka afrika
Tukirudi nyumbani leo hii unaweza fungulia radio au tv playlist yote ni mziki wa afrika hakuna sijui wakina lilbaby sijui mwengine anajita uzi na mwengine dume kabeba mimba hatasijuie nisemaje, ila nafurahi kuona mziki wetu umebadilika na unakua
Kuazia gosple hata kama tunaimba kizungu au tuna copiana sisi kwa sisi ila mziki unatoka africa unaenda huko kwao na wanaukubali. Ninapo ona clip za wabeba ma-box zina zagaa wakicheza mziki wetu huko kwao na wanaupenda mziki wetu nafurahi sana, culture yetu inaenda kwao mimi na enjoy sana
Nipende kuwapongeza wasanii wote wa tz na africa mashariki wakongwe na chipukizi walio ufikisha mziki hadi hapa tulipo, najua wote amuwezi kuwa alikiba, mondi au marioo ila kila mtu kwa nafasi yake nawapongeza.
Leo hii mziki ni ajila na unabadilisha watu maisha nijambo lakupongeza 🔥🔥🔥🔥
#afrika to the world
Mtanisamehe sijui kutofautisha kati ya r na l kwenye uandishi pia sio mwandishi mzuri ila kwakua ni jukwaa huru nimeona niwasilishe kilicho kichwani mwangu
 
KWELI MKUU HUWEZI AMINI HADI SASA WALIOMPIGA RISASI MH LISSU HAWAJULIKANI
 
suluhisho ni katiba mpya tu ndu muandishi hakuna namna.....
 
Back
Top Bottom