Amapiano waachiwe wa Afrika Kusini ndio wanaziweza Bongo na Naija wanapiga makelele tu!

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,026
12,326
Hizi Amapiano toka zilipo anza kuvuma South Africa na wasanii wengi wa Afrika kuanza kuzifanya Wasauzi wamebaki kuwa watabe wa huu mziki.

Wasanii wengi wa nje ya South Africa wanaofanya na wanao jaribu kufanya Amapiano ni kama wanapiga makelele tu hapa nawazungumzia hasa wabongo na Wapopo.

Amapiano za Wabongo na Wapopo wanazichanganya na mabongfleva na maafrobeat mpaka ladha halisi ya Amapiano ina potea kabisa zinabakia kelele.

Wasauzi wanapiga Amapiano kismooth fulani hivi mpaka unafurahi ukikutana na DJ aliepangilia Amapiano za Kisauzi na mwengine anapiga za kibongo na kipopo utofauti wa ukali wa Amapiano ndio utauona.

Ata dance moves za kiamapiano za Wasauzi zipo smooth tofauti na Wabongo na Wapopo maguvu mengi mpaka jasho.
DJ-Zinhle.jpg

Unaweza taja Amapiano zako kali kutoka kwa wasouth unazo zielewa hapa down ⏬
 
Muziki wa amapiano wa south hakuna wa kuufikia ni bora sana , Music ukiimbwa kwa ligha yake iliyoasisiwa nayo inakuwa na ubora wajuu, ukiimbwa kwa lugha nyingine unapoteza ladha

Kwa Mfano hiphop(USA) wasanii wengi wanarap kwa lugha zao duniani lakini zote hizo hazina ladha kama hiphop ya America, sikiliza maneno yanavyotamkwa na jinsi wanavyonata na biti inafurahisha sana , hata na rnb ni hivyo hivyo.
 
Hizi Amapiano toka zilipo anza kuvuma South Africa na wasanii wengi wa Afrika kuanza kuzifanya Wasauzi wamebaki kuwa watabe wa huu mziki.

Wasanii wengi wa nje ya South Africa wanaofanya na wanao jaribu kufanya Amapiano ni kama wanapiga makelele tu hapa nawazungumzia hasa wabongo na Wapopo.

Amapiano za Wabongo na Wapopo wanazichanganya na mabongfleva na maafrobeat mpaka ladha halisi ya Amapiano ina potea kabisa zinabakia kelele.

Wasauzi wanapiga Amapiano kismooth fulani hivi mpaka unafurahi ukikutana na DJ aliepangilia Amapiano za Kisauzi na mwengine anapiga za kibongo na kipopo utofauti wa ukali wa Amapiano ndio utauona.

Ata dance moves za kiamapiano za Wasauzi zipo smooth tofauti na Wabongo na Wapopo maguvu mengi mpaka jasho.
View attachment 2709181
Unaweza taja Amapiano zako kali kutoka kwa wasouth unazo zielewa hapa down
Kuna amapiano moja ya Facalistic inaitwa "TOBETZA" Aiseeeee... Wabongo wangeendelea Tu na singeli piano waachie watoto wa Mandela.. South ndo kina piano
 
Muziki wa amapiano wa south hakuna wa kuufikia ni bora sana , Music ukiimbwa kwa ligha yake iliyoasisiwa nayo inakuwa na ubora wajuu, ukiimbwa kwa lugha nyingine unapoteza ladha

Kwa Mfano hiphop(USA) wasanii wengi wanarap kwa lugha zao duniani lakini zote hizo hazina ladha kama hiphop ya America, sikiliza maneno yanavyotamkwa na jinsi wanavyonata na biti inafurahisha sana , hata na rnb ni hivyo hivyo.
Nakubali. Kizulu kinasound fresh kwenye Amapiano mpaka raha
 
Basata nao wamemezwa na upumbavu huu, mziki wetu uliokua unatutambulisha kama Taifa umepotelea wapi?,tuelewe Tanzania tulikua tunapiga muziki na wengine wanaiga, wakongo wametuiga sana mziki wetu ,waliiga hata upigaji wetu wa Ala kama solo, siwezi nikatembelea Langa na kusikiliza Amapiano, then nije Dar naye Tembo anapiga Amapiano it's craze
 
Ebwana lile dude la uncle waffles linaitwa Tanzania..last week nilikuwa pale longstreet capetown mtaa wa mapopo hilo dude lilinikosha kwakweli tena msauz kaisifia nchi yangu,, from beerhouse to bobs bar to souk to coco yaani clubs kibao lilikuwa ni hilo dude tu. Ukweli ni kwamba amapiano OG ya sauz ni muziki unaotengenezwa na sound engineers most of producers and DJs in south africa ni sound engineers. Amapiano bongo ni makelele tu ya s2kz hayawezi kupigwa hata MTV maana mixing ni uchafu na nyie mnaokesha kidimbwi chungeni sana maskio yanu maana mnasikiliza uchafu nyimbo hazina quality ni kelele uzeeni mtakuwa viziwi muanze kusumbua. Ushauri wangu tusiige wenzetu hawafanyi amapiano kutafuta jina wasauz muziki ni part ya maisha yao kila kona ukipita utakuta kwaya zinaperfom mitaani au vijana wanatumbuiza mitaani kila kona utakuta watumbuizaji wenye vipaji mitaani tu sasa bongo watu wanatafuta kiki tu.
 
Mkuu viota hivyo ulivyovitaja vipo safi sana, loooooo Bob's Bar, Cubana,...kwa S ....ni amapiano ya nguvu, tupige mziki wetu why tuige ya watu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom