Ukristo ni siasa ya kimwili na kiroho; Ukristo ni umoja; Kama Kristo na Mungu walivyo wamoja. Umoja katika Haki ya Mungu

Ukristo ni siasa ya kimwili na kiroho; Ukristo ni umoja; Kama Kristo na Mungu walivyo wamoja. Umoja katika Haki ya Mungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,047
Reaction score
79,390
Hamjambo!

Falsafa ya Yesu ni Mungu katika Ukristo haipo katika personality na ID. Wakristo huamini Yesu ni Mungu sio kwa sababu Mungu ni Mtu au alizaliwa na binadamu.

Uungu wa Kristo ni umoja wao katika baadhi ya Majukumu na utendaji.

Kwa wasioelewa, nitawapa Mfano rahisi,
Mwanamke na mwanaume wanapoungana katika utakatifu wa Ndoa huwa Mwili Mmoja. Lakini hiyo haimaanishi personalities zao zinaondoka au ID zao zinaondoka. Nope!
Mke hawi mume, na mume hawi Mke. Lakini wote huwa mwili mmoja lakini kila mtu na mwili wake.
Kinachozungumziwa hapa ni umoja katika Nia, malengo, mipango, hisia, upendo n.k.

Ukristo ni kuwa Wamoja katika Mungu.
Kupakwa mafuta na kuwa Masihi wa Mungu muumbaji.

Ukristo ni Upendo. Upendo ni umoja katika Uungu wa Mungu wetu unaotupa Haki ya kushinda Waovu na kuushunda Ulimwengu wa Mwili na roho.

Mamlaka ya Kristo haipo kwenye roho tuu Bali hata katika Mwili. Ndio maana ya kupewa Mamlaka mbinguni na Duniani. Ambapo ni Mamlaka ya rohoni(mbinguni) na Mwilini (Duniani).

Wakristo wasiohubiri Mamlaka ya haki Duniani wakijaribu kueleza mamlaka ya mbinguni hao sio Wakristo wakweli.
Kwa sababu Kristo hakai ndani yao. Kwa sababu kama angekaa ndani yao wangekuwa hubiri injili ya kweli ya kushusha mamlaka ya mbinguni(Rohoni) katika Dunia(miilini mwa watu).
Na injili inayozungumziwa na Haki na upendo wa Mungu aliyetuumba.
Kuishusha haki ya Mungu duniani.

Ufalme wa Mungu ni kuhubiri haki na kuhakikisha dhulma haitokei Duniani.

Wanaosema watu wahubiri habari za Mungu wakiwazuia watu wasikemee dhulma hao ni waovu na wahalifu.

Mungu hayupo mbinguni tuu.
Falsafa ya Mungu pamoja nasi ni haki ya Mungu duniani au kwa wanadamu.

Haki ya Mungu haipo tuu mbinguni(Rohoni) Haki ya Mungu IPO pia mwilini(Duniani)
Wanaosema haki itapatikana mbinguni ni waovu wanaozuia haki isitendeke Duniani.

Kupigania Haki kunaenda sambana na Umoja(Ukristo) ambao ni Upendo.
Hakuna haki bila Umoja(Upendo).

Shetani na vibaraka wake huleta mafarakano na utengano wa kijamii ili kuleta dhulma ndani ya jamii.
Divide and rule principles ni kanuni ya kishetani ili kuondoa umoja(upendo) ili kuondoa haki katika Jamii.

Jamii yoyote isiyo na Umoja(upendo) haiwezi kuwa na Haki.
Chuki, uonevu, dhulma ni sehemu ya wagawe uwatawale.

Yesu anasema;
Yohana 17:11
Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

Tunapozungumzia Kuipenda Nchi. Tunazungumzia Ukristo katika Siasa.
Kwa sababu hakuna upendo unaozidi upendo wa Mungu.

Kuipenda nchi(uzalendo) hutokea katika umoja katika Haki.
Umoja katika kuwashinda waovu na wenye dhulma.

Kristo anaposema amemnyang'anya Shetani funguo ya kuzimu. Anamaanisha Haki imeshinda Dhulma.

Unapojiita mzalendo hii no tafsiri ya kushinda dhulma na kutetea haki ya nchi yako na watu wako.
Kuwanyang'anya mafisadi funguo ya utawala.
Kunyang'anya wauaji na watekaji madaraka na kuwashinda. Huo ndio uzalendo.

Uzalendo hauletwi na mtu mmoja. Uzalendo ni matokeo ya umoja wa watu wanaoipenda nchi yao kukabiliana na waovu.

Mungu na haki yake huwalinda wenye Haki na wenye upendo wa kweli.

Wanaosema Watu wasichanganye Mungu na siasa ni Watu wenye Nia ya kudhulumu watu.
Mamlaka zinatoka kwa Mungu katika Haki yake.
Mamlaka isiyotoka kwa Mungu haitendi Haki. Na lazima tuiondoe. Na Mungu mwenye Haki ameahidi kulinda Watu wake.

Wenye Haki hawawezizidiwa Ujasiri na Waovu. Kwa sababu Ujasiri wa wenye Haki hutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini Ujasiri wa waovu hutokana na vitu visivyo na nguvu.

Wazalendo tusikubali kutumika wala kubebwa na upepo wa watu wenye maslahi Yao binafsi badala ya maslahi ya nchi.

Msikubali yeyote miongoni mwenu aonewe.
Kuomba ulinzi wa Mungu ni kuwalinda wale wanaonewa.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom