Ukraine: Wafungwa wenye uzoefu wa kijeshi kuachiwa ili wasaidie kupambania nchi yao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
Muendesha Mshataka Mkuu wa Serikali ya Ukraine ametangaza kuwaachia wafungwa wote wenye uzoefu wa kijeshi ili wasaidie kuipigania nchi yao

Baadhi ya wafungwa wameshaanza kuachiwa. Ili kuweza kupambana na majeshi ya Urusi ambayo yameendelea kupiga nchi hiyo

Aidha wanawake wa nchi hiyo wamesema hawataweza kwenda vitani lakini watapambana kwa kuchangia damu ili kuwanusuru majeruhi wa vita
===
Ukraine to free incarcerated prisoners with military experience to help with the war effort - General Prosecutor’s Office in Kiev.

Authorities will also take into account “military experience, honors and remorse”.

Among those already released are Dmitry Balabuh, jailed for murdering a civilian at a bus stop. Sergey Torbin, jailed for organizing attacks on civil activists
1645961405275.png
 
Duh so Kila kitu lazima uambiwe.. vingine unatumia macho Kuna na ubongo kufikiri..
Dalili zinaonesha Ukraine wanakwisha..
Oh ombeni yaishe mnajikuta wagum kazi kwenu
 
... linapokuja suala la kupigania nchi hususan dhidi ya uvamizi wa mafashisti kama Putin lazima kila aina ya sana na mbinu itumike. Nchi lazima ilindwe kwa njia yoyote ile.
Raisi wa Ukraine anafaa kusaidiwa na kupongezwa, ni shujaa wa karne hii.
anajua fika mpinzani wake ana nguvu kumshinda lakini amekomaa na anahamasisha raia wake kwa nguvu zote.
m
nimemkubali sana.
 
... Sana! Wale wanapigania nchi yao; wanapigania ardhi yao waliyopewa na Muumba. Hawapiganii chama cha siasa kusalia madarakani. Watashinda!
 
Hana ushujaa wowote sana sana anawapeleka raia wake kuuawawa.
 
... Sana! Wale wanapigania nchi yao; wanapigania ardhi yao waliyopewa na Muumba. Hawapiganii chama cha siasa kusalia madarakani. Watashinda!
Kitendo cha kukataa kukimbia na kupigana kufa na kupona ni ushindi mkubwa. Haijalishi watashinda au laah...hawa Ukraine ni washindi dhidi ya majambazi Russia
 
Nimependa sana hii, inafikia hatua mnaweka tofauti zenu za ndani pembeni, hamna cha sijui chama hiki au kile, au Simba/Yanga au serikali au upinzani, inakua muda wa kutetea bendera ya nchi, kutetea ardhi, kutetea watoto wenu, vizazi vijavyo visiandike historia mbovu kuwahusu nyie wa leo.
Kila mmoja chukua silaha, bibi, babu, shangazi, mjomba, vijana wote wa kike au kiume, jaza chupa za petroli, tupigane kwenye vitongoji vyote, milimani, mashambani, kwenye mitaroni, nyumba kwa nyumba, mlango kwa mlango, mahandakini, mapangoni aisei hadi raha......
Ndio kilimkuta Marekani kule Vietnam, wanajeshi wake walikufa hadi akakimbia maana ilifikia hatua ikawa hajui adui ni yupi.
 
Raisi wa Ukraine anafaa kusaidiwa na kupongezwa, ni shujaa wa karne hii.
anajua fika mpinzani wake ana nguvu kumshinda lakini amekomaa na anahamasisha raia wake kwa nguvu zote.
m
nimemkubali sana.
Huyu ni mwanaume wa shoka haswaa,hatishiki na mikwara yote ya Putini na ametoa upinzani wa kutosha kulingana na nguvu za anaepigana nae.
 
Muendesha Mshataka Mkuu wa Serikali ya Ukraine ametangaza kuwaachia wafungwa wote wenye uzoefu wa kijeshi ili wasaidie kuipigania nchi yao

Baadhi ya wafungwa wameshaanza kuachiwa. Ili kuweza kupambana na majeshi ya Urusi ambayo yameendelea kupiga nchi hiyo

Aidha wanawake wa nchi hiyo wamesema hawataweza kwenda vitani lakini watapambana kwa kuchangia damu ili kuwanusuru majeruhi wa vita
===
Ukraine to free incarcerated prisoners with military experience to help with the war effort - General Prosecutor’s Office in Kiev.

Authorities will also take into account “military experience, honors and remorse”.

Among those already released are Dmitry Balabuh, jailed for murdering a civilian at a bus stop. Sergey Torbin, jailed for organizing attacks on civil activists
View attachment 2132955
Kwani kwao hawana j.k.t na mgambo nao wasaidie saidie?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom