Ukosekanaji wa katiba chanzo cha mauaji Oct 29

Ukosekanaji wa katiba chanzo cha mauaji Oct 29

Kuna nchi hazina katiba lakini hawawezi kuwaua raia wao kinyama kama ilivyofanyika huku.
 
We mtoa mada ni kilaza sana we hawa wezi unawaachaje hawa walitakiwa watokomezwe hadi kizazi chao chote washukuru mm nilikua mkoa ambao vibaka kama hawa hawakujitokeza na mm ningesaidia kutokomeza hiki kizazi cha laana kwenye hii nchi
 

Attachments

  • Waliotumwa na kulipwa kuingia mtaani kutaka kuangusha Serikali Oktoba 29 inaelekea hawakupewa ...mp4
    1.7 MB
Huo ndio ukweli na bila katiba mpya wengi watapoteza maisha maana bila kuondoa haya majanga yaliyopo ya katiba mbaya tusubiri mabaya tu
Hata katiba nzuri haijilindi yenyewe. Kama Watanzania tutaendelea na ukondoo wetu, mazafakas wataisigina hata hiyo Katiba mpya na wataendelea kutuchinja au kutupoteza kadri wanavyopenda. Before you know it, nayo itakuwa “kijitabu” tu!
 
Nasikitika bro P unamuamini huyu Mama . Si mkweli! Angekuwa mkweli tusingefika hapa
Naomba usisikitike, kuna vitu vya ajabu anafanya ukidhani ni yeye kumbe sio yeye, yeye asili yake ni hii, Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... ila kutokana na IQ yake, yeye ni anafanyishwa, bila ya yeye mwenyewe kujua kuwa kuna baadhi ya mambo anashauriwa na washauri wake, they are not right, hivyo anaingizwa mkenge, na mfano mzuri ni ni hii kesi ya mchango uhaini, kwanza niliandika humu Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo

Kisha nikiandika Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Nikawatia matumaini PreGE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!

Tena nikasisitiza Pascal Mayalla: Kusema Tutakinukisha au kuandamana sio uhaini; nasema kama mwanasheria

Hivyo kuna vitu vingi tuu rais ameingizwa mkenge zikiwemo kusainishwa sheria batili!, ndio maana nilishauri kwenye nafasi ya urais, tusitegemee tuu zile sifa na vigezo vya kwenye ibara ya 63 ya katiba, pia tuongeze vigezo vya good IQ ambayo tutaipima kwa aptitude test ili rais wetu asiwe ni mtu wa average IQ, ili ikitokea akidanganywa, asidanganyike kiraisi!.

Sio wewe tuu aliyekosa imani na Rais Samia, hata Mbowe alikosa imani na Rais Samia, nikamshauri Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!

P
 
Huo ndio ukweli na bila katiba mpya wengi watapoteza maisha maana bila kuondoa haya majanga yaliyopo ya katiba mbaya tusubiri mabaya tu
Comodo dragon ni mmbishi ila akibanikwa vizuri ni kitoweo murua!
 
Ndyo maana mlienda kuitafuta katiba kwenye maduka ya simu? Mkaenda hadi kwa shilole kutafuta katiba mpya?
Yote ni Katiba mpya kila palipo na mkusanyiko wa watu wengi waahalifu hawawezi kukosa mbona CCM kuna mafisadi na Magenge ya Kialifu na Watu wema bado wamo CCM hiyo sio
Hoja hakuna maandamano ambayo yanakosa uhalifu
 
Inayohitajika ni Katiba ya Wananchi, sio katiba ya Samia...wahenga walisema sikio la kufa halisikii dawa
Katiba ya Samia ni jina tuu la katiba kama ilivyo katiba ya Warioba, katiba ile I get okay ingekuwa katiba ya JK, alipoingia JPM, ilikuwa alete katiba ya Magufuli, Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya! kwa bahati mbaya Mungu akamtwaa kabla ya kutupatia katiba mpya, hivyo sasa anayetupatia katiba mpya ni Rais Samia Suluhu Hassan, hii hii itakuwa ni katiba ya Samia!.

P
 
Yote ni Katiba mpya kila palipo na mkusanyiko wa watu wengi waahalifu hawawezi kukosa mbona CCM kuna mafisadi na Magenge ya Kialifu na Watu wema bado wamo CCM hiyo sio
Hoja hakuna maandamano ambayo yanakosa uhalifu
1. Mwamba yale hayakuwa maandamano, zile ni vurugu zilizoratibiwa kwa nguvu na zikashughulikiwa kwa nguvu.

2. Unakumbuka maandamano yenu mwaka 2024? Yale ndo yalikuwa maandamano, ajenda zilieleweka, mliandamana kanda zote na hakuna sisimizi aliyekufa.
 
Back
Top Bottom