Ukosefu wa fedha Liberia wakatisha likizo ya Wabunge

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1575447793898.png

Bunge la Liberia laitishwa kwa dharura Rais George Weah wa Liberia amewaomba Wabunge wa Bunge la nchi hiyo kukatisha likizo yao na kukutana kwa dharura kujadili mambo muhimu yanayolihusu Taifa hilo likiwemo lile linaloelezwa kuwa ni ukosefu wa fedha.

Taarifa iliyotolewa na Bunge la Liberia haijatoa taarifa zaidi kuhusu ombi hilo, lakini habari zisizo rasmi zinaeleza kuwa huenda Rais Weah anataka kuliomba Bunge kuidhinisha uchapishwaji wa Dola Bilioni 35 za nchi hiyo kwa ajili ya kulipa mishahara ya Watumishi wa Serikali katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu za mwisho wa mwaka.

Liberia imekumbwa tatizo la ukosefu wa fedha na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa Wabunge na Watumishi wa Serikali, ambao wamekuwa wakilalamikia kitendo cha kucheleweshewa mishahara yao ya kila mwezi.


Chanzo: Muungwana Blog
 
Ivi na Tanzania haiwezi kuprint ikapandisha mishahara?

Procedures zikoje?
 
Pesa haiprintiwi tu kama makaratasi ukifanya hivyo uchumi utaanguma vibaya sana utanunua mkate kwa 50,000.
Huyu jamaa amefail yani hakuna kitu
Ivi na Tanzania haiwezi kuprint ikapandisha mishahara?

Procedures zikoje?
 
Itabidi Arsene Wenger aende haraka kuokoa jahazi, Weah ataelewa haraka maelekezo kutoka kwa Mchumi Msomi Wenger.
 
Back
Top Bottom