Tanganyika's national anthem was inspired by the lyrics of a 19th century ruga-ruga war song.Habari zenu ndugu zangu, pole na majukumu ya kila siku, tafadhalini nina shida ambayo naamini naweza saidiwa humu jamvini, ninahitaji kujua ilikuaje tarehe 9 dec 1961, siku ya uhuru wetu sisi watanganyika, je uliimbwa wimbo wa Taifa la Tanganyika ? na kama ulikuwepo kuna mtu yoyote anaweza nisaidia hata verses zake hapa JF? najiona nisie na Nchi kwani siijui wimbo wa Taifa langu na pia hata bendera ya Taifa siioni ikipandishwa. Nisaidiene mistari ya nyimbo kama bado inakumbukwa.
mtakua mmenisaidia sana.
Asante sana na pia Mungu ibarikiTanganyika.
NAWASILISHA.
...wadau wanaoufahamu wimbo wa Taifa wa tanganyika watuwekee hapa jf. kama vipi watangaze tenda ya kutunga wimbo wa tanganyika,hakuna kulala karibia kitaeleweka... narudi bongo huku mwanakwerekwe ntadaiwa passport hivi karibuni...
Unaitwa God save our Queen!
God save our gracious Queen
Long live our noble QueenGod save the Queen!Send her victorious,Happy and glorious,Long to reign over us:God save The Queen!
Kama ingekuwa amri yangu ningeshauri ule wimbo wa "tazama raman utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka...." ni bonge la wimbo
Mbali na kuwa na wimbo wa taifa, Pia tuwe na Bendera yetu ya Tanganyika. Mimi napendekeza iwe na mchanganyiko wa rangi tano. Nyeusi (ikiwakilisha weusi wa asili ya watanganyika), Rangi nyekundu (kuwakumbuka babu zetu waliomwaga damu kwenye vita ya majimaji na ile ya kumuadabisha nduli Idi amini), Rangi nyeupe (kwa sababu Tanganyika imekuwa chachu ya kusaidia Amani na ukombozi wa nchi karibu zote kusini mwa afrika), Njano iwepo (kwa sababu bado ardhi yetu ina madini bwerere na gesi ya kutosha kuzalisha umeme) pia bendera inaweza kuwa na ufito wa kijani (kwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo kwa watanganyika).