Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Fred Mpendazoe, Lissu ni mzalendo, na ukweli anaosema utabaki kusimama.
Namna ulivyoponda hoja zake ni jinsi tu ya kujipendekeza ili mkia uote.
Sina hakika kama utaota.
Mtukuzeni tu yeye aketiye, lakini ukumbuke kuwa tatizo analoliongelea Lissu huzaliwa na hukua. Na kila linapokua huongeza zaidi scope ya waathirika. kila mtu akikumbwa, mtaanza kulialia.
Yupo yule aliyenyooshewa bastola, nadhani unamkumbuka. Kabla ya kuachishwa madaraka sina hakika kama angeweza kuongea kama baada ya kuachishwa. Kama lipo kwa wengine, wewe unachekelea ukidhani hayakuhusu ila yakifika kwako tutakisikia kilio chako, tena cha sauti ya kupaza kuliko wengine.
Nabakia kusubiri.
 
Hata wewe tunajua ni wa kanda ya ziwa. Kwa hali ilivyo sasa. naiona mantiki ya Nyerere kukataa makabila makubwa kupewa uongozi mkubwa. Halafu badala ya kujibu hoja za Lissu moja baada ya nyingine mnaishia kumsema yeye binafsi. Hivi mkia umeota? Maana tuliambiwa ninyi ni ng'ombe msio na mikia. Hata ukatibu kata mzee hajikupa tu?

Mpendazoe isaidie CCM kujibu hoja zote za Lissu na siyo kuleta porojo hapa.
 
Mheshmiwa Mpendazoe, shikamoo!! Kwa sasa nitajikita katika maana ya uzalendo.

Pengine baadae nitarudi kujibu hoja zako zingine. Nimeona msingi wa hoja yako ipo kwenye neno "uzalendo" hadi umehoji uzalendo wa Tundu Lissu (TL) uko wapi.

Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".

Kwa sababu binfasi, sababu za kisiasa, sababu za kutetea maslahi binafsi, watanzania wengi tena wengi wao ni wasomi wamekuwa wakipotosha maana ya neno "uzalendo". Wao kwenye neon "taifa" au "nchi" wanaweka neon "rais" kwenye definition ya neon uzalendo.

Mark Twain alipata kusema "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it". Pia Edward Abbey alipata kusema "A patriot must always be ready to defend his country against his government".

Hapa utaona utofauti kati ya nini mzalendo anapaswa kutetea; Je ni serikali (including rais) au Je ni nchi/taifa?

Serikali ni watu ambao wapo wema na wabaya lakini nchi/taifa lina misingi na miiko yake ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria, umoja, huduma bora za kijamii, amani nk. Je, anayoyafanya TL hata kuhoji uzalendo wake ana-defend nini? Unachofanya wewe Mpendazoe, JPM nk mna-defend nini?

Uzalendo ni "NDIYOOOOO" kwa kila afanyalo Rais hata kama linavunja msingi na mwiko wa taifa letu?

Uzalendo ni kuunga mkono chochote kilicho chema kwa taifa regardless kimefamywa na nani? Kinachopaswa kuungwa mkono ni MTU au KITENDO?

Itoshe kusema umemaliza . Asante
 
ahhahhaah.....Mzee mpendazoe pls nisaidie hawa jamaa wanatoka wapi.
1. Kamishina wa kodi,Mkurugenzi wa Reli,....................................
2. Wale wakuu wa wilaya kati yao 41 ......ni wasu...ma!!
3. Wakurugenzi 53 wa halmashauri wanatoka.....mhhh......
4. Hivi na yule wa ofisi ya rais utumishi ni ndugu au?.....

Halafu mzee mpendazoe,Usilinganishe CDM na Serikali...coz serikali ni kwa wananchi wote while chama ni kikundi cha watu.Ndiyo maana TL hakulalamikia akina salma na annie kupewa ubunge....au yule bwana kupewa unaibu katibu mkuu wa chama chenu......Sasa nisaidie kulinganisha ukabila/ukanda uliyopo cdm kuanzia akina mtei ....makani....slaa....mbowe.Halafu malizia chama chenu kuanzia mwalimu....(butiko...warioba).....mwinyi....(husein,mrisho).......ben....mrisho......pombe...
Ila naomba unisaidie kuwauliza cdm swali hili..."Wenje na masha waliteuliwa kugombea ubunge wa afrika mashariki kwa kuwa ,Wanatoka kanda ya ziwa,Uwezo wao AU kwa kuwa wameoa wachaga?.
Halafu waulize na hawa wa chama chenu swali hili..."Sofia na emmanuel walitenda kosa sawa,lakini sofia akahukumiwa jela,ila emmanuel akapewa ubalozi...hii ikoje,Kwa sababu emmanuel ni mkatol...ki na sofia ni mwis...mu au nini?.....pole pole
 
Kama kweli hicho ulichokiandika ndizo inazihita hoja basi kuna tatizo kubwa kwenye mfumo wetu wa elimu. Dr (PhD) huko ndiko kumjibu mtu kwa hoja!!.
Mtu amesema kuna ufamiliya,ukabila na ukanda katika uteuzi wa nafasi mbalimbali, akatoa ushahidi kuwa fulani na fulani uteuzi wao ni wa kifamiliya, akaongeza nyama kuwa huyu alikuwa afisa wa kawaida hakuwahi kuwa japo manager leo ni katibu mkuu wa fedha hiyo ni hoja, sasa wewe unakuja kuijibu eti rais ni baba wa makabila yote alafu unatamba eti umemjibu kwa hoja!.
Kaza buti mkuu njaa mbaya, vipi mkia unaendelea kuota?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kuwa mkongwe katika siasa za Tanzania,Umekuwa Mbunge kati ya nafasi za juu kabisa za utumishi wa kisiasa kitaifa,ila hoja zako na mihemko yako ni kama vile ndo kwaanza unavunja ungo kisiasa.Huna ulicho andika ni upuuzi uleule unaotukanwa nao kila siku.Huna impact hata robo kwa Taifa kama aliyonayo Tundu lisu ndiyo maana siku moja nilishakwambia hapa hapa jamii forum ni bora ukanyamaza ukabaki na heshima yako ndogo iliyobaki kwenye siasa za nchi hii kuliko huku kutafuta ukuu wa wilaya ambako kunamaliza heshima yako kabisa na hutaupata wenyewe walishakwambia huna mkia.Mbona mwenzio Msindai amenyamaza?ameshajua hakuna U DC kwa wazee tena wasio na mikia.
Umesema umesikiliza hotuba ya Tundu Lisu,kuna matusi kweli aliyotukana kama siyo kukosa hoja mfu?Kutoa maoni mbadala ya kile wanachowaza na kufanya watawala,tafsiri yake ni matusi?Kutetea uonevu wa serikali na vyombo vyake kwa vyama vingine vya siasa ni matusi?sasa soma huu uzi page kwa page ndiyo utaona matusi maana nauhakika hata wakwezako wapo humu na watakutukana.
 
Mpendazoe wewe habari yako ilishakwisha, nadhani unamendea uteuzi wa kuhurumiwa , ongeza jitihada kwani vacant post zipo bado
 
Mheshmiwa Mpendazoe, shikamoo!! Kwa sasa nitajikita katika maana ya uzalendo.

Pengine baadae nitarudi kujibu hoja zako zingine. Nimeona msingi wa hoja yako ipo kwenye neno "uzalendo" hadi umehoji uzalendo wa Tundu Lissu (TL) uko wapi.

Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".

Kwa sababu binfasi, sababu za kisiasa, sababu za kutetea maslahi binafsi, watanzania wengi tena wengi wao ni wasomi wamekuwa wakipotosha maana ya neno "uzalendo". Wao kwenye neon "taifa" au "nchi" wanaweka neon "rais" kwenye definition ya neon uzalendo.

Mark Twain alipata kusema "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it". Pia Edward Abbey alipata kusema "A patriot must always be ready to defend his country against his government".

Hapa utaona utofauti kati ya nini mzalendo anapaswa kutetea; Je ni serikali (including rais) au Je ni nchi/taifa?

Serikali ni watu ambao wapo wema na wabaya lakini nchi/taifa lina misingi na miiko yake ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria, umoja, huduma bora za kijamii, amani nk. Je, anayoyafanya TL hata kuhoji uzalendo wake ana-defend nini? Unachofanya wewe Mpendazoe, JPM nk mna-defend nini?

Uzalendo ni "NDIYOOOOO" kwa kila afanyalo Rais hata kama linavunja msingi na mwiko wa taifa letu?

Uzalendo ni kuunga mkono chochote kilicho chema kwa taifa regardless kimefamywa na nani? Kinachopaswa kuungwa mkono ni MTU au KITENDO?
Wewe ni mjuvi wa kiwango cha lami. Umesoma ukaelimika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisikiliza hotuba ya Mh Tundu Lissu aliyoitoa huko jimboni kwake akimshambulia Mh Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania JPM kwamba ni dikteta uchwara, ni mkabila na anaendesha nchi kwa upendeleo.

Ameomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania na waizomee Tanzania kutokana na uongozi mbaya wa JPM unaogandamiza demokrasia nchini. Mh.Tundu Lissu alionyesha hasira na dharau kubwa kwa Rais wakati akitoa hotuba hiyo.

Kwanza nianze na masuali ya jumla :

Mimi ninajiuliza, je Mh Lissu na viongozi wengine wa upinzani hawawezi kabisa kuikosoa Serikali bila kutumia matusi na kejeli ? Je hawawezi kabisa kutoa maoni yao bila kutoa matusi na kejeli kwa viongozi waliopo madarakani?

Pamoja na Elimu aliyonayo Mh Tundu Lissu haelewi kwamba Mh John P Magufuli amechaguliwa na wa Tanzania na ni kiongozi wa Nchi na lugha anayoitumia dhidi yake inalidhalilisha Taifa ?

Naomba nitazame hoja za Mh Lissu.

1. Madai kuhusu demokrasia kuminywa na haki na Uhuru wa kutoa maoni. Wakati Mh Lissu anadai haya kwa Serikali iliyopo madarakani angewatetea wanachadema kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni na demokrasia ndani ya Chadema. Mfano Lowassa alishindanishwa na nani wakati wa kugombea urais 2015.

Sikumsikia Mh Lissu akimuijia juu Mbowe wakati alipobadilisha gia angani. Wengi watakumbuka uchaguzi wa viongozi wa jumuia za Chama ndani ya Chadema ulivyokuwa umegubigwa na ubabe kwa kisingizio cha maslahi mapana ya Chama. Mh Lissu alikaa kimya.

Dk Slaa aliondolewa kwenye kugombea urais ndani ya Chadema kibabe, Mh Lissu alitetea ujio wa Lowassa. Mh Lissu na Chadema haiwezi ikawa msemaji wa kudai demokrasia nchini wakati ndani ya Chadema kuna udikiteta ulipitiliza.

2. Kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni. Uhuru na haki hiyo haijazuiwa isipokuwa lipo tatizo kubwa upande wa Lissu na wengine kwenye upinzani. Wakijenga hoja na kutoa maoni yao bila matusi sidhani kama watakatazwa.

Hakuna jambo linalokera na kuudhi kama lugha zinazotumiwa Mh Lissu na baadhi ya wapinzani. Watambue pia kama wao walivyo na haki ya kutoa maoni pia Rais nae ana haki zake kama kiongozi wa Nchi. Haikubaliki mtu atumie lugha ya kejeli, dharau, na matusi kwa Rais na kiongozi wa Nchi kwa kisingizio cha haki na Uhuru wa kutoa maoni. Hapana.

3. Lissu amezungumzia suala la ukabila na upendeleo wa kiukoo. Inasikitisha na ni hatari sana kwa kuanza kuleta hoja za ukabila na ukoo au undugu au udini. Ni kweli JPM analo Kabila lake, ukoo wake wa kuzaliwa na dini yake. Lakini JPM kama Rais, ni baba wa Tanzania wote.

Na koo zote ni zake, watumishi wote ni wake, na wanajeshi wote ni wake. Hivyo, Mh Rais anayo haki ya kumchagua yeyote katika nafasi yoyote anayemwona ataweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake bila kujali alikotoka au dini au kabila au ukoo au hata Chama.

Hivyo, hoja alizozitoa Mh Lissu kuhusu ukabila au ukanda ni matatizo yake ya kifikra. Wengine hawaoni kama anavyoona yeye Mh Lissu. Mh Lissu ndiye mwenye ukabila, udini, na ukanda. Watanzania wengi wameondokana na fikra hasi alizonazo Mh Lissu. Inawezekana, hoja za ukabila, ukanda, udini na ukoo bado zipo Chadema.

4. Mh Lissu ameiomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania. Ni jambo La kushangaza kweli! Moja ya viongozi wanaozungumzwa duniani kuhusu uongozi bora ni Rais JPM. Jitihada za Rais JPM katika kupiga vita rushwa na ufisadi zinaonyesha matunda.

Kama Chadema ilikuwa imedhamiria kweli kupiga vita rushwa na ufisadi inatakiwa imuunge mkono Rais JPM. Lakini cha kushagaza kabisa Mh Lissu kuhusu suala la ufisadi amekuwa kimya tangu Chadema wampokee Lowassa. Mh Lissu tangu wakati huo alibadilika.Mh Lissu aligeka jiwe.

Mh JPM anapigania kwa dhati utajiri wa Nchi yetu ili uweze kuwanufaisha watanzania wote. Mh Lissu na hili limemkera mpaka anaombea Tanzania ishitakiwe na makampuni yanayochimba madini nchini !

Mh Rais JPM anapambana kwa dhati na uzembe na ubadhirifu kwenye mashirika ya umma na Serikali, Mh Lissu na hili linamkera kwani alishasema atawatetea wale wote wanaotumbuliwa ! Very sad. Kwa juhudi hizi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5 bado Mh Lissu anashawishi nchi na Jumuiya ya Kimataifa ziisusie Tanzania na kuinyima misaada! Inasikitisha sana.

Uko wapi Uzalendo wa Mh Lissu kwa Nchi yake ?
Mimi ninaamini Mh Rais anastahili kuungwa mkono kwani ameonyesha kwa dhati anatetea wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sitegemei wa kanda ya ziwa aandike tofautu ni ulivyoandika mheshimiwa...
NILITEGEMEA UJIBU HOJA KWA HOJA.... mfano,
1. Aliposema mtoto wa dada, wewe weka hoja kama si mtoto wa dada au la
2. Aliposema fulani ni wa kanda ile, we ungeweka hoja kuhusu hilo

Ukiandika kwa ujumla hivyo unaonekana hujibu hoja za Lissu
 
Inashangaza sana mtu Mzima kama Fred MPENDAZOE kumlaumu Tundu lisu eti sio mzalendo.Napenda kumwuliza Mzee Wa KUHAMAHAMA VYAMA Bw.Fred MPENDAZOE angetuambia UZALENDO wake kwanza ndio amlaumu Tundu Lisu.Kama Fred MPENDAZOE ungekuwa Mzalendo naamini ungesimama kwenye Chama kimoja ukauonyesha huo UZALENDO.Wewe ni mtu Wa kutafuta ukubwa ndio UZALENDO wako.Naamini hata huko uliko ulitegemea utapokelewa Kwa kupewa Cheo na ninakuapia hata ukiomba uongozi hutapata wewe ni Ng'ombe kakatika mkia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
OK let's assume Tundu Lissu Sio mzalendo kwa hayo aliyoyaongea hapo, vipi kuhusu Mkapa? aliyeuza na kubinafsisha mashirika na rasilimali za taifa hili kwa bei chee ?,vp Jk na madudu yake yoote yale kuanzia IPTL hadi ESCROW? vp mzee wa kivuko cha Bagamoyo?,na wale samaki Wake?,Nyumba za serikali?,vp yule mzee anayezeeka vibaya mzee wa ruksa na uuzwaji wa mbuga ya loliondo kwa waarabu?,
Nadhani kwa concept yako ya uzalendo atleast Lissu kaongea hajatenda kuliko hao waliotufanya vibaya na bado unawahesabu kama wazalendo
 
Back
Top Bottom