Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Ng'ombe aliekatwa mkia katika ubora wake.. Kumbuka lakini ni mjusi tu ndie anaeota mkia baada ya kukatika, na sio ng'ombe.. Endelea kutetea kuminywa kwa demokrasia, kukamatwa ovyo kwa wapinzani na tuone kama mkia utaota huo..

Haya unayomsema nayo Lissu, ndio hayo uliyokuwa unayasema kwenye kampeni zako za kugombea ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, ukapigwa bao na sisiemu.. Wewe ni mnafiki wa kiwango cha makanikia..
Umeuburudisha moyo wangu khasbuhi ya leo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Porojo nyingiii. Hakuna hata sehemu moja umejibu hoja za Lissu.
Nachokiona hapa ni kujaribu kugeuza tu kibao. Hizo nchi wahisani bila hata kuambiwa na mtu wao wana means zao za kupima mambo....uhuru wa maoni/upashanaji habari, demokrasia, vita dhidi ya rushwa,ubadhirifu na ufisadi, nk.

Kama unaona JPM anafanya vizuri kwenye vita dhidi ya rushwa/ufisadi/ubadhirifu, basi mwenzio Lissu anaona JPM hafanyi vizuri kwenye demokrasia, uhuru wa maoni na utawala bora. Vigezo vya kuendelea kuwa na usaidizi toka kwa hao wahisani sio vita dhidi ya rushwa na ufisadi tu.

Ni pamoja na hayo mengine. Hata JK aliyefanya vizuri katika kukuza demokrasia, kibao kilimgeukia mwishonimwishoni kwenye issue ya Tegeta Escrow, na matokeo yake unayajua.

By the way, Fatuma Karume kaeleza vizuri tu...kuwa huo uchochezi wa Lissu ni upi? Maana ili uwe uchochezi lazima uonyeshe wazi kuwa fulani alimchochea fulani ili huyo aliyechochewa atende JINAI fulani.

Sioni popote Lissu alipomchochea yeyote ATENDE jinai....alichofanya ni kuwakumbusha watu kutokubali utawala wa kidikteta na uvunjaji wa katiba. Hapo hakuna jinai.

Ni sawa na nyimbo tunazoimbiwa na watawala kila siku kuwa tuilinde amani, umoja na mshikamano na tuwaepuke wanataka kutupotezea amani. Likewise hakuna tatizo mtu mwingine akitukumbusha kuukataa udikteta.
 
Nashangaa mzee mkapa ametutukana tena zaidi ya mara moja lkn yupo tu....
Aah Fred Mpendazoe katika ubora, sasa mngemjibu kwa hoja, Hoja inajibiwa kwa Hoja, Lissu kaongea mengi ambayo watz tulikuwa hatujui na hasa sie wa vijijini, sasa ilitakiwa 1 huko Lumumba asimame nae amjibu sasa wananchi tungewaelewa kuwa mchele ni upi na pumba ni zipi.

Lakini mkimkamata na kumuweka jela na kumnyima dhamana, hapo mnajenga chuki, mngemjibu kwa hoja kama polepole anavyojibu watu kwa hoja tunaomuelewa tunamuelewa na wasiomuelewa ndio hivyo lakini amejibu hoja, kitendo cha kumuweka ndani wananchi tutaamini kuwa yaliyosemwa na Lissu ni kweli.

Nadhani umeona kauli ya yule mwanasheria aliyekwenda jioni japo atoe dhamana aachiwe aende kwenye mkutano, lakini askari wamegoma na kusema wanasubiri maagizo kutoka kwa wakubwa.

Je Dotto ni Mpwa wa JPM??
Je deputy wa Dotto ni Mpwa??
Magufuli ameajiri mkuu wa tume ya uchaguzi, kwao
Magufuli aneajiri mkuu wa polisi wa kwao
Mkuu wa majeshi wa kwao
And the list goes on and on......

Again; expert permits wamepewa wakatoiki tu wengine wamekataliwa
Wapinzani wakifanya mikutano hushikwa, hupigwa na kuwekwa ndani, CCM wanapeta

Yote hayo kweli si kweli?

If that is true, then that is nepotism

Kama si kweli Tundu ni sawa na mlevi
 
Je Dotto ni Mpwa wa JPM??
Je deputy wa Dotto ni Mpwa??
Magufuli ameajiri mkuu wa tume ya uchaguzi, kwao
Magufuli aneajiri mkuu wa polisi wa kwao
Mkuu wa majeshi wa kwao
And the list goes on and on......

Again; expert permits wamepewa wakatoiki tu wengine wamekataliwa
Wapinzani wakifanya mikutano hushikwa, hupigwa na kuwekwa ndani, CCM wanapeta

Yote hayo kweli si kweli?

If that is true, then that is nepotism

Kama si kweli Tundu ni sawa na mlevi
u nailed it mkuu
 
Yani nikajua unajibu hoja za Lissu lakini cha kushangaza unaanza kumzungumzia mbowe na mambo ya chadema ,hivi chadema ndio inaongoza nchi!?!?
Unahoji uzalendo wa lissu unajua maana ya uzalendo!?!?
Jibu hoja anacho sema Lissu ni sahihi, kwanini?
anacho kisema Lissu si sahihi, kwanini?
sasa wewe umeleta blablabla nyingi na kuingiza mambo ya uchama ndani.
 
Wameishiwa hoja wamechanganyikiwa na kutapatapa.

JPM muarobaini wa wapinzani😀.
 
Mpendazoe,ni lini taifa hili tuliacha kutambulishana kikabila au kikanda?umesahau uzanzibari na utanganyika?Mbona tukienda kutibiwa wakati wa kuandikishwa tunaulizwa kabila gani?Umesahau ukihojiwa polisi unaulizwa kabila na dini yako?Tusiaminishwe visvyokuweko.
Kwanini viongozi wachague lugha ya kuisikia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri ungetoa list ya hayo matusi ningekuelewa zaidi. Kuwa baba wa familia haimaanishi uchague watoto wa kuwapenda, baba bora ni yule anayetoa fursa sawa kwa watoto wake.
 
Mheshimiwa achana na lisu maana hata mkuu alisema lisu ni ng'ombe asiye na mkia, ila kusema dr slaa alitolewa kugombea uraisi hapo napingana na wewe kwani dr hakuchukua fomu popote ya kugombea uraisi
 
Back
Top Bottom