Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Fred tuambie Lissu katukana tusi gani? Udikteta uchwara ni tusi au sifa
Huyu mzee ningependa nijue kwanza elimu yake! Maana hakuna alichoandika! Kaangalia upande mmoja tu wa shilingi! Upande wa pili hakuandika. Katika kuandika, lazima utoe strengths and weakness of other sides! Sasa yeye kaongelea lissu pekee, akasahau upande wa pili.
In short, andiko lake limeangukia kwenye fallacy bias!
 
Mzee wewe hata ufanye nini huaminiki tena, CCM, CCK, CHADEMA, CCM umeshakatwa mkia, japo home boy lakini endelea tu kusugua bench.
 
Uko wapi UZALENDO wako wewe Fred Mpendazoe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkia bado haujaota [emoji3]
Mpendazoe,ni lini taifa hili tuliacha kutambulishana kikabila au kikanda?umesahau uzanzibari na utanganyika?Mbona tukienda kutibiwa wakati wa kuandikishwa tunaulizwa kabila gani?Umesahau ukihojiwa polisi unaulizwa kabila na dini yako?Tusiaminishwe visvyokuweko.
Kwanini viongozi wachague lugha ya kuisikia?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawashangaa sana wananchi, wachumi, viongozi wa dini na wanasiasa wa Tanzania. Naomba tutafakari pamoja yafuatayo na kisha, pamoja na maoni yangu, tujibu maswali yatakayofuata:

Section A (Sehemu ya kwanza)
Phase I (Awamu ya kwanza) (November 2015-June 2017)
Rais: Haiingii akilini kwa nchin yetu kutegemea misaada. Sisi tuna kila kitu, hatupaswi kuendesha nchi yetu kwa kutegemea
misaada. Kwanza hii misaada ina masharti mengi, na masharti mengine yanakwenda kinyume na utamaduni wetu.
Katika kipindi changu cha uongozi sitategemea misaada. Tunatakiwa sisi tukopeshe na kusaidia mataifa mengine na
siyo kusaidiwa. Misaada inatweza utu wetu.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Tanzania tumempata Rais tuliyemhitaji tangu zamani. Tumechoka
na uhuru wa bendera. Tunatakiwa kujitegemea maana tuna kila kitu. Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada
ambayo wakati mwingine inatweza utu wetu. Hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa kutegemea misaada. Huyu
anayekataa kuongoza nchi kwa kutegemea misaada anatufaa sana! Tumuunge mkono. Tanzania tuna kila raslimali na
ni aibu kutegemea misaada.

Phase II (Awamu ya pili) (July 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kinyume na Katiba. Kuna ukandamizaji mkubwa wa demokrasia nchini. Nchi haifuati mfumo wa vyama vingi. Vyama vya upinzani vinazuiwa kufanya shughuli za siasa. Viongozi wa upinzani wanakamatwa ovyo bila sababu maalumu. Jeshi la polisi, wakuu wa wilaya na mikoa wanatumika kukandamiza demokrasia ya vyama vingi. Mihimili mingine ya dola inadharaulika na kunyimwa uhuru wao. Uhuru wa kutoa maoni nchini umekosekana. Serikali inatumia fedha za kodi zetu na misaada kukandamiza demokrasia. Kwa hali hii tutaomba jumuiya za kimataifa ziinyime Tanzania misaada kwani inatumika vibaya kuminya demokrasia nchini.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Huyu Lissu haitakii mema nchi. Hatuwezi kuendesha nchi na kuwahudumia watu wetu bila misaada toka nje. Mtu anayetaka kukwamisha misaada hatufai, apuuzwe kabisa. Msaada ndio nguzo ya maendeleo yetu. Hivi tukinyimwa misaada ataumia Lissu au Rais? Watakaoumia ni wananchi. Nchi haiwezi kwenda bila misaada.

Swali: Unapata picha gani ya wasomi, wananchi, wanasiasa na wachumi wa Tanzania?

My take: Kinachoungwa mkono Tanzania siyo nguvu ya hoja bali nani katoa hoja.

Section B (Sehemu ya pili)
Phase I (Awamu ya kwanza) (Julai 2015-Juni 2017)
Mkapa: Watanzania acheni kulialia. Watanzania ni wapumbavu na malofa.
Itikio la viongozi wa dini: Kimyaaaaaaaaa

Phase II (Awamu ya pili) (Julai 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kidikteta. Huyu kiongozi wetu ni udikteta. Udikteta uchwara umetamalaki nchini. Tuupinge kwa nguvu zote, viongozi wa dini wapinge na kila mtu kwa nafasi yake apinge maana hakuna aliye salama.

Itikio la viongozi wa dini (hasa kupitia msiba wa mke wa Mwakyembe): Hatutaki lugha za kuudhi na kuwakejeli viongozi wetu. Hatutamuunga mkono anayempinga Rais wetu na kumtolea lugha za kuudhi au matusi. Hiyo tabia ikome.

Swali: Unapata picha gani ya viongozi wa dini nchini?

My take: Tangu enzi na enzi viongozi wa dini (mafarisayo na masadukayo) wamekuwa upande wa tabaka tawala. hawajawahi kuwa upande wa wanyonge. Pia watu hawa hawakemei ubaya wa dhambi bali huangalia nani kafanya dhambi ndipo wakemee.
 
Hivi wanyonge nchi hii wanapatikana mkoa gani? Tumekumbatia unyonge na kuuvaa kama vile ni kitu cha kujivunia... utasikia raisi wa wanyonge,.. nimejitoa mhanga kuwatetea wanyonge. Nchi huru halafu tunajiita wanyonge? Mababu zetu na baba zetu walipigania nchi hii iwe huru ili kuondoa unyonge iliosababisha tutawaliwe, leo bado tuna raisi wa wanyonge? Ukiniambia nchi hii bado ina wajinga nitakubaliana na wewe lakini siyo wanyonge, tusichanganye mambo.
 
SIKU HIZI KUMWAMBIA KIONGOZI AFUATE SHERIA NI UCHOCHEZI?
Mpenda zoe jifikirie
 
HESHIMA KUU MPENDAZOE!
Binafsi mimi naamini katika ushindani hasa katika kuleta maendeleo na ningekuwa na uwezo ningefanya tafiti yenye hypothesis ya "Hakuna tofauti katika maendeleo kwenye mfumo wa chama kimoja na vyama vingi"
Nirudi kwenye hoja zako na kwa ufupi tu nijaribu kukuzindua,
  • Demokrasia-Umemlaumu Lissu kuwa hapiganii demokrasia ndani ya Chama chake lakini anapigania demokrasia ndani ya Taifa-Hili halihitaji elimu kubwa ili nitakusaidia kukuuliza impact ya uvunjaji wa demokrasia katika chama ambacho sio tawala na kuvunja demokrasia ndani ya serikali (yenye jeshi,polisi,vifaru ndege,shushushu n.k).Katika hilo pia umezungumzia Slaa kuondolewa kibabe,si kweli Gwajima alijibu,TUndu Lissu akaeleza,CCTV camera zikaonyesha waliomkaribisha Slaa kwenye pess conference,tuseme zaidi?
  • Uhuru wa kutoa maoni-Hapa umezungumzia lugha ya kuudhi-Naomba nikuulize ni nani aliyetumia lugha ya kuudhi zaidi kati ya aliyosema Lissu na yule aliyezungumza Bukoba akiwatuhumu watu kwa majanga ya asili?Vipi kuhusu watoto wa wenzio kuwa vilaza, Vipi "waliochukua pesa itawatokea kwenye mahali popote palipo wazi mwilini?"
  • Ukabila na upendeleo-Hapa sitii neno lakini Lissu alitaja watu kwa majina na unasaba wao kwa Mkuu kwa nini umeshindwa kupangua hii?Nakukumbusha ya kuwa ukabila na ukanda ulianzishwa na walio madarakani katika kuvunja nguvu upinzani-CUF-Waislamu,CDM wachaga na northerners.Yote ilikuwa katika kupata ushindi lakini hatukujua kama tunapanda mbegu.
  • Kuhusu uzalendo na kupigania nchi-Hili halina shaka ya kuwa JPM amejaribu lakini bado yeye alikuwa sehemu ya uozo wote huu na hii inampunguzia sifa ambayo unataka apate leo.Lakini pia Mkuu alikuwa ujenzi na mpaka leo hakujatokea majipu huko,hili nalo unalionaje?
Tumuunge mkono Raisi wetu kwa kusema yale tunayoona kuwa hayaendi sawa naye atusikilize arekebishe au autuelimishe pale tulipokosea.Tusimuunge mkono katika yale ambayo tunaamini ya kuwa kwa asilimia kubwa kakosea.
Chuki dhidi ya upinzani iko wazi mno na hili si jambo jema!!!
 
Wewe ng'ombe usio kuwa na mkia, nakuuliza hivi uzalendo wenu upo wapi nchi inakosa misaada ya mcc mingine mingi mwaka wa pili mful

Sent from my HUAWEI MT7-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Kwa taarifa yako, huyu mnafiki kwa sasa anachukiwa sana na watanzania, kila mtanzania anajua jinsi anavyotumika na wazungu.
Wenye akili kama yako ndo wanaamini kuna mtu anatumiwa na wazungu.Mzungu gani mwenye time na nchi omba omba? Nchi yenye viongozi wasio na plan ya kuiona nchi yetu ikijitegemea hata kwa siku moja?
 
Mpendazoe kwa umri wako hoja hii unajidhalilisha sana. Hujielewi umesimamia wapi zaidi ya kuonyesha unafiki na uchumia tumbo tuu.

Lissu ametoa hoja ambazo zilihitaji majibu na sio kusema katukana, kamtukana nani? ona hata Polisi wamechoka ndio maana wanatoa majibu kuwa NI AMRI TOKA JUU.

Hiyo kauli ukiiangalia kwa jicho la tatu ni kama kusema sisi hatuoni kosa la huyu lakini aliyeko juu ndio katoa amri.

Jambo ambalo ni kinyume na katiba na haki za kiraia. Wewe kaa kimya tuu, umejichujia na huna hoja yeyote zaidi ya njaa.
Siyo kosa lake, huyo mnafki huwa namuona mara kwa mara Kinyerezi mwisho kwa hakika jamaa amechoka ile mbaya na kaunda suti anazovaa ndio hizohizo.

Usiombe upigike uzeeni hamna namna ni lazima ajikombe ili akumbukwe lakini tatizo hana mkia.
 
Kwa taarifa yako, huyu mnafiki kwa sasa anachukiwa sana na watanzania, kila mtanzania anajua jinsi anavyotumika na wazungu.

Hata Yesu alichukiwa na wayahudi kwa kuwaambia ukweli. Kama Lissu atachukiwa na watanzania wote kwa ukweli ule aliouongea ni bora achukiwe tena sana. Na iwapo cdm utachukiwa na watanzania kwa ukweli wa Lissu ni bora ichukiwe hata ikibidi kufa ife. Ukweli hauhitaji support hata ukibaki peke yako.
 
Swali kabla ya kujibu. Upo wapi uzalendo wa kiongozi asiyeheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Nawashangaa sana wananchi, wachumi, viongozi wa dini na wanasiasa wa Tanzania. Naomba tutafakari pamoja yafuatayo na kisha, pamoja na maoni yangu, tujibu maswali yatakayofuata:

Section A (Sehemu ya kwanza)
Phase I (Awamu ya kwanza) (November 2015-June 2017)
Rais: Haiingii akilini kwa nchin yetu kutegemea misaada. Sisi tuna kila kitu, hatupaswi kuendesha nchi yetu kwa kutegemea
misaada. Kwanza hii misaada ina masharti mengi, na masharti mengine yanakwenda kinyume na utamaduni wetu.
Katika kipindi changu cha uongozi sitategemea misaada. Tunatakiwa sisi tukopeshe na kusaidia mataifa mengine na
siyo kusaidiwa. Misaada inatweza utu wetu.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Tanzania tumempata Rais tuliyemhitaji tangu zamani. Tumechoka
na uhuru wa bendera. Tunatakiwa kujitegemea maana tuna kila kitu. Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada
ambayo wakati mwingine inatweza utu wetu. Hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa kutegemea misaada. Huyu
anayekataa kuongoza nchi kwa kutegemea misaada anatufaa sana! Tumuunge mkono. Tanzania tuna kila raslimali na
ni aibu kutegemea misaada.

Phase II (Awamu ya pili) (July 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kinyume na Katiba. Kuna ukandamizaji mkubwa wa demokrasia nchini. Nchi haifuati mfumo wa vyama vingi. Vyama vya upinzani vinazuiwa kufanya shughuli za siasa. Viongozi wa upinzani wanakamatwa ovyo bila sababu maalumu. Jeshi la polisi, wakuu wa wilaya na mikoa wanatumika kukandamiza demokrasia ya vyama vingi. Mihimili mingine ya dola inadharaulika na kunyimwa uhuru wao. Uhuru wa kutoa maoni nchini umekosekana. Serikali inatumia fedha za kodi zetu na misaada kukandamiza demokrasia. Kwa hali hii tutaomba jumuiya za kimataifa ziinyime Tanzania misaada kwani inatumika vibaya kuminya demokrasia nchini.

Itikio la wasomi, wachumi, wananchi na wanasiasa: Huyu Lissu haitakii mema nchi. Hatuwezi kuendesha nchi na kuwahudumia watu wetu bila misaada toka nje. Mtu anayetaka kukwamisha misaada hatufai, apuuzwe kabisa. Msaada ndio nguzo ya maendeleo yetu. Hivi tukinyimwa misaada ataumia Lissu au Rais? Watakaoumia ni wananchi. Nchi haiwezi kwenda bila misaada.

Swali: Unapata picha gani ya wasomi, wananchi, wanasiasa na wachumi wa Tanzania?

My take: Kinachoungwa mkono Tanzania siyo nguvu ya hoja bali nani katoa hoja.

Section B (Sehemu ya pili)
Phase I (Awamu ya kwanza) (Julai 2015-Juni 2017)
Mkapa: Watanzania acheni kulialia. Watanzania ni wapumbavu na malofa.
Itikio la viongozi wa dini: Kimyaaaaaaaaa

Phase II (Awamu ya pili) (Julai 2017)
Lissu: Nchi inaongozwa kidikteta. Huyu kiongozi wetu ni udikteta. Udikteta uchwara umetamalaki nchini. Tuupinge kwa nguvu zote, viongozi wa dini wapinge na kila mtu kwa nafasi yake apinge maana hakuna aliye salama.

Itikio la viongozi wa dini (hasa kupitia msiba wa mke wa Mwakyembe): Hatutaki lugha za kuudhi na kuwakejeli viongozi wetu. Hatutamuunga mkono anayempinga Rais wetu na kumtolea lugha za kuudhi au matusi. Hiyo tabia ikome.

Swali: Unapata picha gani ya viongozi wa dini nchini?

My take: Tangu enzi na enzi viongozi wa dini (mafarisayo na masadukayo) wamekuwa upande wa tabaka tawala. hawajawahi kuwa upande wa wanyonge. Pia watu hawa hawakemei ubaya wa dhambi bali huangalia nani kafanya dhambi ndipo wakemee.
Dawa ya viongozi wa dini ni kuwanyima sadaka tu ili nao waonje ukali wa maisha.

Kama kutowa sadaka ni muhimu basi wape sadaka wenye uhitaji direct na siyo kuwapa sadaka hawa maporoko uchwara.
 
Mpendazoe UZALENDO NI NINI? LABDA UTUSAIDIE TAFSIRI NA CONTENTS ZA NENO UZALENDO! Swali jingine, nitajie Wazalendo wa nchi hii waliopo kwa Sasa na utuambie uzalendo wao, Je! Wewe ni mmoja wapo?

Back to your thread! Kikao gani kilimuidhinisha Dr. Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA 2015? MWAKA 2010 STYLE GANI ILITUMIKA KUMTEUA DR. SLAA KUWA MGOMBEA WA RAIS KUPITIA CHADEMA? JE! UTARATIBU HUO ULIKUWA tofauti na alivyopitishwa Lowassa kugombea kupitia Chadema mwaka 2015?

Umezungumza Lissu kutoa matamshi ya Matusi, naomba uniambie au unitajie Matusi yaliyopo kwenye maelezo yake! Ukishindwa basi inastahili kupuuzwa kama any other Stupid punk!
Niishie kwanza hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom