Mbona ndugu yangu bado unarudia swali hilo hilo la kumsema vibaya kiongozi kama ni kosa au si kosa la jinai. Nimekujibu kwamba jibu la swala lako hilo litatolewa na mahakama ambako Lissu atapelekwa hivi punde.
Halafu polisi hawawajibiki kukueleza wewe au mimi sababu za kumshikilia Lissu au mtu yo yote mwingine. Polisi wanawajibika kutoa sababu hizo kwa mahakama watakompeleka, na si kwako wala mwingine ye yote. Hivyo subiri utazisikia atakapofikishwa kwa Pilato. Haraka ya nini? Kwani Tundu ndiyo mtu wa kwanza kukamatwa na polisi?