Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,482
- 40,496
Bora wabaki na watoto wao, kwa usalama na afya ya mtotoHizi habari za single mothers Kuna watu watakuja na povu.
Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mkipata wa kuwaoa, pelekeni mtoto shule (boarding) na mwanaume uliyezaa naye atoe matumizi.Tukibaki nao tena tunakosa wakutuooa
Nadhani sisi wanaume, tusikimbie majukumuInaumiza sana kwa kweli,bora kummwagia hata usoni tu kuliko kumwagia ndani kisha mnapata mtoto anaanza kuteseka
Inasikitisha sanaTatizo wazazi wa sasa wanafanya watoto mitaji mfano sisi wakiume mtu anaona amlee tu kwake ili aje msaidia baadae akienda kwa mam ake anaweza kutusahau
Huu ni ujinga na umaskini mi nashuhudia mdogo wangu hajawai kuishi kwa raha mtoto wa baba mdogo yaani baba mdogo analazimisha akae nae yeye na anateswa na mkewe mpya mbele yake mara anyimwe chakula mtoto tangu darasa la nne mpaka form four hajapelekwa kwa mama ake anateswa sana kaisha mwili hatakiwi hata likizo kwenda huko huyu baba ake maisha hana yuko radhi alale njaa na mtoto wakati mother mzazi wa mtoto nguvu anazo analima anapata chakula we acha
Mungu si athumani yule father mdogo alifariki mwanae alikuwa kashamliza form four na ana miaka miwili nyumbani ndo akapata upenyo kwa kwenda kwa mama ake na kasholewa
Amini mkuu Bora alelewe na mama yake mzazi ,single mother ndo mpango mzimaKumekuwa na tabia ya wanandoa kuzaa nje, inawezekana kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.
Wakati nilipokuwa mdogo, kuna wakaka wawili walikuwa mapacha wanaishi na mama yao ambaye alikuwa jirani yetu. Wakati huo, hao wakaka walikuwa na miaka 25 hivi kwa kukadiria. Walikuwa warefu, wamejazia, na weusi kiasi; mnavyojua tena ulevi wa warembo wa mjini, wakashawishika, na dada mmoja akazaa na jamaa mmojawapo.
Yule dada alifikiri kuzaa na jamaa, angepata ndoa; Mambo yakawa tofauti. Basi yule dada akamtelekeza mtoto kwa mwanaume. Mwanaume naye akampa mama (bibi wa mtoto) yake amlelee mtoto.
Unavyojua tena, bibi wa mtoto alikuwa bado anapenda ujana. Akawa anamtesa sana yule mjukuu; yule mtoto akawa anakuja nyumbani kwetu, nampatia chakula, mpaka akawa rafiki yangu.
Baada ya mwaka mmoja, sisi tukawa tumeama ule mkoa, imepita kama miaka miwili hivi, tukapata habari yule mtoto alishafariki. Niliumia sana, nikajua chanzo ni wao kutokuwa karibu na mtoto.
Kwa sasa, yule bibi yake pia alishafariki.
Nilichojifunza; mtoto yeyote unayezaa nje ya ndoa alelewe na mama yake mzazi; we uliyemzalisha, jukumu lako ni kutuma hela ya matumizi tu, ili mtoto apate huduma bora.
πππAfterall kila mtu apambane na uterus!!! yake
Kinachotakiwa, aliyeweka mbegu ndio agharamie matunzo ya mtoto akiwa chini ya himaya ya mama yake; inapotokea mama anaolewa tena, mama anaweza akampeleka shule (boarding) kwa gharama ya baba wa mtotoJe mtoto wa mumeo aliyemzaa nje kabla ya kuoana akalelewe wapi..wanaume wao wanawaleta ndani akae na kulelewa na mke wa ndoa...km na wewe una wako asiletwe pale akae na bibi yake
Wapo ila wachache sanaWanaume mjue, hakuna atakayempenda mtoto kama mama yake!!!!!!!! (Unless wamama wachache wenye matatizo yao)
Acha mama alee mwanae.
Mambo ya kutia wake zenu dhambi acheni.
Mama yako au ndugu zako hatompenda mwanao kama ambavyo angependwa na mama yake
Afterall kila mtu apambane na uterus!!! yake