Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,174
- 39,936
Kumekuwa na tabia ya wanandoa kuzaa nje, inawezekana kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.
Wakati nilipokuwa mdogo, kuna wakaka wawili walikuwa mapacha wanaishi na mama yao ambaye alikuwa jirani yetu. Wakati huo, hao wakaka walikuwa na miaka 25 hivi kwa kukadiria. Walikuwa warefu, wamejazia, na weusi kiasi; mnavyojua tena ulevi wa warembo wa mjini, wakashawishika, na dada mmoja akazaa na jamaa mmojawapo.
Yule dada alifikiri kuzaa na jamaa, angepata ndoa; Mambo yakawa tofauti. Basi yule dada akamtelekeza mtoto kwa mwanaume. Mwanaume naye akampa mama (bibi wa mtoto) yake amlelee mtoto.
Unavyojua tena, bibi wa mtoto alikuwa bado anapenda ujana. Akawa anamtesa sana yule mjukuu; yule mtoto akawa anakuja nyumbani kwetu, nampatia chakula, mpaka akawa rafiki yangu.
Baada ya mwaka mmoja, sisi tukawa tumeama ule mkoa, imepita kama miaka miwili hivi, tukapata habari yule mtoto alishafariki. Niliumia sana, nikajua chanzo ni wao kutokuwa karibu na mtoto.
Kwa sasa, yule bibi yake pia alishafariki.
Nilichojifunza; mtoto yeyote unayezaa nje ya ndoa alelewe na mama yake mzazi; we uliyemzalisha, jukumu lako ni kutuma hela ya matumizi tu, ili mtoto apate huduma bora.