Penye wengi pana mengi, ndoa isiyo eleweka, anaweza kudai mgawanyo wa Mali huyu?

Thaconfession

JF-Expert Member
Jun 16, 2021
295
575
Nita-summarize mnooo, ili nisikuchoshe!
Iko hivi;

Walikutana chuoni (2008), first date ikapelekea mimba, mtoto alipozaliwa kutokana na mashaka mengi kwa jamaa akaamua kupima DNA, ikasoma POSITIVE! Jamaa akaamza kulea mtoto. Kila mmoja akiwa kwake lakini mawasiliano mazuri kati ya wazazi hawa.

Mwaka 2011 jamaa akaamua kwenda kujitambulisha ukweni, akitarajia kufuata taratibu za kuoa kabisa, (japo hakuwa akiishi na mama mtoto). Ile hali ya "sitaki mtoto wangu alelewe na baba mwingine" ilimmeza jamaa!

Baada ya kwenda ukweni, mwanamke akamtembelea jamaa mkoa anaoishi, akakaa wiki moja akaondoka na mimba, (mtoto wa pili) na baada ya hapo mwanamke akawa amejihakikishia kuwa huyu ni mumewe, japo hawajaishi pamoja wala kufunga ndoa, ila wana watoto 2!

Mwaka 2016, jamaa akaanza kuonja chungu ya mwanamke, KIBURI, JEURI, DHARAU ikawa sehemu ya maisha kila anapomtembelea mzazi mwenzake, jamaa akakata mguu kwenda kwa mzazi mwenzake! (na mwanamke akaacha kwenda kwa jamaa)-USHINDANI!

Baada ya kurudi, jamaa akaanzisha mahusiano mengine, akazaa naye! Huko mkoani mzazi mwenzake naye akazama penzini na mwanaume mwingine, jamaa akawa anapata hizo habari ila hakumfuatilia kwani alikuwa tayari na mahusiano mengine, na ana mtoto tayari!

Sasa miaka yote ya kila mmoja kuishi kivyake, (kati yake na mzazi mwenzake) jamaa alikuwa anakomaa kujijenga kiuchumi, huku mzazi mwenzake akiwa hana mchango wa hata shilingi 100!

Mwaka huu, inasadikika njemba ya yule mwanamke imeamua kuoa mwanamke mwingine (baada ya ku-date kwa zaidi ya 5 years). Hii ikamchanganya bidada...akaamua kurudi kwa baba watoto wake, anaomba radhi kwa KIBURI JEURI na DHARAU alizokuwa nazo, anaomba jamaa amdudie, jamaa amegoma!

Baada ya kukataa ameanza fujo, za chochote ulichonacho lazima tugawane! Jamaa amehamaki, how comes unadai mgawanyo wa mali ambaazo haujachuma kabisaaa !

Je, mwanamke huyu ana hiyo HAKI hata mbele ya sheria? Wajuzi wa mambo haya tafadhali,....uwanja ni wenu
 
Mambo mengine bhn hasa huyo mwanamke amepata wapi ujasil wa kudai mgao hajuwi hata cement ili shushaje kwenye gari.??
Amekomaa huyooo kwamba kwa kuwa wana watoto 2, basi ana assume ana haki ya kugawana mali, au lah jamaa amrudie!

Yaani mshkaji amekuwa "the only option" maana dada umri umesonga (anaitafuta 40) na jamaa aliyemtegemea na ame-date naye for years ame-opt kwenda kuoa mwanamke mwingine!
 
huyo jamaa ni wewe!!!

je, wametafuta au mna chet cha ndoa???

kam hana, then hana chake labda watoto watakuwa na chao
Hahahaaaa, naomba kukubaliana na hoja yako ili nipate shule zaidi...karibu sanaa

N.b hawana/(sina) cheti cha ndoa, hawajawahi (sijawahi) kuishi pamoja, japo wamezaa (tumezaa) watoto 2!
 
Amekomaa huyooo kwamba kwa kuwa wana watoto 2, basi ana assume ana haki ya kugawana mali, au lah jamaa amrudie!

Yaani mshkaji amekuwa "the only option" maana dada umri umesonga (anaitafuta 40) na jamaa aliyemtegemea na ame-date naye for years ame-opt kwenda kuoa mwanamke mwingine!
Ame fell watoto wala sio kigezo cha mgao.
 
Back
Top Bottom