Ukizaa nje ya ndoa; muache mtoto alelewe na mama yake mzazi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
28,808
39,011
Kumekuwa na tabia ya wanandoa kuzaa nje, inawezekana kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.

Wakati nilipokuwa mdogo, kuna wakaka wawili walikuwa mapacha wanaishi na mama yao ambaye alikuwa jirani yetu. Wakati huo, hao wakaka walikuwa na miaka 25 hivi kwa kukadiria. Walikuwa warefu, wamejazia, na weusi kiasi; mnavyojua tena ulevi wa warembo wa mjini, wakashawishika, na dada mmoja akazaa na jamaa mmojawapo.

Yule dada alifikiri kuzaa na jamaa, angepata ndoa; Mambo yakawa tofauti. Basi yule dada akamtelekeza mtoto kwa mwanaume. Mwanaume naye akampa mama (bibi wa mtoto) yake amlelee mtoto.

Unavyojua tena, bibi wa mtoto alikuwa bado anapenda ujana. Akawa anamtesa sana yule mjukuu; yule mtoto akawa anakuja nyumbani kwetu, nampatia chakula, mpaka akawa rafiki yangu.

Baada ya mwaka mmoja, sisi tukawa tumeama ule mkoa, imepita kama miaka miwili hivi, tukapata habari yule mtoto alishafariki. Niliumia sana, nikajua chanzo ni wao kutokuwa karibu na mtoto.

Kwa sasa, yule bibi yake pia alishafariki.

Nilichojifunza; mtoto yeyote unayezaa nje ya ndoa alelewe na mama yake mzazi; we uliyemzalisha, jukumu lako ni kutuma hela ya matumizi tu, ili mtoto apate huduma bora.
 
Tatizo wazazi wa sasa wanafanya watoto mitaji mfano sisi wakiume mtu anaona amlee tu kwake ili aje msaidia baadae akienda kwa mam ake anaweza kutusahau

Huu ni ujinga na umaskini mi nashuhudia mdogo wangu hajawai kuishi kwa raha mtoto wa baba mdogo yaani baba mdogo analazimisha akae nae yeye na anateswa na mkewe mpya mbele yake mara anyimwe chakula mtoto tangu darasa la nne mpaka form four hajapelekwa kwa mama ake anateswa sana kaisha mwili hatakiwi hata likizo kwenda huko huyu baba ake maisha hana yuko radhi alale njaa na mtoto wakati mother mzazi wa mtoto nguvu anazo analima anapata chakula we acha

Mungu si athumani yule father mdogo alifariki mwanae alikuwa kashamliza form four na ana miaka miwili nyumbani ndo akapata upenyo kwa kwenda kwa mama ake na kasholewa
 
Inasikitisha sana
 
Kumekuwa na tabia ya wanandoa kuzaa nje, inawezekana kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.

Wakati nilipokuwa mdogo, kuna wakaka wawili walikuwa mapacha wanaishi na mama yao ambaye alikuwa jirani yetu. Wakati huo, hao wakaka walikuwa na miaka 25 hivi kwa kukadiria. Walikuwa warefu, wamejazia, na weusi kiasi; mnavyojua tena ulevi wa warembo wa mjini, wakashawishika, na dada mmoja akazaa na jamaa mmojawapo.

Yule dada alifikiri kuzaa na jamaa, angepata ndoa; Mambo yakawa tofauti. Basi yule dada akamtelekeza mtoto kwa mwanaume. Mwanaume naye akampa mama (bibi wa mtoto) yake amlelee mtoto.

Unavyojua tena, bibi wa mtoto alikuwa bado anapenda ujana. Akawa anamtesa sana yule mjukuu; yule mtoto akawa anakuja nyumbani kwetu, nampatia chakula, mpaka akawa rafiki yangu.

Baada ya mwaka mmoja, sisi tukawa tumeama ule mkoa, imepita kama miaka miwili hivi, tukapata habari yule mtoto alishafariki. Niliumia sana, nikajua chanzo ni wao kutokuwa karibu na mtoto.

Kwa sasa, yule bibi yake pia alishafariki.

Nilichojifunza; mtoto yeyote unayezaa nje ya ndoa alelewe na mama yake mzazi; we uliyemzalisha, jukumu lako ni kutuma hela ya matumizi tu, ili mtoto apate huduma bora.
Amini mkuu Bora alelewe na mama yake mzazi ,single mother ndo mpango mzima
 
Je mtoto wa mumeo aliyemzaa nje kabla ya kuoana akalelewe wapi..wanaume wao wanawaleta ndani akae na kulelewa na mke wa ndoa...km na wewe una wako asiletwe pale akae na bibi yake
 
Kinachotakiwa, aliyeweka mbegu ndio agharamie matunzo ya mtoto akiwa chini ya himaya ya mama yake; inapotokea mama anaolewa tena, mama anaweza akampeleka shule (boarding) kwa gharama ya baba wa mtoto
 
Na wala si mwanaume kukimbia majukumu yake,ila ni mwanamke mpumbavu tu ndie anayeweza kumtelekeza mtoto wake kwa mme wake,ila kwa wanaojielewa hawezi acha mwanae iwe mvua ama jua
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom