Ukiwa Profesa, kuna elimu yoyote ya msingi ya ziada unayokuwa nayo tofauti na elimu nyingine za chini?

engijape

Senior Member
Nov 8, 2014
178
97
Jamani nauliza hivi kwa sababu nimeangalia kesi inayoendelea kati ya Winshear Gold Corp na Tanzania ARBN 20/25 kwa kweli inasikitisha. Profesa hana majibu yoyote yanayoweza kuishawishi Tribunal kuamua in favor of Tanzania. Kwa sababu hiyo, ninasikitika sana kuona wasomi na walimu wakongwe wa vyuo vikuu hawafanyi yanayostahili kufanywa na wao kwa maslahi mapana ya nchi.

Prof. Mbarawa, yeye amesaini mkataba bila kujua ni mkataba, bali akijua ni makubaliano. Prof. Sospeter Muhongo, naye kafanya yake wakati akiwa waziri wakati ule. sasa jamani Uprofesa usio argue kabla ya kutenda jambo ni uprofesa gani? hasa jambo lenye maslahi ya kitaifa.

Mikataba hii imeendelea kuiletea nchi madhila makubwa sana kimataifa na hata kitaifa. Tutaendelea kuwa na watu wa ajabu ambao kila kukicha wanaliingizia taifa hasara ya kukamatwa kwa rasilimali zetu ama kulazimika kulipa uzembe alioufanya mtu anayejiita Profesa na nguli wa mambo fulani. Jamani hili Taifa linamwitaji Mungu sana kuliko kawaida.
 
Inawezekana hata wewe kuna makosa mengi sana umefanya ila kwasababu hufahamiki unajiona upo vizuri kwa 100%
 
Nini kimezuia wewe kuwa msomi kama wao ili uwatendee haki watu wengine.
hajasema kuwa yeye yuko vizuri 100%. kuwa vzr kwa ASILIMIA hiyo ni sifa ya MUNGU.

ila kiukweli "wasomi" wetu hawajatutendea haki kwa kweli. kila siku ni uozo tu.
 
Back
Top Bottom