Ukiwa ni wewe utamfikiriaje mama mkwe wako

Ukiwa ni wewe utamfikiriaje mama mkwe wako

kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake hata kile kidogo Mungu anachotujaalia tunapaswa kushukuru na kuongeza bidii ya kufanya makubwa bila ya kusahau Riziki ni mafungu na kupata ni majaaliwa
 
Na mimi ntasubiria apite mwanamke wa uhakika then nasema daaah!! Cheki mzigo huo.. Hapo nahonga hata nyumba... Na nione sasa watasemaje vichaa hao
 
mumewe mama mkwe yupo bush analima mahindi hata baiskeli hana... nitamuuliza vp baba mkwe yeye analo??
 
Kupiga kimya ni jibu la mjinga! Kwa heshima ya mke just keep quite sio kila kitu ujibu ...... Respect her kama unavyompa heshima mama yako mzaz na tukumbuke mzaz habadilishwi...for the sake of your wife's love nyamaza
 
''Kweli mama, gari zuri sana hilo, jamaa amejitahidi kwa kweli.'' Mungu akitusaidia baadae tutapenda na sisi tumiliki kama hilo, kwa sasa hiki kivitzi kinatusaidia sana mama yangu''



Jibu zuri sana tena lenye busara na maadili ndan Yake. Asante
 
''Kweli mama, gari zuri sana hilo, jamaa amejitahidi kwa kweli.'' Mungu akitusaidia baadae tutapenda na sisi tumiliki kama hilo, kwa sasa hiki kivitzi kinatusaidia sana mama yangu''



Jibu zuri sana mkuu...ataomba msamaha mwenyeweee
 
nani kakwambia udume unapimwa kwa umilikaji wa magari?
 
Nampotezea maana me sio mme wake kusema amenidharau labda maana kama mme wake hana hata baiskeli anaona "range" lazma atahamaki
 
Kabisa Mkuu. Kuna watu wengine huwa wanajisahau kwenye kuongea, Inatakiwa tu kutumia hekima kidogo kumfanya afikiri, au unakaa tu kimya unajidai hujasikia.
Jibu zuri sana mkuu...ataomba msamaha mwenyeweee
 
Kabisa Mkuu. Kuna watu wengine huwa wanajisahau kwenye kuongea, Inatakiwa tu kutumia hekima kidogo kumfanya afikiri, au unakaa tu kimya unajidai hujasikia.
MM ningemjibu vibaya ila kwa jibu hili nimejifunza kitu kikubwa sana
 
Nimefurahi sana kusikia umejifunza kitu kaka, Karibu sana Engineer2014.

Kumjibu mtu vibaya unakuwa unajikosea adabu wewe mwenyewe. Majibu ya upole na hekima kusaidia kumfanya aliekosa afikiri mara ya pili. Ila ukimjibu vibaya unampa relief. Fikiria mtu akutukane akitegemea utamrudishia matusi au umpige, Then ukanyamaza au ukasmile tu wala usijibu chochote au ukamwambia tu Asante nashukuru sana; ukaenda zako au ukaendelea na mambo yako.. unafikiri unamuacha na hali gani moyoni/kwenye akili yake?.. ila ukimjibu au kumtukana unakuwa umempa unafuu maana ndiko alichotegemea kwako.

Ni hatar kumpa mtu mwingine uwezo wa kuamua reactions/feelings zako (No one can make you inferior without your own consent - Elenor). Huwa najiuliza tu kirahisi, hivi ukinitukana matusi (yatajiandika usoni kwangu?kwamba kila mtu atajua umenitukana? Huwa najiuliza ni kitu gani nifanye ili unayetukana udhalilike zaidi? (either ntacheka, ntakaa kimya au ntakushukuru au ntakupongeza kuwa unajua kutukana vizuuri sana) baasi. Mtu akimtukana mwenzie anayeonekana na kuonesha ujinga na upumbavu wake ni yule anayetukana na sio anayetukanwa. Maneno maneno yapo, ni kutafuta tu njia ya kukabiliana nayo kirahisi bila kukuathiri wewe.


MM ningemjibu vibaya ila kwa jibu hili nimejifunza kitu kikubwa sana
 
Back
Top Bottom