Ukiwa kama abiria unasafiri safari ya mbali ni vizuri ule nini njiani na uepuke kula nini

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,181
11,601
Safari ni hatua, Safiri salama.

Mpendwa,

Mthalani abiria anasafiri kwa basi kutoka mkoa moja kuelekea mkoa mwingine.

Ni aina gani nzuri ya vyakula avitumie njiani na aina gani ya vyakula abiria huyu msafiri aviepuke kula njiani, ili hatimae safari yake iwe tulivu, huru, nzuri na salama kiafya?
 
Kuna vile Viepe hua unakuta wameweka kwenye kimfuko tayari, chukua hiyo na zile Juisi za Avocado (Wanatengenezeaga nyumbani) hua kwenye chupa za soda za take away, kula kabisa

Ukiwa ndani ya gari, utanishukuru baadae.
Hivyo kila stendi lazima upate mkuu.
 
Tafuta Biscuits mfano; Digestive kabox kakubwa, juice, maji, peremende mchanganyiko, hivi ni vya kuanzia safari hadi unafika, maana safarini siyo sehemu ya kushindilia tumbo.

Njiani sasa mle mnaambiwa 'kuchimba dawa dakika 10, shuka kanywe chai moto ya rangi na bites kidogo, achana na kubeba machips au maubwabwa.

Binafsi safarini huwa nanunua mapema Brown bread, mix jam juice na maji hadi nafika, bila kusahau peremende.
 
hii muzuri zaidi 👌💪
 
Safari ni hatua, Safiri salama.

Mpendwa,
Mthalani abiria anasafiri kwa basi kutoka mkoa moja kuelekea mkoa mwingine.
Ni aina gani nzuri ya vyakula avitumie njiani na aina gani ya vyakula abiria huyu msafiri aviepuke kula njiani, ili hatimae safari yake iwe tulivu, huru, nzuri na salama kiafya?
karanga za kukaanga ama korosho na kama ni nyama iwe ya kukaanga
 
Ni vizuri usile.

Aibu ya kusumbuliwa tumbo njiani ni mbaya sana....

Usile kabisa, au kunywa chai asubuhi tu...
actually ndio chimbuko la bandiko langu, nimesafiri hivi leo akatokea abiria moja kwa utambulisho wa mavazi na lafudhi alikua mmasai,
Na alipandia basi letu njian na basi halikua na choo cha ndani na abiria huyo hakua amepata siti alisimama...

Ndugu yangu ,
kwa bahati nadhani tumbo likamvuruga na kufurukuta, akatoa sauti kubwa simamisha gariiiiiii, abiria wakawa wanamshangaa......

Akashauti tena mara ya pili simamisha gariiiiiii nichimbe dawa tumbo imefurugaaaaa tumbo yangu maskini abiria yule mpaka akakaa chini.......

Abiria wakashtuka na kuona kwamba sasa huyu anaporomosha muharo sasaivi...

Ndipo kelele za abiria zikasaidia dereva wa basi akasimamisha, abiria yule hakua amevaa chochotete ndani zaidi ya shuka alizokua amejifnga, na aliposhusha mguu njee ya mlango wa basi tu, palepale akafanye yake pwraaaaaaaaaaa akashusha muharo wa nguvu sana....

alipomaliza akakusanya kitita cha majani makavu akajichamba nayo mara mbili akawa anaingia kwenye basi, abiria wakashauti wakagoma hadi ajichambe na maji....

wakamrushia chupa za maji akajichamba vizur ndipo akaingia kwenye basi tukaendelea na safari....

So,
milo ni muhimu izingatiwe kabla, wakati na baada ya safari...
 
Back
Top Bottom