Ndugu wanajamii naungana na Paul Mayalla ktk makala zake za Kwa Maslahi ya taifa.
Tukiwa ktk wikendi hii ni vema tukatafakari jambo hili. Kumbe cheo ni dhamana. Siasa ni swala la kitaifa sio la mtu binafsi na kwamba usijimilikishe michakato ya kitaifa kufika hatua ya kuumiza watu wengine ili kujionesha wewe ndio mzalendo sana.
Kumbuka ukifanya hivyo sana sana unafurashisha na kunufaisha wapambe wako lakini ukiondoka nafasi hiyo hiyo atachukua mwingine na nchi itasonga mbele. So kama ulikuwa unadhani bila wewe nchi haisongi mbele unajidanganya.
Mfano tunao sasa, Mh Rais Samia Nchi inasonga vizuri tu. waliodhani bila wao hatuwezi kusonga mbele wajiulize tena na tena. Kukuru kakara zote pengine hazikuwa maana sana kwao bali kwa wapambe wao.
Tujiulize tena je Jiji la Dar es salaam limesinama? Si linasonga mbele bila Paul Makonda? Sasa yale maugomvi yalikuwa ya nini?
Leo nani angeamini kuwa Uhuru Kenyata iko siku ataungana na Raila Odinga wawe na wazo moja na maono mamoja?
Kama wewe unaweka swala la siasa kama jambo binafsi kiasi cha kuanza kuwinda na kutesa watu sababu ya siasa, kutukana na kukera watu sababu ya siasa now you must have learned.
Ipo siku Kiongozi mkubwa wa CCM tena yamkini Mwenyekiti ataungana na Mpinzani; sijui utakuwa upande gani ndugu yangu . Linapokuja swala la Maslahi ya Taifa watu makini huwa wanakuwa kitu kimoja kama Uhuru Kenyata na Raila Odinga.
Je Kwa sababu IGP ni mwingine ndio kusema polisi yetu haitafanya kazi? La hasha itasonga ktk majukumu yake pengine kwa ubora zaidi. Sasa kubambikia kesi watu kwa nini?
Wilaya ya Hai hawana Maji kwa sababu Sabaya hayupo? Au kuna hospitali imefungwa kwa sababu hayupo Mzalendo General Sabaya?
Vipi Chama tawala ccm hakisongi mbele sababu Mangula hayupo? Sasa walishindwa nini kushauri mambo mema yakupendeza Mungu na wanadamu?
Vipi Bunge nalo limefungwa kwa sababu Ndugai hayupo? Linasonga mbele tena likiwa Live. Sasa majivuno na makasiriko yalikuwa ya nini kwa Mr Job?
Mwisho: Huu ndio muda mwafaka pekee kwa Rais Samia kuhakikisha Nchi inatawalika kwa misingi ya sheria bora na Katiba bora.
Ipo siku ataihitaji na kama atafata huu ushauri huko mbeleni atanishukuru.
Nakutakia Kazi njema Mh Rais Samia Suluhu ktk ujenzi wa Taifa.