ukitegemea mwanaume wa miaka hii kumbe unalala njaa eeeh!

ukitegemea mwanaume wa miaka hii kumbe unalala njaa eeeh!

ahahaaa ujue raha ya chakula kitamu tumbo liwe empty bwana!ila imekula kwangu aisee nimepigwa njaa usiku sikujua kama nitafika asubuhi aisee kidogo nile vipodozi
Nimecheka kwa sauti mpaka nimejishtua mwenyewe! Saa 3 usiku mbona sio usiku sana? Si ungenunua chips vumbi njiani?Lol!
 
^^
Si rahisi mtu kukosa vyote..anyway umenishangaza sana kwani wanaume masikini tunapashwa humu mpaka tunajuta kuijua jf
^^

hahahaaa....... Best umenichekeshajeeee!!!!!!
Hampashwi banaa, hizo ni changamoto tu, ili nanyi muongeze bidii kwenye utafutaji.
 
Polee sana Smile kulala na njaa, pamoja na kuwa ulilala na njaa kwa kweli nimecheka… Story imenifurahisha mno. Hata hivyo naomba niweke sawa yafuatayo (tokana na vile nijuavyo mimi).

Usione mwanaume sababu tu ana uwezo wa Pesa , gari nzuri ama vitu vizuri na vya gharama ukatumia kigezo hicho kufikiria kuwa akiwa ni mpenzi wako basi maisha yako yatakuwa mepesi. Wakaka/baba hasa wa mijini wengi wenye pesa ama wasio na pesa the way huwa treat wanawake wao ni tokana na tabia zao za ndani.


Imani kuwa ukiwa na mwanaume mwenye pesa basi ushakuwa settled huwa ni kwa wachache na si wanawake wote hubahatika hivyo. Tena wanaume wengi wenye pesa wana tabia fulani ya kuhakikisha anampata mwanamke (walau kwa siku moja/ama kadhaa) - Wanapishana level za kuhonga tu, kuna wale wachache atakupa gari, kuna wale watakao kupeleka nje for shopping, kuna wale ambao atakununulia simu ya gharama ila mwisho wa siku akishapata kile alichotaka kwako ;


  1. Anakuacha mara moja na hataki tena umtafute.
  2. Anajenga misingi ya wewe kuwa kipozeo chake, siku akitaka mwanamke akakosa ndipo hapo tu atakapo kutafuta.

*Else labda kweli mpo katika mahusiano na imetokea kuwa mmependana.

Suala la mwanaume simple… Kama unamaanisha asiye na pesa then labda kama hutaki huyo mwanaume kamwe asije kufanikiwa kipesa. Mwanaume wako (kama ilivyo Mwanamke) utamjua tabia yake hasa na jinsi anavyokuthamini akiwa na pesa… Mara nyingi mtu ambae hana pesa huwa mara nyingi na tabia Fulani za umakini hali akiwa na pesa anafanya vile ambavyo anataka na kuona yeye ni sahihi. Ni rahisi kumjua mpenzi wako kama ana pesa kuliko asipokuwa na pesa... Ndio maana unakuta wengi wakilalamika pale tu Mwenza/Partner wake alivyofanikiwa na kuwa na pesa kubadilika kwa tabia.

Mwisho wa siku ni mle mle tu.
kwanza asante kwa kunipa pole ingawaje umenicheka my dear! kiukweli usiku nimeuonaje mchungu?
back to topic love!
mimi sio kwamba sitaki au sipendi mwanaume aliefanikiwa ! ni ndoto ya kila mwanamke kuwa na mwanamme alie kistable kimaisha kila mtu anataka furaha duniani huku!ila maisha nayo hayapo rahisi kiivo kama ulivoonyesha hapo juu...dunia nayo ina watu wa aina nyingi..ni kweli ukitaka kujua tabia ya mwanaume apate pesa na ukitaka kujua tabia ya mwanamke ukose pesa!pesa ndo inaonekana kurun haya mahusiano ya siku hizi...tabia za watu zinajificha kwenye hizi not!
kwa upande wangu mimi naposema napenda mtu simple namaanisha napenda mwanaume cool sipendi mtu high yaani yule ambae kila mdada jicho lipo kwake hope unanielewa mamii! this guy kiukweli yupo vizuri anaweza kuwa na mwanamke yoyote si unajua mjini hapa watu wengine miili yao ndo atm zao?...yaani ni yule mwanaume ambae ukiingia nae mahali macho yote kwenu...mi siwezi napenda maisha yangu simple ...napenda mtu ambae naweza kumuhandle sio kwamba napenda kucontrol mtu ila sipendi mtu wa kunipa maswali kichwani kwangu!
by the way unapotea sana bwana ...ile blog yako nimeisahau nimeitafuta kweli hebu nikumbushe dear!
 
^^
Si rahisi mtu kukosa vyote..anyway umenishangaza sana kwani wanaume masikini tunapashwa humu mpaka tunajuta kuijua jf
^^
unakuwa hadi maskini wa moyo!usaidiweje sasa?
maskini hata wa tabia nzuri!? mwanaume sio pesa tu my dear kuna utajiri zaidi ya pesa ! pesa zipo tu na zinatafutwa kuna watu wana pesa lakini hawapendwi vile vile! nikuulize kwanza wewe ni maskini?
 
Nimecheka kwa sauti mpaka nimejishtua mwenyewe! Saa 3 usiku mbona sio usiku sana? Si ungenunua chips vumbi njiani?Lol!
ahaaaa sili chips dear si unajua nataka mwakani nigombee u miss bongo?
 
Ahahahaah Smile, nenda kapate supu BREAK POINT aisee nitalipa!!!!

Siku nyingine Mentor nikikuomba mtoko ukubali...tunapanda daladala na dinner ni kwangu...mengine pigia mstari!!!!!!:tape:
ahahaaaaaa .....nitakutafuta jioni bwana...bora hata nyumbani
 
wapo wanaolilia wanaume wenye pesa! ila sio mimi..pesa sio kila kitu ..na kukosa pesa pia sio kuwa na mapenzi..kuna mtu ni maskini wa vyote huyo asaidiweje?

Promo Only.
=====================
Ukipata Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa
=====================
 
umenkumbusha one day nliitwa na njemba mida ya jion nkamualika na sista angu tukanywe na kula nyama choma tuenjoy,tukajitoa ufahamu hata mia mifukoni hatuna kilichotokea najuuta hata spaleta hatukunywa na tukaishia kutembea kwa mguu frm kona ya bwiru hadi karibu na nela tupo hoi tumechoka njaa inauma ndo kupata lift ya kuturudisha uswazi.
ahahaaaaa pole
 
hahahahahahahaaaaaaaaaa
hii stori imenichekeshaje best? pole sana

ila hapa ndo pameniacha hoi zaidi: "mimi sitaki kuingia majaribuni si mnajua tena roho i radhi ila mwili ni dhaifu!"
 
^^
Umeniacha kidogo AshaDii from your intelligence and experience,ili ku maintain upendo mwanaume abaki katika pato la hali tu? Yaan asiwe tajiri wala masikini ili mwanamke awe secure?
^^

Himidini... Post yangu imelenga kwa wanaume watongozaji kwa lengo la kulala na wewe na si kuwa katika mahusiano. Hili ndilo lililomtokea Smile, huyo kaka siku ya kwanza tu kufanikiwa kutoka nae anatoa taarifa za ku book chumba; ni wazi shida yake ilikuwa kulala nae then asepe.

Kungekuwa na upendo wala hata kidogo uwasilishi wake ungekua tofauti na alivyofanya siku hiyo.

Nikija suala la pesa katika mahusiano; Pesa ni muhimu sana tu lakini siyo ambayo inajenga mahusiano (Ingawa inasaidia kujenga mahusiano); kuna wasio na pesa na wanaishi kwa amani kuliko walizo nazo. Hivyo iwe mwanaume aliye na uwezo ama asiye na uwezo kuimarika na kuwa katika mahusiano ni matokeo ya matendo na jitihada za wahusika katika mahusiano hayo.
 
U miss bongo wa nini kama ulishapitishwa na Lemutuz kuwa ni mbabes kwa kweli?
ahaaaa raisi wetu wa mabebs hajanipitisha bado kaniambia nitoe kwanza hiki kitambi loh!
 
hahahahahahahaaaaaaaaaa
hii stori imenichekeshaje best? pole sana

ila hapa ndo pameniacha hoi zaidi: "mimi sitaki kuingia majaribuni si mnajua tena roho i radhi ila mwili ni dhaifu!"
unajua sisi ni binadamu dear ..huwezi kusema hutaki kulowana wakati unachenza kwenye mvua!
 
Nimefurahi sana ulivyomfanyia huyu mwanaume, kwanini watu wanafanyia watu wengine hesabu hivyo?? Ila dada usitembee bila pesa yako mfukoni, vijana wengine matapeli tuu....Pole sana na hongera kwa msimamo ulionesha!!!
ahahaaa ujue raha ya chakula kitamu tumbo liwe empty bwana!ila imekula kwangu aisee nimepigwa njaa usiku sikujua kama nitafika asubuhi aisee kidogo nile vipodozi
 
ahaaaa raisi wetu wa mabebs hajanipitisha bado kaniambia nitoe kwanza hiki kitambi loh!
Kwani bado haujafuatilia DVD yenye maelekezo ya kutoa kitambi? Muuze Superman anajua zinapatikana wapi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom