Mkuu Juvenile kabila haliolewi anaolewa mtu. Sidhani kama kabila ni sifa kubwa katika kupata mke ama mume. labda kama unawapigia debe wasafwa. Binafsi ninawafahamu sana wasafa na nimeishi nao kwa muda mrefu sana, sifa ulizowapa hazi-apply kwa wote automatically. NO. hizo hutokea on indiviual basis.
Na ili uone kuwa nawafahamu vizuri naongezea hayo yalielezwa na mkuu Shemtibuko hapo juu. sehemu nyingine walipo wasafwa ni Uyole, Mbalizi, Igoma, Ilungu, Ilomba, Ntangano, Nsongwi, Mantanji, Inyala, Kawetele, Iduda n.k. na majina yao ya asili ni kama (kwa wanaume)Shungu, Mbwiga, Ndele, Nzunye, Mwava(kwa wanawake) Tabu, shimba, Nzoho, Ilongo ama Yilongo, Shaali, Mbozyo, Mwisyo, Shoogoo.