Ukitaka kutokufa mapema ishi taratibu Kama kobe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
20,128
46,470
Wakuu nimemchunguza Kobe kwa muda mrefu nikaja na hitimisho kuwa viumbe vyote ambavyo vinafanya mambo yake taratibu/polepole Basi vina uwezekano mkubwa wa kuishi maisha marefu tofauti na viumbe ambavyo viko speed speed katika Mambo yake.kwa mfano kuku,nzi,mbu na mijusi wako fasta fasta ndo maana wanakufa mapema.kobe yeye anajivuta vuta Sana na wanyama wengine ambao wanajivuta vuta wakitembea, wanakula taratibu, Wana sex taratibu nimegundua life span yao Ni kubwa
Kwa hiyo hata kwa sisi binadamu ukitaka kuishi maisha marefu basi kuwa mpole.usiwe rough rough ukataka kutumia kila kitu vingine ambavyo sio vya lazima viache,safari ambazo sio za lazima achana nazo,starehe ambazo Ni za kipumbavu zikatae achana nazo,sehemu zisizo na ulazima usikae.maana jinsi unavyojitumia wewe ndivyo unavyojila mwenyewe.Kumbuka E=MC SQUARE manaake speed ya Mambo yako ikiwa kubwa na jinsi mda unavyoenda binadamu unaji destruct mwenyewe.usiwe mtu wa kula kula ovyo kila kitu.fanya mambo taratibu concentrate kila Jambo vuta pumzi vizuri na uisikilizie.jiepushe na karama au sherehe zenye shangwe kupitiliza
Lakini kumbuka usiwe polepole siku nzima lazima upate muda pia wa kufanya mazoezi angalau dakika 45 kwa siku inatosha.masaa mengine yanayobaki ishi Kama Kobe yaani ikibidi hata ukiwa unatembea tembea na fimbo Kama mzee wa miaka tisini jivute vute ukifanya hivyo nakuhakikishia utaishi miaka mingi na utaona mengi.hiyo Ni Imani yangu wakuu
IMG_20190305_182709.jpeg
 
Wanyama wengine ambao wanaishi miaka mingi kutokana na tabia yao ya uslow ni tembo na nyangumi
 
Uko sahihi yaan nchi yetu wazee sana ni wachache lakini nchi za kiarab wazee sana ni wengi kusikia msiba ni nadra sana na ukisia mtu kafaa lazma huyo ni mzee sana, kama kijana labda ajali au kwa maradhi ya kurithi, nikagundua sio kila kifo ni mipango ya mungu(ni kujipa moyo)vingne tunajitakia kufanya jambo/mambo kupita kiasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli basi Leyland Albion miaka ya sabini, kupata ajali ilikua nadra sana , na gari ndogo speed mwisho sitini hamna ajali. Tatizo sasa hivi dunia imebadilika ukienda mwendo wa Kobe hata smartphone utaziona kwa wenzio bro... , Ila nimekuelewa kwenda pole pole ni kukwepa vizingiti....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom