Ukitaka kujua Ufanisi wa Rais Magufuli, ruhusu mikutano ya Siasa.

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
3,851
Wanabodi,
Kama kweli Rais Magufuli anataka kujipima ufanisi wake, basi aruhusu, mikutano ya Siasa kwa vyama vyote, kwa Mujibu wa Ibara ya 3 ya Katiba ya Tanzania.

Hii itasaidia kukosorewa na kujirekebisha.

Kuzuia vyama vingine vya siasa kufanya Mikutano, ili hali Rais na Waziri Mkuu, wanafanya siasa, kwa resources za Serikali, ni sawa na kuingiza Timu fainali bila timu pinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule mseminari Hana kifua cha kukubali ukosoaji

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Thubutu! Mioyoni mwao wanajua kuwa hawaungwi mkono na watanganyika wengi ndiyo maana kila siku ni vitisho kwa kwenda mbele.
 
Hataki kufa na pressure mapema baba wa watu . Anaujua mziki wa wapinzani mpaka kupiga pushap hadharani mlidhani alipenda. Muachenii jamani
 
Hilo jambo Mkulu hawezi kulikubali, kwa kuwa Mkulu hana uwezo wa kujibu hoja za upinzani.

Anachotaka yeye ni sawasawa unawapandisha mabondia 2 ulingoni, halafu bondia mmoja unamfunga kamba mikono yake yote na yule bondia mwingine humfungi kamba, halafu unawaambia wale mabondia wapigane.

Hivi katika mazingira hayo unapomshangilia yule bondia ambaye hakufungwa mikono yake kwa kumpiga yule bondia ambaye kafungwa mkono yote......

Hivi wewe utakayekuwa umamshangilia yule bondia ambaye hajafungwa mikono kwa kumpiga yule bondia ambaye amefungwa mikono, hivi tukikkuita wewe kuwa mpumbavu na lofa utalalamika?
 
  • Thanks
Reactions: bne
Mikutano ya siasa nadhani ni ruksa kwa mbunge/diwani wa eneo husika sema tu mara nyingi intelijensia inafanya forecast na kutabiri uvunjivu wa amani, hivyo vibali kuminywa. Kilichokatazwa ni kualika "mamluki"ili kujiongezea nguvu na kuvutia nyomi la watu (say Bulaya kumualika Lissu kwenye mkutano wake huko Bunda). Hapa ndo kwenye utata. Kwanini uzuie movement ya watu na uhuru wao wa kusema chochote popote ilhali hawavunji sheria za JMT?
 
Kwenye majimbo yao

Mwenyekiti wa chama cha siasa ngazi ya taifa anaongea vipi na watanzania na kuhamasisha kupata wanachama wapya wakati sio mbunge? Au hata kama ni mbunge, hicho chama ni cha jimbo lake tu kwa mujibu wa sheria za nchi, na watanzania wasafiri kwenda kwenye jimbo lake?
 
Mikutano ya siasa nadhani ni ruksa kwa mbunge/diwani wa eneo husika sema tu mara nyingi intelijensia inafanya forecast na kutabiri uvunjivu wa amani, hivyo vibali kuminywa. Kilichokatazwa ni kualika "mamluki"ili kujiongezea nguvu na kuvutia nyomi la watu (say Bulaya kumualika Lissu kwenye mkutano wake huko Bunda). Hapa ndo kwenye utata. Kwanini uzuie movement ya watu na uhuru wao wa kusema chochote popote ilhali hawavunji sheria za JMT?
Bulaya kumualika lissu ni uwamuluki lkn polepole na shaka kwenda kwenye mikutano ya wabunge wa ccm sio uwamaluki.
Aibu kubwa hii kwa ccm haitawacha salama
 
Usijekutuletea Machafuko Nchini Tanzania
Hadi Sasa Hujaona Yule Mmoja Kakunja Ngumi Tayari Ikiruhusiwa Haa Itakuwa Ugomvi
 
Bulaya kumualika lissu ni uwamuluki lkn polepole na shaka kwenda kwenye mikutano ya wabunge wa ccm sio umamluki.

Ndo hapo sasa. Mkuu anapiga kampeni na kuwapandisha jukwaani "mamluki" waendelee kumshambulia adui aliyefungwa kamba miguu na mikono yote. Mkijaribu nyie, huo ni uchochezi na mtapewa kesi ya kufanya "kusanyiko lisilo halali"
 
  • Thanks
Reactions: bne
Nimesoma hoja zote hapo juu, nimeona kuja Inzi wa Kijana wanaropoka tu, hoja zao dhaifu sana

Hivi Kama TWAWEZA walisema hicho chama kinapendwa na Watu wa vijijini/wazee na wajinga

Hao wajinga ndio wanaandika utumbo huku
 
Back
Top Bottom