Hayati Magufuli alijua Vyama Vya Siasa havina uwezo wa Kufanya mikutano akaifutilia mbali. Mwenye macho haambiwi tazama!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,005
142,040
Ni zaidi ya Mwaka tangu Mikutano ya Siasa iruhusiwe lakini imefanyika Mikutano kiduchu.

Hata CCM Mikutano yao inabebwa na Watu wa serikali Ndio Unasikia kule Chato Bavicha wakalalamika msafara wa Komredi Makonda umesheheni magari ya serikali.

Ukiona Chama cha Upinzani kinamudu Mikutano ujue kimelipwa na Wahuni fulani ili kuleta chokochoko mfano Operesheni naniliu.

Magufuli Alikuwa sahihi kuzuia Mikutano ili Watu wafanye Kazi badala ya kuendesha Majungu.

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Usituletee habari za mtu ambaye hakuwa na akili. Jifunze kwa mwenye akili rais wetu wa sasa amewaruhusu km wameshindwa ni wenyewe je unajisikia kelele? Huyu ndiye rais mwenye akili siyo minguvu ili wapate sababu.
 
Sasa hiyo operesheni ni utapeli tu, Dp world kapata tender. Wanaona aibu hata kujitokeza hadharani, walikuwa wanahubiri uzushi.
 
Ni zaidi ya Mwaka tangu Mikutano ya Siasa iruhusiwe lakini imefanyika Mikutano kiduchu

Hata CCM Mikutano yao inabebwa na Watu wa serikali Ndio Unasikia kule Chato Bavicha wakalalamika msafara wa Komredi Makonda umesheheni magari ya serikali

Ukiona Chama cha Upinzani kinamudu Mikutano ujue kimelipwa na Wahuni fulani ili kuleta chokochoko mfano Operesheni naniliu

Magufuli Alikuwa sahihi kuzuia Mikutano ili Watu wafanye Kazi badala ya kuendesha Majungu

Mungu wa mbinguni awabariki!
Mawazo ya wana ccm bwana.
Vyama vya siasa kufanya mikutano sio huruma na hisani ya raisi bali ni haki ya kikatiba. Lakini kwakuwa hata raisi mwenyewe ambaye amepatikana kwa watu kuheshimu katiba naye alisema si lazima mtu kuifuata unaweza kuelewa tatizo kubwa lililopo nchi hii.
Japo namkubali jpm kwa mengi, ila kuizuia alikosea na alivunja katiba.
Iwe uwezo wanao au hawana waache wafanye wakiweza maana ni haki yao kikatiba.
Ccm yenyewe inafanya mikutano ya siasa mwaka mzima tena makatibi wake wakisindikizwa na polisi ikiambatana na watendaji wa serikali. Kama mmekubali demokrasia weka fair grounds. Mna resources, vyombo vya dola bado, upendeleo wa kufanya siasa kwa kutumia.mgongo wa chama tawala, bado hata kile kidogo mnakiogopa?
Nashangaa ccm inaogopa nini maana hata kwa tume huru bado itashinda tu maana watanzania walio wengi hawana habari na kile kinachoendelea wao kinachowafurahisha ni kiongozi kupiga simu akiwa jukwaani akaganya maigizo.
 
usituletee habari za mtu ambaye hakuwa na akili. Jifunze kwa mwenye akili rais wetu wa sasa amewaruhusu km wameshindwa ni wenyewe je unajisikia kelele? Huyu ndiye rais mwenye akili siyo minguvu ili wapate sababu

Unakatwa na abdul
 
Back
Top Bottom