Ukitaka kujua thamani ya muda, safiri Km 40 ndani ya lisaa limoja, halafu jaribu kusafiri Km 40 ndani ya 1/3 ya lisaa

Hakuna Muda unaopimwa hivyo, muda unapimwa kwa Sekunde sio Sh/dakika ( Time is measured in Second not Sh/Minute.)
Hakuna muda tutakao okoa kwa Sh per Minute!
 
Kama wewe ni dereva, siku jaribu kuendesha kwa speed ya 40km/hr kwa muda wa lisaa limoja , hapa utakuwa umesafiri km 40; halafu jaribu kusafiri umbali huo huo wa km 40 kwa theluthi (1/3) ya lisaa, yaani tumia dakika 20 (endesha 120km/hr kwa muda wa dakika 20), hapa utakuwa umesafiri umbali ule ule wa Km 40 ila tu utakuwa umetumia muda mfupi mara tatu zaidi. Sasa kokotoa mafuta uliyotumia mara ya kwanza na yale uliyotumia mara ya pili. Utakuta kiwango cha mafuta uliyotumia mara ya pili ni kikubwa zaidi ya kiwango ulichotumia mara ya kwanza kwa mwendo wa taratibu, hivyo ili kuokoa muda kwa kuendesha haraka imetugharimu mafuta (pesa zaidi). Kama tofauti ya mafuta ni lita 10, je thamani ya muda uliookolewa katika case yetu hii ni shs.ngapi per minute?
Rejea elimu yako ya fizikia. Kuna kiwango cha mwendokasi (speed) ambacho ni mafuta hutumika vizuri (optimal fuel consumption). Hii ina maana katika mwendokasi wa chini au wa juu sana mafuta hutumika sana. Isitoshe hujazungumzia kasi ya kufikia mwendokasi wowote (acceleration) ambayo pia huchangia matumizi ya mafuta.
 
Back
Top Bottom