Ukitaka kujua thamani ya muda, safiri Km 40 ndani ya lisaa limoja, halafu jaribu kusafiri Km 40 ndani ya 1/3 ya lisaa

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Kama wewe ni dereva, siku jaribu kuendesha kwa speed ya 40km/hr kwa muda wa lisaa limoja , hapa utakuwa umesafiri km 40; halafu jaribu kusafiri umbali huo huo wa km 40 kwa theluthi (1/3) ya lisaa, yaani tumia dakika 20 (endesha 120km/hr kwa muda wa dakika 20), hapa utakuwa umesafiri umbali ule ule wa Km 40 ila tu utakuwa umetumia muda mfupi mara tatu zaidi. Sasa kokotoa mafuta uliyotumia mara ya kwanza na yale uliyotumia mara ya pili. Utakuta kiwango cha mafuta uliyotumia mara ya pili ni kikubwa zaidi ya kiwango ulichotumia mara ya kwanza kwa mwendo wa taratibu, hivyo ili kuokoa muda kwa kuendesha haraka imetugharimu mafuta (pesa zaidi). Kama tofauti ya mafuta ni lita 10, je thamani ya muda uliookolewa katika case yetu hii ni shs.ngapi per minute?
 
Mkuu kundesha gari ikiwa 120km/h huku Rev ipo 3000 au 3500 na kuendesha 40km/h huku Rev ipo 2000 au 2500 itategemea gari inateknolojia gani VVTi au
 
Mkuu kundesha gari ikiwa 120km/h huku Rev ipo 3000 au 3500 na kuendesha 40km/h huku Rev ipo 2000 au 2500 itategemea gari inateknolojia gani VVTi au
Provided kila kitu kina baki constant, kwa gari hiyo hiyo, lazima mafuta utakayotumia kucover the same distance at a shorter period of time (faster) lazima yatakuwa mengi zaidi, this is a fact! Time is just as much a physical factor as Length and mass.
 
Kama wewe ni dereva, siku jaribu kuendesha kwa speed ya 40km/hr kwa muda wa lisaa limoja , hapa utakuwa umesafiri km 40; halafu jaribu kusafiri umbali huo huo wa km 40 kwa theluthi (1/3) ya lisaa, yaani tumia dakika 20 (endesha 120km/hr kwa muda wa dakika 20), hapa utakuwa umesafiri umbali ule ule wa Km 40 ila tu utakuwa umetumia muda mfupi mara tatu zaidi. Sasa kokotoa mafuta uliyotumia mara ya kwanza na yale uliyotumia mara ya pili. Utakuta kiwango cha mafuta uliyotumia mara ya pili ni kikubwa zaidi ya kiwango ulichotumia mara ya kwanza kwa mwendo wa taratibu, hivyo ili kuokoa muda kwa kuendesha haraka imetugharimu mafuta (pesa zaidi). Kama tofauti ya mafuta ni lita 10, je thamani ya muda uliookolewa katika case yetu hii ni shs.ngapi per minute?

USHAURI: Francis, naamini miongoni mwa faida za JF ni kuelimishana. Kwenye andiko lako kuna neno lenye ukakasi, na bila shaka tukiliacha liendelee, wengi watalitumia na kuiharibu lugha yetu. Kiswahili hakina neno "lisaa" wala "masaa". Badala yake kuna saa -hata kama ni moja au 20 -tuna "saa" tu. Nakuomba sana hili neno "lisaa" ulikwepe maana linaleta ukakasi kwenye lugha hii adhimu na ya kupigiwa mfano duniani.
 
Acha siasa jibu swali hii ndio shida ya watu wa arts maneno mengi
 
Umetumia gharama kubwa na kuwahi kufika eneo husika imekusaidia kukamilisha kazi zako na kupata muda wa ziada kupanga mipango mingine ya kifedha ambayo hiyo ndio italipia gharama zile za mafuta kwa hiyo hapo umepata faida.

Umetumia muda mrefu na gharama nafuu kufika kwenye kazi zako utafanya kazi kwa muda mfupi bila kukamilisha na kwa ufanisi wa chini maana utakuwa na uchovu wa safari kwahiyo hapo utakuwa umepata hasara
Mfano hai:-
- wewe ni fundi friji unatakiwa site ukarekebishe friji ukaamua kutumia usafiri wa bodaboda ambao ni gharama ikakucost elf 5 ukafika kule mapema ukakamilisha kazi ukalamba 30K ukawa na muda wa ziada kwenda kufanya kazi nyingine ambayo inakuingizia pesa.

- tuje upande mwingine wewe fundi friji umeamua kupanda daladala ambapo mpaka kufika site inakugarimu mia 6 lakini kutokana na foleni na kusimama kila kituo ukachelewa kufika eneo la tukio na uchovu kibao kwanza hutoimaliza kazi na ukiimaliza itakuwa chini ya kiwango.
Conclusion:
Time is money, ndio maana siwashangai wale wanaonunua Magari badala ya kujenga
 
Nimerudi,na moja kwa moja naingia kwenye mada.naassume kila mtu humu anajua misingi ya mwendo kwa kufuata kanuni za newton(newton's laws of motions).mada yetu inahusika zaidi na newtons second law(the acceleration of a body depends upon two variables,a force acting on a body and the mass(weight)of the body
Sasa consider katika hoja yako gari ni hilo hilo,mfano toyota brevis inatoka dar kwenda msata,assume umbali kati ya dar hadi msata ni km 40,siku ya kwanza,dereva alitumia saa 1 kufika msata,means gari ilitembea kwa speed ya 40km/hr.assume kwamba kutoka speed 0km/hr hadi 40km/hr alitumia sekunde 10,acceleration ya gari au rate ya badiliko la speed la gari(hii hubadilika kutokana na jinsi unavyokanyaga mafuta,ndiyo maana ikaitwa accelerator) ni {(40-0)*1000}/{3600*10}=1.11m/s^2.siku ya pili dereva huyo huyo alichukua gari hiyo hiyo akapita njia hiyo hiyo kwenda msata(assume pia factor zingine zipo constant),akatumia dakika 20,hivyo aliendesha kwa speed ya 120km/hr na kutoka speed ya 0km/hr hadi 120km/hr alitumia sekunde zile zile 10(hapa dereva alikanyaga sana mafuta)means acceleration yake sasa ikawa ni {(120-0)*1000}/{3600*10}=3.33m/s^2.
kiuhalisia siku ya kwanza dereva alitumia mafuta kidogo kufikia constant speed ya 40km/hr kwa sekunde 10 baada ya hapo gari ikawa inaunguza mafuta kwa constant rating ya gari kufuatana na mzunguko wa engine na gear ratio(assume katika speed 40km/hr engine revolution ni 1500rpm na gear ni namba 3,engine itakuwa inatumia nguvu yake kubwa kuzungusha gear kubwa ili kuovercome weight ya gari na opposing forces za kwenye gari ili kubalance speed ndogo,kitu ambacho ni waste.
katika case ya siku ya pili,dereva alitumia mafuta mengi kwa sekunde chache kufikia spidi ya 120km/hr na baada ya hapo katika speed kubwa gear inayoengage ni ndogo namba 5 kwenda mbele hivyo kwa revolution ile ile ya 1500rpm engine inatumia nguvu ndogo kuzungusha gia ndogo kubalance speed kubwa!

na hapa ndiyo maana katika specifications za ulaji wa mafuta hutolewa mara mbili kwa town trips na kwa highway,kwa highway consumption huwa ndogo kwa sababu nilizoeleza hapo juu na kwa town trip consumption huwa kubwa kwa factosr nilizotaja hapo juu na foleni,kuaccelerate mara kwa mara huchangia ongezeko la ulaji wa mafuta

CONCLUSION
thamani ya muda hupimwa kwa uwiano wa;muda mchache kwa shughuli unayocover kwa muda huo.dereva wetu hapo juu thamani ya muda kwake ilikuwa kubwa siku ya pili alipotumia muda mchache kusafiri kilometa nyingi
(next time nitakuja na faida na hasara za gari zenye cylinder nyingi kwa faida na hasara za gari zenye cylinder chache,)
thank you FRANCIS DA DON
 
Back
Top Bottom