Ukitaka kuichukia Serikali ingia JF mara nyingi

Sifieni ila ifikapo mwisho wake anatakiwa a Left wengine tuje tufanye yetu mwisho 2030. Hakuna raisi wa milele bongo Hapa
 
Hivi; huu upumbavu utakoma lini? Si Kila anaenungunika alikua hana kipato halali.
Haitaji kua na elimu ya msingi darasa 4, eti ndipo ujue madhira yanayo wakumba wakurima wa nchi hii kwa awam hii ya 5.wakulima wa Rudewa hawana wa kumuuzia Mahindi hata kwa hiyo bei ya kutupwa ya debe 1tsh 3000. nenda kagera ;kahawa mmekopa hamtaki kulipa.
Bado Mbao zimeshuka bei, cha ajabu mashamba yenu ya Mfindi, Buhindi, kyamunena. Hamjashusha bei za miti.
Mnajitoa ufaham? Au kweli hamnzo?
 
Kina makonda mpo wengi...kila akikosolewa jiwe mnaona ni jinai ilihali kumkosoa wakati mwingine ni kwa madhumuni ya kumjenga... mfano alivyochimba biti kwamba katiba mpya si kipaumbele chake kwa sasa ilikuwa ni habari ya kusherehekea kwa upande wako?
 
Dada wewe ni mnafiki au ni mvumilivu tu sio huichukii hii serikali. Ukweli ni huu ukiingia JF Mara kwa mara utaujua ukweli kuhusu serikali hii . Hivyo ni jukumu lako kuwa mvumilivu au uichukie.
 
Mkuu wapo wenye A/C 3 humuhumu kila muda wao wanafungua nyuzi tu za kumkejeli Mh Rais
 
Na bila kusahau ujenzi wa meli mpya ziwani viktoria na ufufuaji wa meli ya Mv. Viktoria
 
Nenda kasome gazette la Mzalendo, Tanzanite bila kusahau Uhuru [emoji648]
 
Ukweli ni kwamba threads ambazo zinatupiwa humu nyingi zinapandikiza chuki dhidi ya serikali.

Watu wapo kwaajili ya kusema mabaya tu ya serikali lkn hawataki kusema mazuri ambayo ni mengi zaid ya hayo mabaya.

Nilichogundua ni kwamba wanaichukia serikali wamegawanyika ktk makumdi yafustayo:

Kuna watu wameumbwa kupinga kila kitu anachofanya mtu mwingine hata kama ni kizuri.

Kuna watu wengine wanaambukizwa chuki bila kutafuta ukweli ,
kundi hili ni la watanzania wanaoishi nje ambao wanadhani kila kinachopostiwa humu ni cha kweli.

Kundi hili limepotoshwa na kujikuta linachuki kubwa dhidi ya serikali kwasababu tu wamechagua kupata habari kupitia jf ambayo imejaa wenye hila dhidi ya serikali.

Kundi jingine ni lile lililo wahanga walioharibiwa masrahi yao kwasabbu hawakutumia njia halali kuishi.

Kundi hili lina watu wa aina nyingi kama ifuatavyo, wapo walikuwa wanapata pesa kifisadi, waliokuwa wanaishi kwa kuuza madawa ya kulevya, waliokuwa wanakula mishahara ya wafanyakazi hewa, waliokuwa navyeti feki, walifukuzwa kazi kwa uzembe, wenye chuki binafsi na Mh. Rais na wapinzani.

Naomba niwe mkweli Rais Magufuri hana mpinzani mtaishia kumchafua hapa jf lkn kwenye jamii ya wanyonge tunamuona ni mkombozi wetu.

Ndiyo, ni mkombozi wetu kwa sababu amesababisha ya fuatayo, elimu bure, fyl over tazara , interchange ubungo, reli ya umeme, daraja la kigamboni, daraja la kilombero, upanuzi wa barabara ya moroco, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, ufanisi kwa watumishi wa serikali, ubora wa mfumo wa ulinzi wa ndani na nje ya nchi, kuboreshwa kwa bei ya korosho, kukua kwa pato la taifa, ununuzi wa ndege sambamba na kufufua shirika la ndege, ujenzi wa viwanda viingi, ongezeko la ajira, uhuru kwa machinga, mahakama ya mafisadi, kumaliza tatizo la kukatika katika kwa umeme, usambazwaji wa umeme mijini na vijiijin, uthibiti wa mwendo kasi kwenye mabasi ya abiria, na mengine meeeeengi lkn yoooote haya ni kwa kipindi cha miaka mitatu tu.

Nisemacho leo punguzeni chuki dhidi ya serikali semeni na mazuri acheni kujaza watu chuki dhidi ya serikali yao.

Ni maombi yangu Magufuri awe Rais wa milele wa nchi yetu tuone kama mtahama nchi.
Akili za kina Amber Rutty ni shida.we ni kusifu na kuabudu tu
 
Monicca, hoja yako imechoka sana kama kupenda kwako kunaishia kwenye haya uliyoandika hapa.
Ulipopambanua makundi yanayopinga hukuwa na ufahamu hata kidogo wa kutaka kujua kuwa kati ya hao wanaopinga si kwa sababu hizo ulizoorodhesha wewe. Kuna wengi tu wanayoyapenda hayo mazuri yanayofanywa na serikali, lakini wanachukizwa na mambo ya msingi zaidi yanayokiukwa na viongozi hao hao. Uongozi unapokiuka mambo ya msingi kama uhuru na haki, uongozi huo hata ufanye mazuri gani hauwezi kukosa upinzani

Ndio, ni kweli kabisa, kuna watu mbalimbali ambao misingi ya upingaji wao ni kunyimwa ulaji n.k. Hawa wapo sana humu JF. Lakini fahamu kuwa ni serikali hiyo hiyo inayowaongezea ujiko kwa kutenda yasiyo ya haki ambayo wapinzani wa kweli wanayapigania.

Usipende kurahisisha upinzani kwa serikali kwa kufumbia mabaya inayoyafanya serikali. Sote tungependa sana serikali yetu ipigane vita ngumu ya kulinda mali za waTanzania zisifujwe na kuliwa na watu wachache. Inapofanya hivyo ihakikishe haitendi nje ya taratibu na sheria zilizopo. Kama hazipo sheria hizo, kuna taratibu za kuziweka na isiwe ni kutumia mabavu tu kwa vile kuna vyombo vya dola nyuma yake.

Rais Magufuli angefuata taratibu katika mambo mengi anayoyatenda hadi sasa, wapinzani wake wangekuwa na kazi ngumu sana ya kumpinga. Ni njia anazotumia ndizo zinazoharibu hata hayo mazuri tunayoyataka wengi wetu.

Kwa hiyo Monicca, usitake kutanguliza hoja yako ionekane kuwa kila asiyependa yanayofanywa na uongozi wa Mh Magufuli hana akili za kupambanua yanayoonekana. Huna uwezo wa kufikiri kwa niaba ya wengine.
 
Sasa Mkuu kwanini wewe usiweke hayo mazuri?
Ameyaweka kwenye aya ya mwisho.
Ina maana, kwake akisha kula na kwenda chooni maisha yamekamilika, hana matarajio zaidi ya hapo katika maisha yake.
Wapo watu wengi sana wenye mawazo kama haya; na ni hawa ndio wanaosababisha matatizo makubwa katika nchi nyingi.
 
Mimi naingia Mara nyingi halafu siichukii Serikali na ninaamini kuwa si kwamba wanaJF ni kundi la kuichukia Serikali. Humu wapo watu wa aina zote. Hata viongozi wa ngazi za juu za Serikali wapo na wanaendelea kuipenda Serikali. Tena wengine hawapiti kabisa Jukwaa la Siasa, wanamajukwaa yao. JF ni ya kila mtu jomba, usitutangaze vibaya huko nje.
 
Ukweli ni kwamba threads ambazo zinatupiwa humu nyingi zinapandikiza chuki dhidi ya serikali.

Watu wapo kwaajili ya kusema mabaya tu ya serikali lkn hawataki kusema mazuri ambayo ni mengi zaid ya hayo mabaya.

Nilichogundua ni kwamba wanaichukia serikali wamegawanyika ktk makumdi yafustayo:

Kuna watu wameumbwa kupinga kila kitu anachofanya mtu mwingine hata kama ni kizuri.

Kuna watu wengine wanaambukizwa chuki bila kutafuta ukweli ,
kundi hili ni la watanzania wanaoishi nje ambao wanadhani kila kinachopostiwa humu ni cha kweli.

Kundi hili limepotoshwa na kujikuta linachuki kubwa dhidi ya serikali kwasababu tu wamechagua kupata habari kupitia jf ambayo imejaa wenye hila dhidi ya serikali.

Kundi jingine ni lile lililo wahanga walioharibiwa masrahi yao kwasabbu hawakutumia njia halali kuishi.

Kundi hili lina watu wa aina nyingi kama ifuatavyo, wapo walikuwa wanapata pesa kifisadi, waliokuwa wanaishi kwa kuuza madawa ya kulevya, waliokuwa wanakula mishahara ya wafanyakazi hewa, waliokuwa navyeti feki, walifukuzwa kazi kwa uzembe, wenye chuki binafsi na Mh. Rais na wapinzani.

Naomba niwe mkweli Rais Magufuri hana mpinzani mtaishia kumchafua hapa jf lkn kwenye jamii ya wanyonge tunamuona ni mkombozi wetu.

Ndiyo, ni mkombozi wetu kwa sababu amesababisha ya fuatayo, elimu bure, fyl over tazara , interchange ubungo, reli ya umeme, daraja la kigamboni, daraja la kilombero, upanuzi wa barabara ya moroco, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, ufanisi kwa watumishi wa serikali, ubora wa mfumo wa ulinzi wa ndani na nje ya nchi, kuboreshwa kwa bei ya korosho, kukua kwa pato la taifa, ununuzi wa ndege sambamba na kufufua shirika la ndege, ujenzi wa viwanda viingi, ongezeko la ajira, uhuru kwa machinga, mahakama ya mafisadi, kumaliza tatizo la kukatika katika kwa umeme, usambazwaji wa umeme mijini na vijiijin, uthibiti wa mwendo kasi kwenye mabasi ya abiria, na mengine meeeeengi lkn yoooote haya ni kwa kipindi cha miaka mitatu tu.

Nisemacho leo punguzeni chuki dhidi ya serikali semeni na mazuri acheni kujaza watu chuki dhidi ya serikali yao.

Ni maombi yangu Magufuri awe Rais wa milele wa nchi yetu tuone kama mtahama nchi.
Kwahiyo JF nzima majukwaa yote ni kuisema serikali tuu? Hapa umewaza kimo cha mbilikimo... By the way hivi unaweza kuzuia mitazamo ya wengine? Hivi serikali ina ukamilifu kiasi gani mpaka isikosolewe?
 
Ameyaweka kwenye aya ya mwisho.
Ina maana, kwake akisha kula na kwenda chooni maisha yamekamilika, hana matarajio zaidi ya hapo katika maisha yake.
Wapo watu wengi sana wenye mawazo kama haya; na ni hawa ndio wanaosababisha matatizo makubwa katika nchi nyingi.
Kiukweli inasikitisha, yaani ni wengi sana, juzi wakati Zitto ametoka mahakamani pale akawa anasema kuwa "Nchi haiko sawa" wife akarukia akasema nchi haiko sawa kivipi mbona mimi naona mambo fresh tu, nikamtazamaaaaa halafu nikaamua kutoka zangu nje tu maana kilichokua kinafuata ni ubishi na mwisho wa siku angekula makofi.
 
Back
Top Bottom