Ukitaka kuichukia Serikali ingia JF mara nyingi

Ukitaka kuichukia Serikali ingia JF mara nyingi

Ni wewe ulivyojiandaa kupokea yatokayo humu,
 
Labda hana mpinzani kwenye ndoa ya bi mdashi wako hivyo anamshinda kete mshua wako
 
siwezi kuchukia ila nasikitikia mtu mzima kuwa na akili ndogo,kushabikia tu kwa kufuata mkumbo kisa njaa kukusumbua.
Na mtaliwa sana!!
Lazima nishabikie maana tuna serikali imara isiyoyumbishwa na yeyote yule..naamini itakuwa serikali ya kudumu
 
Lazima nishabikie maana tuna serikali imara isiyoyumbishwa na yeyote yule..naamini itakuwa serikali ya kudumu
Serikali imara kwa kufanya mauaji kwa wasio na hatia?
Kuteka watu na kusingizia wasiojulikana?
Yakimkuta mtu wako utakuja elewa,sikulaumu huenda sio kosa lako ila ni la jinsia yako
 
Hii leo umeandika wewe? Au nayenyewe ni ya ngono?
Sasa kwa jinsi unavyowaza na kuandika ngono muda wote unaweza kuwaza nje ya hapo kweli? Hebu niambie ukweli haujaandikiwa na mdogo wako wa primary kweli?
 
Serikali ina wajibu wa kufanya hayo yote umeeleza na zaidi, pia wananchi wana haki kupongeza na kukosoa kila jambo kuhusu mustakabali na maslahi ya Nchi/Taifa lao.
Jamiiforums ni sehemu pekee wananchi wachache wanaweza kuweka hisia zao juu ya jambo lolote lenye mashaka dhidi ya serikali, hapo tunazungumzia ukosoaji na mapendekezo mengine. Lakini ukitaka kupongeza serikali popote pale upo huru na vyeo unaweza pata on spot, kwa hivo nadhani umepata jibu kwanini JF na si kwingineko unakutana na hicho unachotafsiri ni chuki.
 
Unapokimbilia kutoa matusi means umeishiwa points na umshapanic
Kuna tusi hapo? Tatizo la JF kwa sasa tuna GT wachache Sana wanaochangia wengi wamekuwa wasomaji tu na hii ni kwa sababu wengi hawajui maana na kwa vile hawaulizi maana hawaambiwi maana, sema tena nimetukana
 
Ukweli ni kwamba threads ambazo zinatupiwa humu nyingi zinapandikiza chuki dhidi ya serikali.

Watu wapo kwaajili ya kusema mabaya tu ya serikali lkn hawataki kusema mazuri ambayo ni mengi zaid ya hayo mabaya.

Nilichogundua ni kwamba wanaichukia serikali wamegawanyika ktk makumdi yafustayo:

Kuna watu wameumbwa kupinga kila kitu anachofanya mtu mwingine hata kama ni kizuri.

Kuna watu wengine wanaambukizwa chuki bila kutafuta ukweli ,
kundi hili ni la watanzania wanaoishi nje ambao wanadhani kila kinachopostiwa humu ni cha kweli.

Kundi hili limepotoshwa na kujikuta linachuki kubwa dhidi ya serikali kwasababu tu wamechagua kupata habari kupitia jf ambayo imejaa wenye hila dhidi ya serikali.

Kundi jingine ni lile lililo wahanga walioharibiwa masrahi yao kwasabbu hawakutumia njia halali kuishi.

Kundi hili lina watu wa aina nyingi kama ifuatavyo, wapo walikuwa wanapata pesa kifisadi, waliokuwa wanaishi kwa kuuza madawa ya kulevya, waliokuwa wanakula mishahara ya wafanyakazi hewa, waliokuwa navyeti feki, walifukuzwa kazi kwa uzembe, wenye chuki binafsi na Mh. Rais na wapinzani.

Naomba niwe mkweli Rais Magufuri hana mpinzani mtaishia kumchafua hapa jf lkn kwenye jamii ya wanyonge tunamuona ni mkombozi wetu.

Ndiyo, ni mkombozi wetu kwa sababu amesababisha ya fuatayo, elimu bure, fyl over tazara , interchange ubungo, reli ya umeme, daraja la kigamboni, daraja la kilombero, upanuzi wa barabara ya moroco, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, ufanisi kwa watumishi wa serikali, ubora wa mfumo wa ulinzi wa ndani na nje ya nchi, kuboreshwa kwa bei ya korosho, kukua kwa pato la taifa, ununuzi wa ndege sambamba na kufufua shirika la ndege, ujenzi wa viwanda viingi, ongezeko la ajira, uhuru kwa machinga, mahakama ya mafisadi, kumaliza tatizo la kukatika katika kwa umeme, usambazwaji wa umeme mijini na vijiijin, uthibiti wa mwendo kasi kwenye mabasi ya abiria, na mengine meeeeengi lkn yoooote haya ni kwa kipindi cha miaka mitatu tu.

Nisemacho leo punguzeni chuki dhidi ya serikali semeni na mazuri acheni kujaza watu chuki dhidi ya serikali yao.

Ni maombi yangu Magufuri awe Rais wa milele wa nchi yetu tuone kama mtahama nchi.
Nani tena?musiba umetumia acc ya mke wako.
 
Back
Top Bottom