Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 968
- 542
Hapa kazi tu. Siangalii aina ya kazi, ninachoangalia ni uhalali wa kazi. Kazi yoyote halali nitaifanya ilimradi tu wajibu wangu kama Baba kwa wanangu, kwa mke wangu na wategemezi wangu nautimiza. Kuchagua kazi kwangu ni mwiko. Elimu yangu si kikwazo kwangu kufanya kazi zilizo nje ya taaluma yangu. Sihitaji kuonekana kwa watu navaa tai nzuri na koti kiatu cheusi kilichong'arishwa vyema nafanya kazi kwenye ofisi yenye kiyoyozi kizuri ilihali maslahi yangu ni duni.
Ni bora niitwe kichwa Mbovu na watu huku mwenyewe nikitambua kuwa kichwa changu ni kizuri kuliko wote na mawazo yangu ndiyo tegemeo kwa watu wengi. Lazima nisimame imara nitengeneze njia wengine wapite pasipo na kikwazo. Siku zote sieleweki na wala sitabiriki lakini ndivyo nilivyo. Kuna ambao wanaonielewa kidogo na hata kudiriki kunifuata. Daima nasimamia kile ninachokiamini hata kama nikibezwa na wote. Wakati mwingine natumia busara siwezi kumkatisha tamaa mtu juu ya mawazo anayonipa pale ninapoyaona hayana msingi kwangu. Sikubali kukwamishwa daima nitatafuta njia ya kuruka kizingiti katika namna ya ajabu. Utashituka kikwazo chako nimekikwepa na Mwenyezi Mungu daima ananisimamia na kuniongoza. Kila siku naibuka na wazo jipya maendeleo ya watu ndiyo ninayoyataza zaidi hata kama si mwanasiasa, sitaki kuona anayejaribu akikwama.
Siishi kuwaduwaza watu kwa namna nilivyo, maisha niishiyo, mchangamo wangu na watu pamoja na mashirikiano. Natambua thamani ya marafiki, nikiwa na shida hata na raha, rafiki anakuwa msaada mkubwa kuliko ndugu. Sihitaji kujenga chuki na mtu wala kutengeneza uadui, nahitaji kuongeza marafiki wenye msaada kwangu. Siwakani ndugu zangu, nafasi yao kubwa na muhimu kwangu. Lakini maisha ya ubakini rafiki wana umuhimu mkubwa. Ingawa kuna wengine ni wanafiki ni muhimu kuwatambua na kwenda nao kwa tahadhari kubwa, vinginevyo watakuwa sababu ya kukudondosha.
Kujifunza hakuna ukomo. Na mwalimu si lazima awe Profesa wa chuo kikuu ama Daktari. Hata muhitimu wa darasa la saba au asiyesoma kabisa anaweza kuwa mwalimu mzuri katika kukufundisha maisha. Dharau ikiwekwa kando ndiyo msingi wa kufanikiwa. Usisahau uliko toka. Maisha yako ni historia yenye mafunzo mazuri ya kukukumbusha ulikotoka na ulipo. Ni muhimu kuienzi. Mapito yako, changamoto zako pamoja na Fursa ulizopitia ndizo zinazokufanya uonekane ulivyo.
Mafanikio yako yana mchango mkubwa kutoka kwa mke wako. Usithubutu kumdharau kwa namna yoyote ile. Mshirikishe, Msikilize na mjadiliane kwa hoja katika kila jambo unalotaka kilifanya. Pesa haitakiwi ikubadilishe. Jiweke katika namna ambayo siku ukiwa na pesa au huna pesa uonekane uko vilevile, hujabadilika. Pesa haipaswi kukuchanganya. Pesa inapaswa iwe nyenzo ya kukutumikia katika kuboresha maisha.
Dunia yetu ni mapito, usimdharau mtu wala kumdhulumu.
Aman Ng'oma
0767989713
Dodoma
Tanzania.