Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

anonimuz

Senior Member
Nov 5, 2007
102
71
daladala-dar-es-salaam.jpg

Mambo vipi wakuu,

Nimeamua kujikita kwenye biashara ya daladala na bado nipo kwenye hatua ya utafiti. Nimepitia threads nyiiingi sana humu na watu wengi wanaoipiga vita hii biashara wanakuwa na hoja za "Biashara pasua kichwa", "Madereva watakunyonga" n.k bila kuelezea kiundani changamoto wali/nazopata katika biashara hii. Madhumuni ya thread hii ni kutaka kupata ushauri

1) Kutoka kwa watu ambao walifanya hii biashara ikawashinda. Watueleze matatizo waliyokumbana nayo.

2) Kutoka kwa watu ambao bado wanafanya hii biashara na inaenda vizuri. Watueleze namna wanavyoiendesha na kukabiliana na matatizo ya hapa na pale. Tukipata watu wakatupa mfafanuo wa gharama na mapato itakuwa vizuri zaidi.

3) Kutoka kwa watu wenye uzoefu thabiti wa magari kuhusu aina ya magari (Toyota Hiace, Toyota Coaster, Isuzu, Nissan etc) yanayofaa kwa biashara hii. Mapungufu na faida ya kila aina.

4) Juu ya hili: Nimeamua kuanza kwa kununua Nissan Civilian mbili ila baadhi ya ndugu, jamaa, na marafiki wanatoa ushauri wa kwamba uimara wa gari hizi ni wa wasiwasi, "spare" mgogoro etc. Mwenye ufahamu juu ya hili tafadhali. Hasa wale ambao wanamiliki magari haya.

5) Juu ya hili: Nimekua nikifanya malinganisho ya gharama na mapato ya uendeshaji kwa Dar na mikoani ila bado sijafikia hatua ya kuamua ipi inalipa zaidi. Wale wenye biashara hii Dar NA mikoani, tunaomba muongozo wenu hapa

Mwisho ningependa wamiliki na wadau wengine watueleze wanauonaje muelekeo wa biashara hii kwa Dar, sasa ambapo DART ipo njiani.

Nafahamu kuwa ni rahisi mno mtu kuchangia "thread" kiushabiki zaidi kwa kuandika "one liner posts" kama "biashara pasua kichwa" na kadhalika ila ningependa tuweke ushabiki pembeni na tujitahidi kuchangia uzi huu kutokana na uzoefu tulionao kwenye biashara hii na kufafanua hoja zetu.


WADAU WENGINE WANAHITAJI KUJUA NINI KUHUSU BIASHARA HII?
Umuofia kwenu!

Jamani mimi ni employee katika private sector. Katika kufikiria namna ya kujiongezea kipato nimewaza kukopa pesa benki ili niagize hiace na nianze kupiga ruti za Kasulu-kigoma au kasulu-kibondo. Hii Biashara sijawahi kuifanya ila nategemea kuisimamia baada ya kutafuta dereva anayeweza kuaminika.
Ningependa kujua yafuatayo;

1. Hiace aina gani inayofaa?
2. Kwa mazingira ya Kigoma engine gani inafaa? CC zake pia aina ya mafuta (diesel/petrol)
3. Profit margin ya huku ikoje, katika misimu ya mvua na kiangazi?
4. Ningependa kujua pia kuhusu bima ya gari ya Biashara kama hii ya hiace, especially comprehensive/premium ikoje?
5. Kama nimenunua from Japan, gharama ya kuweka viti vya abiria ikoje?
6. Pia ningependa pia kujua chochote kile kinachohusiana na biashara hii kutoka kwa wazoefu/majongwe wa biashara hii.

NB:
Kasulu-kigoma ni 90 km na nauli ni Tsh. 5,000/= na
Kasulu -Kibondo ni 150 km na nauli ni Tsh. 10,000/=.
Barabara zote ni za vumbi na gari linaweza likaenda na kurudi kwa siku bila shida.

Thanks!


MICHANGO TOKA KWA WADAU
UELEWA WA KINA KUHUSU BIASHARA HII

Sorry wakuu kwa kuwaletea mada ambayo ni ya muda mrefu toka iandikwe but mimi nimeisoma leo na nimejifunza kitu nikaona ngoja niwaleetee wadau ambao hawakupata kuiona nao wajifunze jambo kidogo

Baada ya kununua basi dogo la kwanza (Hiace) na kulisajili kwa biashara ya kusafirisha abiria Mjini (daladala); nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto ziliponizidia niliaazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri. Nikamfuata mzee wangu mmoja hapa Mjini Iringa ambaye ameanza biashara ya kusafirisha mizigo na abiria tangu mwaka 1978.

Mzee wangu huyu baada ya kunisikiliza aliniambia sentensi moja tu na akasema huo ndio ushauri anaonipa na ambao utanisaidia. Alisema hivi, Kijana wangu! Ili umudu biashara ya magari hasa hizi daladala unatakiwa uwe mjeuri-jeuri kwa madereva, makondakta na wakati mwingine kwa matrafiki. Nikataka anipe ufafanuzi kuhusu hili ndipo akaongeza ufafanuzi huu, Hawa watu ninaokwambia usicheke nao ndio ambao wanaweza kukuliza ama kukufanya ufurahi. Ukizubaa katika hili usishangae kujikuta muda umepita, gari limechakaa na faedha za kununulia gari jingine huna.

Ushauri wa mzee wangu huyu niliufanyia kazi na ulizaa matunda (kwangu) Uzoefu wangu katika biashara hii ya daladala unachagizwa pia na nafasi ya uongozi niliyoapata kushika kuanzia mwaka 2009 hadi januari 2012. Nilikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi ya abiria mkoani Iringa kinachojumuisha magari yote ya abiria ukiacha mabasi ya mikoani. Nafasi hii ilinipa kufahamiana na kushirikiana na wafanyabiashara wengi wa magari ya abiria Iringa. Hivyo nafahamu chungu na tamu za biashara ya daladala na machozi yao nayajua.

Ukiacha changamoto ya faida (ambayo nitaichambua kwa kina kwenye makala hii) biashara ya daladala ina timbwili-timbwili si mchezo. Madereva wanasumbua sana, faini za barabarani zisizoisha na uharibifu wa magari ni kama chachandu chungu kwenye biashara hii.

Kati ya biashara nilizowahi kuzifanya biashara ya daladala inaongoza kwa kupasua kichwa Miezi machache iliyopita wamiliki wa daladala-Dar es Salaam waliwasilisha kusudio la kupandisha nauli za daladala kwa asilimia mia tatu (300%) mbele ya baraza la watumiaji wa huduma za usafiri.

Baraza hilo pamoja na SUMATRA waliwagomea wamiliki wa daladala kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu hizo ni pamoja na Mosi; wamiliki wa daladala walishindwa kuwasilisha taarifa za kifedha za biashara zao.(Approved financial statements) Pili sababu walizozitoa kuhusu kupanda gharama walidai (exagrated) zilikuzwa mno na kukosa ushahidi wa bei katika soko. Baada ya kufuatilia mnyukano ule niliwahurumia sana wamiliki wa daladala kwa sababu wenye rungu la kuwasaidia hawajui viatu vya umiliki wa daladala vinavyobana na kuumiza.

Nimetafiti biashara hii katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Dodoma huku Iringa nikiwa nimeifanya kwa vitendo. Sehemu karibu zote changamoto zinafafanana ingawa kuna tofauti ndogo ndogo kutegemea na tamaduni za kimaeneo. Sehemu hizi zote viwango vya fedha inayolazwa ni shilingi kati ya elfu thelethini (30,000) na elfu arobaini (40,000) kwa siku kwa mabasi madogo (Hiace Super Roof). Kwa mabasi ya kati (Coaster) kiwango kwa siku ni kati ya elfu hamsini (50,000) hadi elfu themanini (80,000) kwa siku. Sasa twende kimizania ya uhasibu hapa.

Bei ya kununua basi dogo (Toyota Hiace Super Roof) pamoja na kusajili leseni, njia, na taratibu zote ili ianze biashara ni kati ya shilingi milioni ishirini hadi milioni ishirini na tano (20M-25M). Bei ya kununua basi la kati (Coaster) ni kati ya milioni thelathini na tano hadi milioni arobaini na tano (35-45). Magari hayo yote ni yale yaliyotumika kule Japan (Used Cars) Tukokotoe mahesabu ya basi dogo.

Kwa upande wa mapato kama gari inalaza shilingi elfu 30 kwa siku ina maana kwa mwezi unakusanya shilingi 840,000 (laki nane na arobaini elfu). Hesabu hizi ni kwa siku ishirini na nane. Siku mbili kikawaida hutengwa kwa ajili ya kufanya service ya gari ambayo ina fanyika kwa mwezi mara mbili kila baada ya siku 14.

Tushuke kwenye matumizi. Galoni moja la kilainishi kizuri(oil) ni shilingi elfu 45, gharama ya kubadilisha sahani za breki ni shilingi 25, vifaa ambatanishi vya service ni karibu shilingi 20. Ukichanganya na ufundi na ikiwa unafanya service ya uhakika katika gari lako kila service moja unatumia shilingi laki moja kwa kadirio la chini.

Katika kipengele cha service kwa mwezi unatumia kama laki mbili. Mshahara wa dereva kwa mujibu wa sheria za SUMATRA zinazoambatana na masharti ya kupewa leseni yanakutaka mmiliki wa gari ulipe kuanzia kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi shilingi elfu themanini. Kodi za serikali ikiwemo leseni ya barabara, leseni ya njia, zima moto, mapato na ushuru wa manispaa/jiji ni wastani wa shilingi elfu sitini kadirio la chini.


Nyingi ya kodi hizi zinalipwa kwa mwaka lakini hapa nimezigawanya katika mafungu ya miezi 12. Mwisho tujumlishe mshahara wa wewe Mjasiriamali unayemiliki gari. Najua wajasiriamali wengi hawana utaratibu wa kutenga mishahara yao kwa biashara zao, lakini hata kama hutengi mshahara tukadirie kuwa unajilipa shilingi elfu themanini tu kwa mwezi.

Sasa ukichukua mishahara ukajumlisha na kodi ukajumlisha na gaharama za matengenezo (service) unapata matumizi ya shilingi laki nne na ishirini elfu (420,000). Kiharaka haraka unaweza ukadhani faida inayobaki ni shilingi laki nne na ishirini (420,000).

Hapa ndipo wafanyabiashara wengi wa magari ambapo hufilisikia kwa kusahau jambo la muhimu kuliko yote. Jambo hili la muhimu ni gharama ya uchakavu wa gari (depreciation cost). Gharama hii kitaalamu hutakiwa kujumuishwa kwenye kipengele cha matumizi.

Tunaposema gharama ya uchakavu ni pale unapoelewa kuwa ikiwa gari inatembea basi tairi zinazidi kuisha, vyuma vinasagika na bodi linachakaa. Kinachoamua kiwango cha gharama ya uchakavu ni makadirio ya muda ambao gari lako litakaa kabla ya kuchakaa kabisa. Kuna njia kadhaa za kitaalamu lakini hapa nataka nitumie njia rahisi ya kijasiriamali ili tuelewe vema.

Mathalani kama gari yako inapita kwenye barabara nzuri unaweza kukadiria kuwa uhai wa gari lako utakuwa ni miaka mitano. Unachofanya unachukua thamani ya kununulia hadi kusajili gari ianze biashara kisha unagawanya kwa miaka mitano. Twende pole pole hapa.

Tumesema wastani wa chini wa basi dogo ni shilingi milioni 20 hadi ianze biashara. Ukichukua milioni 20 ukagawanya kwa miaka mitano unapata shilingi milionI 4 ambayo ndio gharama ya uchakavu kwa mwaka. Sasa chukua milioni hii 4 kisha gawanya kwa miezi kumi na mbili unapata wastani wa shilingi 333,000 (laki tatu na thelathini na tatu elfu). Hii fedha tunaiingiza kwenye sehemu ya matumizi.

Kwa maana hiyo jumla kuu ya matumizi yetu kwa mwezi inakuwa ni shilingi 753,000/=(laki saba na hamsini na tatu elfu). Ili uelewe faida HALISI unayozalisha kwa mwezi chukua mapato ya mwezi (840,000) kisha utoe na matumizi ya mwezi (753,000). Ukikokotoa hapo utaona faida HALISI ya biashara ya daladala ikiwa una basi dogo kwa mwezi ni shilingi elfu themanini na saba (87,000/=) tu! Najua mahesabu haya yatawastua wengi na wengi wanaweza wasiyaelewe na kwa kutoyaelewa wanaweza wasiyakubali. Bahati nzuri ni kuwa nimeshafanya biashara hii huku nikiwa na digrii ya biashara kutoka chuo kikuu hivyo naelewa ninachokisema hapa. Labda nitafsiri maana ya mahesabu hayo hapo juu kwa lugha nyepesi na ya picha.

Iko hivi; ukinunua gari la milioni 20 leo, baada ya miaka 5 linaweza kuwa limeshachakaa kabisa. Wakati huo gari litakapochakaa unatakiwa uwe na fedha mkononi za kununua gari jingine kutoka katika biashara hiyo hiyo na ubakiwe na fedha nyingine ambayo ndiyo tutaiita FAIDA. Ile hela utakayorudishia gari lililochakaa ni mtaji ulioanza nao. Kwa mahesabu hayo hapo juu ambapo tumeona faida HALISI ya daladala ikiwa unamiliki Hiace Super Roof ni shilingi elfu themanini na saba kwa mwezi.

Kwa faida hiyo (@87,000/=) itakuchukua Mjasiriamali miaka 19 ili afanikiwe kununua gari jingine la pili! Mliowahi kufanya biashara ya daladala mtakubaliana nami kuwa; ukiona mtu ameongeza daladala ya pili ndani ya mwaka mmoja ama miwili basi uwe na uhakika kuwa fedha ya kununulia gari ya pili hajaitoa kwenye gari ya kwanza kwa asilimia mia moja.

Ni ama amechukua mkopo au fedha ameongezea kutoka vyanzo vingine. Naomba nieleweke vema hapa. Sisemi kuwa biashara ya daladala hailipi, la hasha! Lakini faida HALISI iliyopo kwenye daladala ipo tofauti sana na vile SUMATRA na abiria wanavyoitazama ama kuifikiria.

Mtazamo na mawazo ya wadau hawa ndio yamekuwa yakisababisha kuwakatalia wenye daladala ama kuwakubalia kwa mbinde kila wanapotaka kuidhinishiwa kupanda kwa nauli. Mathalani, kilainishi (oil) ambacho mwaka 2006 kilikuwa kikiuzwa shilingi 19,000/= leo kinauzwa 45,000/=. Tairi ambalo wakati huo liliuzwa kwa shilingi 85,000/= leo linauzwa 165,000/=. Gari lililokuwa linauzwa milioni 12M mwaka 2006 leo linauzwa milioni 22M (Toyota Hiace Super Roof).

Kwa mabadiliko hayo nauli za daladala zilitakiwa zipande kwa asilimia 236% kutoka mwaka 2006 hadi leo. Lakini hali ni kinyume, kwani maeneo mengi nauli ya daladala imeongezeka kwa kati ya shilingi 50 hadi 100 ongezeko la kati ya asilimia 25% hadi 50% tu.

Ndio maana SUMATRA na baraza la watumiaji walipowagaragaza wamiliki wa daladala kwa kufutilia mbali madai yao ya kupandisha nauli, nilijichekea na kusikitika tu. Hata hivyo sina neno na wala sina lawama kwa SUMATRA wala baraza la watumiaji; kwa sababu wenye daladala wenyewe walishindwa kujitetea utetezi wenye nguvu za hoja.

S
ource: suleimanmagoma.blogspot.com

UZOEFU: CHANGAMOTO YA MADEREVA KUTOKUWA WAAMINIFU
Nilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.

Leo dereva anakwambia center-ruber imeisha, kwa hiyo badala ya Tsh 40,000 unapata 15.Kesho asbh ndo kwanza unaingia ofisini anakwambia timing belt imekatika...inatumika pesa ya jana na haitoshi inabidi utoe yako mfukoni.

Siku ya tatu na ya nne akikuhurumia ukakusanya 80 basi siku inayofuata unaambiwa nimepigwa bao na majembe. Ilikuwa nilipe 250,000 so nimewapoza 35,000. so hesabu yako mkuu hii hapa elfu tano! Gosh!!!

Picha hizo zimeendelea mpaka nikatia shaka, akipiga dereva wkt mwingine nachomoka kuthibitisha tatizo. Ajabu! Mara kadhaa ni uongo kunakuwa hakuna cha majembe wala mashoka! Bse of that nimewatimua kila nikigundua usanii huo, ndani ya mwezi 1 madereva wanne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.

Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!
UZOEFU: SUALA LA UAMINIFU WA DEREVA NA KONDAKTA

Kwa mtu aliyewahi fanya hiyo biashara anaweza kukuelewa kiurahisi sana ni magumu mangapi unayapitia. Believe me, madereva wengi wa daladala hawana shukrani, me nina hiace na nimewapa hesabu ndogo tu walete 30,000 kwa siku na mara zote siku za sikukuu yoyote ile iwe ni Idd, Pasaka au Krismas. Huwa nawaachia siku moja ili wapate hela ya sikukuu, lkn ndugu yangu ni kama kosa. Kila siku ni visa, mara majembe, mara tairi lina pancha, mara pump wakati siku ukiwa free na ukiwakomalia unakuta hamna ugonjwa wowote wa gari na gari bado iko safi kabisa!

Hao jamaa ni wezi hawana mfano! Utakuja filisika and then watakucheka! Inabidi tu utafute tender ya shule, hoteli ... au utafute dereva mwingine mzuri (sijui utamtoa wapi manake kigamboni madereva wote wanajuana pale na ndio tabia yao).

Believe me, njia za kule zina hela sana, si Tungi, Kisiwani, Vijibweni, wala Kibada. Hesabu wanapata ila mtakuwa mnagawana nusu kwa nusu!

Ningekushauri utafute dogo mmoja wa kitaa unayemuamini then asimamie gari yako na yeye ndo akuletee hesabu na uwe unampoza ... me i did the same and it worked out mpaka huyo dogo alipoenda shule then wakaanza upumbavu wao tena. Now nimewatishia kuwatimua ndo kidogo wamejirekebisha lkn ni presha tupu!

pole sana!
USHAURI: MSHAHARA NA UKOMO WA DEREVA KUHUSU GARI
Kila biashara/shughuri yoyote ina ugumu na karaha zake

Biashara ya daladala inalipa na ni nzuri kwa wale wasio na muda mchana .As rule of thumb. HIACE (Tajiri=24days x 45,000/=, Service= 2days x 45,000/=, trafic &s umatra & majembe=2days x 45,000/=, Dereva= 2days x 45,000/=).Break even ni 22months.
Hayo ndiyo mahesabu ya makadirio kwa uzoefu.

Katika utafiti nilioufanya wamiliki wa daladala wanaoendelea vizuri wanafanya yafuatayo bila kukosa.

1. Hakikisha siku ya service gari inatengenezwa vizuri na unasimamia
2. Gari yako iwe nzima sana (pesa ya gari si yako hadi utakaporudisha mtaji).
1. Mafuta full tank ni ya tajiri, yanakaguriwa kituo cha mafuta au anapopaki daily.
2. Leseni na certificate vyote original anashika tajiri
3. Mshahara kwa mwezi kwa hiace ni 50,000/= coaster ni 90,000/= kwa mwezi.
4. Akilete hesabu pungufu, akipoteza suti, jeki, spanner au uzembe wowote unaandika deni anakatwa mwisho wa mwezi.
5. Ajira yake iwe na referee, barua ya mjumbe na ujue kwake na awe ameoa
6. Ukiendesha gari kwa miezi 30 fikiria kuuza, kwa kuwa hiyo ndo faida safi
7. Chagua garage 2 zenye mafundi unaowaamini ili ukipigiwa simu, nawe unawaelekeza dereve apeleke garage unatakayo mwambia,

DEREVA ASIPEWE MADARAKA YA KUTENGENEZA GARI YAKO

Hayo machache, pia maguta yana karaha/kero sana, ila ukifanya kama ndo maisha yako inakutoa kama vile daladala.
HAKIKISHA USALAMA NA UZIMA WA GARI KILA SIKU

Pole sana ila zingatia ushauri huu: Kwanza kabisa hakikisha magari yako wakati wote ni mazima na hayana hitilafu yeyote inayoweza kuyafanya yasimame. Pili hakikisha kila siku unasoma millage kabla gari halijaanza safari na mara limalizapo safari zake. Tatu hakikisha madereva unaowakabidhi g magari yako wana lesseni halali za udereva na hakikisha unawafahamu vizuri, makazi yao, wadhamini na viongozi wao wa serikali za mitaa wanayoishi na ikiwezekana wawe na wadhamini wakuaminika.

Hakikisha kuwa kila wakimaliza kazi jioni/usiku, unapima (mwenyewe kiasi cha mafuta kilichobaki na kuongeza hadi kiasi ambacho unajua kitatosha kwa kazi ya kesho) awali nilikueleza kuwa hakikisha kuwa unarekodi millage ili kujua ni umbalii gani kwa siku gari yako inasafiri, hii itakusaidia kujua wastani wa mafuta yanayohitajika kwa siku. Kwa nchi kama kenya madereva hupewa sheet maalumu ambayo hurikodi mlolongo mzima wa safari na gharama zote ambazo dereva atakuwa ametumia
kwamfano:

Ubungo - posta -abiria 24 @ sh 300 =7200/= km 9
posta -Ubungo- abiria 30@ sh 300=9000/= km 9 n.k

Aidha unatakiwa kuwa na mkaguzi (manager) wa kuaminika ambaye kwa nyakati tofauti atakuwa anafuatilia nyendo za gari lako na kuhakikisha kuwa madereva wakati wote wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Gari inapoharibika hakikisha unafika wewe mwenyewe/msimamizi wako na kuhakikisha gari linapelekwa kutengenezwa kwenya gereji zinazoaminika.

Hakikisha gari lako umelipa kodi zote kuepuka usumbufu wa kukamatwa na askari na kusababisha upotevu wa mapato. haya ni machache tu ila biashara ya daladala inahitaji usimamizi wa karibu na umakini mkubwa pia hakikisha dereva, fundi na kondakta wako unawapa vivutio na mikataba inayoeleweka ili waifanye kazi yao kwa bidii na uaminifu.
KUFANIKIWA KUNATEGEMEA SANA UBORA WA GARI NA USIMAMIZI

1. Gari ilikuwa Isuzu Journey Long

2. Niliweka hesabu ya chini kwa kulenga kumshawishi dereva atunze gari (70,000/= per day)

3. DSM Gongo la mboto - Temeke (Route fupi sana na bora kwa gari)

4. KUfanikiwa kunategemea sana ubora wa gari na usimamizi. Gari ikiwa imara utakwenda service mpaka service. Maana yake pesa utaiona. Na Kwa utaratibu niliokuwa nautumia, service ilikuwa ikifanyaka kila jumanne ya wiki ya pili. Tatizo ni pale dereva anapoanza tamaa na kupata route za kwenye barabara za vumbi.

Gari litaanza kula hela kwa matengenezo na utaichukia kazi. Pia kama ukianza na gari bovu utaapa kutogusa tena biashara ya daladala. Hao jamaa wengine sijaelewa wanatumia utaratibu upi kuhakikisha dereva habadili route, ila wengi nimegundua wanazingatia sana dereva mwaminifu. Ila kwa anayeendesha mwenyewe (mmiliki), huyo hamna shaka ana asilimia kubwa sana ya kufanikiwa (hata hesabu itakuwa kubwa).

5. Kitu ambacho nitafanya tofauti- gari lazima liwe kamili. Pia dereva lazima awe MZEE WA MAKAMO MWENYE FAMILIA. Yes, niko serious. Vijana wameniua. Watu wazima wanatend kuheshimu kazi zao na kujali familia zao. Vijana wengi wana ujanja ujanja ili ku-maximize profit. Wanajua ukimfukuza wewe atapata ajira sehemu nyingine. Pia kuwa na gereji yako ambapo utakuwa unatengeneza gari lako ni muhimu mno.

Awepo fundi maalum ambaye atakuwa kama personal na close associate, huyu atakutoa sana kwani hata likitokea tatizo kwenye gari wewe utapiga simu tu, naye atakwenda eneo la tukio kuicheki gari. Hii itaondoa ujanja ujanja wa madereva kusingizia magonjwa au kukuficha magonjwa yanayotokana na uzembe wao. Mfanye awe kama rafiki yako wa karibu utashukuru. Dereva akikutaarifu kwamba kuna ugonjwa, unamzuia kutengeneza unamwambia kuna fundi anakuja, wataogopa kiasi fulani. Hii niliifanya mwishoni kabisa, na huyu fundi ndiye akanishauri niiuze gari ninunue nyingine. Pia alinisaidia sana kwa mambo ambayo otherwise madereva wangeniliza.

Nadhani nimefunguka vya kutosha, karibuni kuchangia wakuu.
PATA UZOEFU HUU
Mkuu biashara ya HIACE nzuri ila ubaya unakuja ukiwa una kazi ya ziada na unategemea hiace halafu umempa dereva gari ukitegemea kila siku hataleta pesa kama ulivyopanga HIACE nzuri ya kuagiza mpk kufika mkononi na kufanya kazi ni kati ya mln 25 mpk 30 katika biashara ya daladala ukiwa unaanza zingatia mambo haya hasa kama ya mkopo ili ufikie malengo bila kufeli.

Katika siku 365 za mwaka toa siku 52 kuwa gari haitafanya kazi inamaana katika wiki siku 1 haifanyi kazi(hapa unielewe haimaanishi kila wiki ipumzike ila kuna service(kumbuka service bora ni ya kilomita sio kuhesabu siku)
kuna kuharibika pakubwa gari ikakaa hata siku tatu inatengenezwa kuna kukamatwa ikakaa police na dharura nyingne ) hivyo piga hesabu gari itafanya kazi na kuleta pesa siku 300 tu katika mwaka

Ina maana kwa mkopo wa kuweza kupata HIACE nzuri ili umalize mkopo kwa mwaka 1 rejesho kwa mwenzi ni ni km mln 2.7 ina maana kwa uwiano wa kila siku kwa mahesabu ya juu hapo ni 115000/= ndio maana nikauliza dereva anaweza kuleta laki kwa siku.

HIACE ya DIESEL manual ni nzuri kibiashara ila HIACE ya petlor ni nzuri kwa kudumu ila itakuumiza kwnye mafuta

lkn kumbuka gari kudumu si kukaa miaka mitano au mitatu ni kilomita inazotembea ndo maana nikakwambia kwa hiace ya mkopo usiipelele ruti ya kilomita nyingi itakucost mbele coz utapotaka kuuza isiwe imechoka sana

nyingne kumbuka barbara yoyote ya vumbi inaua gari halaka hivyo kuwa na tagert fupi yaan ukimaliza mkopo gari ifanye kazi muda fulani uuze uongeze pesa ununue mpya

huko kasulu sipajui ila nina uzoefu tu wa barabara nyingi za tanzania zinafanana ni kiwango cha kokoto vishiringi kibao bodi inachezacheza
 
Karibu Alnadaby kwenye shughuli hii ya kusafirisha abiria katika miji mikubwa.Kitu cha kwanza kabisa katika bajeti yako weka 30% ya mapato yako kwa ajili ya mafisadi wa barabarani, hakuna jinsi kubali kugawana mapato na hao jama kwani ndiyo wadau.

Pili fuatilia sana mienendo ya madereva na makonda,maana wengi ni wavuta bangi na hawana akili ya kawaida.

Na kma unashindwa kufanya hivyo nakushauri haraka uza gari tafuta bishara nyingine mkuu.
 
Makalangilo, p

Linapokuja suala la Anti-Corruption, tunaona ni jinsi gani ambavyo mazingira yanatengenezwa kwa anayetaka kufanya biashara ili ajiongezee kipato kuwa ngumu!

Kumbuka mtu huyu analipa malipo yote halali yatakiwayo ili kuendeleza NJI HII lakini wakamuaji wasio rasmi wana 30% yao kutoka ktk biashara hiyo! Hapo hapo wanataka uwaajiri watumishi hawa kwa mishahara minono!
 
Adha na kero hatimaye zimefikia mahali ambapo madereva wa daladala waliamua wao wenyewe kugoma na kuzipanga gari kuanzia hapo Sahara hadi barabara yote ya Pamba Rd ikawa haipitiki kwa msongamano magari zaidi ya mia na ushee, hadi Mkuu wa Mkoa akafika na kuuliza kulikoni!

Kero za rushwa na ufisadi wa trafiki zilimwagwa na wakulu wote wa usalama barabarani wakiwa wanajifaragua maana tatizo la kutokuwa na mahali pa kupakilia abiria lilizaa mradi wa kuwakomoa madereva.

Matokeo Mkuu wa Mkoa alishtuka kwa kutokuwa na habari na tatizo hilo na akaahidi kulitafutia ufumbuzi.

Mradi huu wa kifisadi ulioundwa na Mapolisi wa Trafiki wa Mwanza wa kuwapiga bao madereva kwa kupakia abiria bila kituo (Hakuna vituo)umewanufaisha wana usalama barabarani wengi hapa Mwanza wakiwa wamejijengea majumba kwa hela za kufisadi za kuwapiga bao madereva.

Stendi hiyo ya Sahara sasa imeruhusiwa kwa muda kupakia abiria na hali inaelekea kuwa shwari leo hii.

Nilipoanza biashara hii nilidhani ni biashara kama zingine kumbe ni maradhi makubwa! Sasa natafuta mnunuzi wa Hiace nitafute biashara nyingine.
 
Dont give up the fight ELLY!

Give them for u to survive!

Wape na uje uyaweke hadharani kuwa ushahidi tosha!
 
Ipo shughuli nyingine yoyote ungeweza kufanya tofauti na kubeba abiria ukitumia hiyo Hice? Pengine umewahi kuwa na mawazo ya namna hii, labda ukaona hailipi.

Unaweza kushirikisha wadau hapa? Unaweza kuambulia different ideas usilazimike kuuza Hice.
 

UZOEFU: CHANGAMOTO YA MADEREVA KUTOKUWA WAAMINIFU

Nilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.

Leo dereva anakwambia center-ruber imeisha, kwa hiyo badala ya Tsh 40,000 unapata 15.Kesho asbh ndo kwanza unaingia ofisini anakwambia timing belt imekatika...inatumika pesa ya jana na haitoshi inabidi utoe yako mfukoni.

Siku ya tatu na ya nne akikuhurumia ukakusanya 80 basi siku inayofuata unaambiwa nimepigwa bao na majembe. Ilikuwa nilipe 250,000 so nimewapoza 35,000. so hesabu yako mkuu hii hapa elfu tano! Gosh!!!

Picha hizo zimeendelea mpaka nikatia shaka, akipiga dereva wkt mwingine nachomoka kuthibitisha tatizo. Ajabu! Mara kadhaa ni uongo kunakuwa hakuna cha majembe wala mashoka! Bse of that nimewatimua kila nikigundua usanii huo, ndani ya mwezi 1 madereva wanne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.

Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!
 
Cha muhimu pata dereva qualified usichukue tu hawa wa mtaani ambao ni longolongo tu na wamezidi usanii. Au tafuta tender ya kubeba wanafunzi hela mabayo wazazi wa wanafunzi au shule sijui itakuwa inakulipa wewe and not trhough dereva.

Halafu siku nyingine kama hauko busy sana chukua daladala yako mwenyewe endesha ukiwa na konda kama weekend hivi halafu ucgheki mapato yake yatakuwa kiasi gani. Au weka limit ya kiasi kama ni laki kwa siku iwe laki na kama wamekamwatwa na majembe au traffic au nani wewe ndo udeal nao straight saa zingine si vizuri sana kuwaachia madereva to deal na kila kitu esp wa daladala.
 
Kumiliki daladala inabidi uwe kichaa kidogo.

Ni lazima uwe na akili kama za watu wanaofanya kazi kwenye daladala ndio mtaenda sawa, vinginevyo utakuwa unafanya kazi wa kuwafaidisha dereva na konda wake.
 
JS,

Nimejaribu kuwa nayo over the week end malipo yanakuwa mazuri hasa, wao wanakwambia ni kawaida kuwa na abilia wengi week end na siku za sikukuu (Ambazo ndizo siku mi nipo nyumbani)

Kwa upande wa pili ni vigumu mimi kumalizana na majembe na matrafiki maana nakuwa kazini. Na wao wanatake advantege hiyo!
 
Sumbalawinyo,

Unachosema ni kweli Sumbalawinyo lakini we upo kazini tangu asubuhi mpaka saa kumi na mbili huo muda wa kukomaa nao si ndo inakuwa issue? Ilifika kipindi nikaamua niipaki kabisa lkn bado nikaona si wazo la busara.
 
Pole sana mkuu,

Madereva wa daladala ndiyo tabia yao. pole sana! Tafuta tu dereva mwaminifu!

Ushauri:

Wewe mkabidhi gari. Mwambie hii nakukabidhi wewe. Mpunguzie hesabu mpaka labda 35. Kisha mwambie aihudumie kila kitu, Na wewe hutaki kusikia longolongo lolote. Mwambie akupe hesabu ya wiki nzima!

Hayo mambo ya bao, sijui nini ni juu yake, wewe hayakuhusu!

Hapo lazima uwe na roho ya paka la sivyo utakuwa unafanya biashara ya kuuza ubuyu na visheti kila siku!
 
Pole sana ndugu yangu.

Biashara nyingi ndivyo zilivyo, wafanyakazi wengi wanalazimika kuwa majambazi kwa sababu ya masha magumu na mishahara midogo. wewe mtu unamlipa laki 1.5 au 2 dar au arusha unategemea aishi maisha gani, analazimika kuwa fisadi.

Mambo ni hayohayo hata ukiwa na hoteli au roli. Kikubwa kama umeamua kufanya biashara ni kuchakarika na kuwa kaksi, wakati mwigine unaweka mtu wako kuwa konda au deree.

Ikiwezekana unasuka mwenyewe wakati mwingine. all in all nisingekushauri kufanya biashara ya usafirishaji kuwa biashara ya kwanza (i prefer uzalishaji mali).

Ukipata tenda ya kukodisha itakupunguzia presha.
 
pole sana mkuu,
madereva wa daladala ndiyo tabia yao. Pole sana!
tafuta tu dereva mwaminifu!

ushauri:
Wewe mkabidhi gari. Mwambie hii nakukabidhi wewe. Mpunguzie hesabu mpaka labda 35. Kisha mwambie aihudumie kila kitu, na wewe hutaki kusikia longolongo lolote. Mwambie akupe hesabu ya wiki nzima!

Hayo mambo ya bao, sijui nini ni juu yake, wewe hayakuhusu!

Hapo lazima uwe na roho ya paka la sivyo utakuwa unafanya biashara ya kuuza ubuyu na visheti kila siku!
Dereva mwaminifu atampata wapi?
 
biashara ya daladala ni sawa na kufuga kuku! kama hufugi au huendeshi mwenyewe personally, hesabu umeumia. sasa subiri nyepesinyepesi kuwa dereva wako naye kanunua daladala....................... mjini hapa
Hii nayo ni kiboko aisee! Sasa tutatokaje mjini hapa sie wenye mitaji midogo?
 
Biashara ya daladala kwa mfanyakazi wa ofisini ni ngumu. Anayefaidi ni dereva. Chukua ushauri wa Mkuu mmoja hapo juu wa kutafuta tenda za shule au mahoteli.
 
Biashara ya daladala kwa mfanyakazi wa ofisini ni ngumu. Anayefaidi ni dereva. Chukua ushauri wa Mkuu mmoja hapo juu wa kutafuta tenda za shule au mahoteli.
Natoa shukurani zangu kwa wote waliochangia mawazo. Nakubaliana na ukweli kuwa biashara ya daladala kwetu tunaofanya kazi ni ngumu mno.

Nimeanza kufanyia kazi wazo la kutafuta tenda za shule, so km kuna mwenye link si mbaya akaniunganisha.

Changamoto tuliyonayo ni kufahamishana juu ya ni biashara gani mfanyakazi anaweza kufanya na ni zipi amabazo zitamuweka katika wakati mgu kama mfanyakazi (I.e. zinahitaji very close supervision)

Naendelea kupokea mawazo yenu wakuu.
 
Pole sana ndugu yangu. Watafute wapenda tena mujahidina kabisa ndo anakufaa kwani wewe unawatafuta vibaka tu. Pia nenda kijijini kwenu tafuta kijana aliyetulia mwambie unampaka zi kisha awe konda kama kuna ujinga atakwambia tena unampamasharti utaona matunda.

Ishu ingine wewe usimkabidhi dereva gari mkabidhi konda ndio atafute dereva kwahiyo linakuwa lao sim moja ukiona hivi unapiga chini konda sio dereva waizi ni makonda.
 
Back
Top Bottom