Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake


UZOEFU: CHANGAMOTO YA MADEREVA KUTOKUWA WAAMINIFU
Nilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.

Leo dereva anakwambia center-ruber imeisha, kwa hiyo badala ya Tsh 40,000 unapata 15.Kesho asbh ndo kwanza unaingia ofisini anakwambia timing belt imekatika...inatumika pesa ya jana na haitoshi inabidi utoe yako mfukoni.

Siku ya tatu na ya nne akikuhurumia ukakusanya 80 basi siku inayofuata unaambiwa nimepigwa bao na majembe. Ilikuwa nilipe 250,000 so nimewapoza 35,000. so hesabu yako mkuu hii hapa elfu tano! Gosh!!!

Picha hizo zimeendelea mpaka nikatia shaka, akipiga dereva wkt mwingine nachomoka kuthibitisha tatizo. Ajabu! Mara kadhaa ni uongo kunakuwa hakuna cha majembe wala mashoka! Bse of that nimewatimua kila nikigundua usanii huo, ndani ya mwezi 1 madereva wanne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.

Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!
Vipi uliendelea na hii biashara?
 
Mnahangaika bure njoo garage-ni kwetu tuna madereva mafundi kabisaaa!! yaani ana vyeo viwili ni fundi na ni dereva ila mshahara wake ni mara mbili ya dereva wa kawaida!! gari ikiharibika aje garage kwetu sisi!

atachuku spana atafungua atarekebisha anavyojua yeye!...saweni ndg zangu!....ila service ni kwetu!! akipoteza uaminifu dhamana ni kwetu sisi km mkurugenzi wa garage! tunaweza weka mwingine!
 
Mnahangaika bure njoo garage-ni kwetu tuna madereva mafundi kabisaaa!! yaani ana vyeo viwili ni fundi na ni dereva ila mshahara wake ni mara mbili ya dereva wa kawaida!! gari ikiharibika aje garage kwetu sisi!

atachuku spana atafungua atarekebisha anavyojua yeye!...saweni ndg zangu!....ila service ni kwetu!! akipoteza uaminifu dhamana ni kwetu sisi km mkurugenzi wa garage! tunaweza weka mwingine!
Mnapatikana wapi na gerage yenu inaitwaje?
 
Hii biashara bana ina changamoto zake, ofcourse ni part ya biashara zangu kwa sasa.

Mimi naindesha hivi,
Ninazo 2, Nissan Civilian na Toyota Coaster, ambazo roughly nimezinunua kama kwa 50,000,000/= total

Kwa siku za wiki kila moja inaleta 80,000 x2 x5 = 400,000
Jumamosi ni 70,000 x 2 = 140,000
na Jumapili 60,000 x 2 = 120,000

Jumla 1,060,000 kwa wiki.

Matumizi yapo hivi.
Kila baada ya wiki 2 ni services ambayo gharama zake ni kama ifuatavyo.

Engine Oil Lita 20 = 96,500 (kila gari inakula 10Lita)
Oil Filter inaweza kua hata 36,000
Fundi 20,000

Matumizi ya kila mwezi
Msimamizi wa magari yote mawili 200,000

Hapa kuna matumizi mengine hayapo, yaani assumption ni kua kila kitu kiko poa. Hivyo sijaweka matairi, motor vehicle, TLB, bearing labda, Betrii, repair ya pasi ndogondogo n.k.

Msimamizi huyu ni mjomba wangu, na madereva + makonda katafuta yeye.

Hua napigaga tripu za kustukizia pale yanapolala kuangalia kama ni kweli yanalala saa 3-4 usiku. Maana yanaweza kua yanakesha wakakuulia gari.


Kifupi inanilipa kiasi,
Tafuta msimamizi, mlipe vizuri na jaribu kua nae karibu!!
Na vp kama nikiamua kuendesha mwenyew nikatafuta kondakta tu
 
Original Pastor, hilo la kumweka ndugu kama konda nimelifanya japo sikumtoa kijijini. Kilichotokea ni kuwa mheshimiwa alitafuta dereva kweli lakini hakuishia hapo aliweka na konda pia! Kila wakati yeye yupo chini ya mti akisubiri aletewe hesabu ya kila trip wanayofanya.
Bongo hii kila mtu anataka kuwa bosi ale pesa rahisi tu
 
Hii biz haitabiriki mi nimenunua minibus nissan civilian toka jp nikampa Mzee mmoja niliyemuamini aniingizie mahesabu ya laki moja kwa siku. Kafanya kazi vizuri mwezi mmoja leo kanitumie taarifa eti gari imepata breakdown inahitaji sh milioni mbili kwa sasa niko confused.
Break down is too general kwanini asiseme shida ni nini? Ni break, au gear box au nini hasa?
 
UELEWA WA KINA KUHUSU BIASHARA HII

Sorry wakuu kwa kuwaletea mada ambayo ni ya muda mrefu toka iandikwe but mimi nimeisoma leo na nimejifunza kitu nikaona ngoja niwaleetee wadau ambao hawakupata kuiona nao wajifunze jambo kidogo

Baada ya kununua basi dogo la kwanza (Hiace) na kulisajili kwa biashara ya kusafirisha abiria Mjini (daladala); nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto ziliponizidia niliaazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri. Nikamfuata mzee wangu mmoja hapa Mjini Iringa ambaye ameanza biashara ya kusafirisha mizigo na abiria tangu mwaka 1978.

Mzee wangu huyu baada ya kunisikiliza aliniambia sentensi moja tu na akasema huo ndio ushauri anaonipa na ambao utanisaidia. Alisema hivi, Kijana wangu! Ili umudu biashara ya magari hasa hizi daladala unatakiwa uwe mjeuri-jeuri kwa madereva, makondakta na wakati mwingine kwa matrafiki. Nikataka anipe ufafanuzi kuhusu hili ndipo akaongeza ufafanuzi huu, Hawa watu ninaokwambia usicheke nao ndio ambao wanaweza kukuliza ama kukufanya ufurahi. Ukizubaa katika hili usishangae kujikuta muda umepita, gari limechakaa na faedha za kununulia gari jingine huna.

Ushauri wa mzee wangu huyu niliufanyia kazi na ulizaa matunda (kwangu) Uzoefu wangu katika biashara hii ya daladala unachagizwa pia na nafasi ya uongozi niliyoapata kushika kuanzia mwaka 2009 hadi januari 2012. Nilikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi ya abiria mkoani Iringa kinachojumuisha magari yote ya abiria ukiacha mabasi ya mikoani. Nafasi hii ilinipa kufahamiana na kushirikiana na wafanyabiashara wengi wa magari ya abiria Iringa. Hivyo nafahamu chungu na tamu za biashara ya daladala na machozi yao nayajua.

Ukiacha changamoto ya faida (ambayo nitaichambua kwa kina kwenye makala hii) biashara ya daladala ina timbwili-timbwili si mchezo. Madereva wanasumbua sana, faini za barabarani zisizoisha na uharibifu wa magari ni kama chachandu chungu kwenye biashara hii.

Kati ya biashara nilizowahi kuzifanya biashara ya daladala inaongoza kwa kupasua kichwa Miezi machache iliyopita wamiliki wa daladala-Dar es Salaam waliwasilisha kusudio la kupandisha nauli za daladala kwa asilimia mia tatu (300%) mbele ya baraza la watumiaji wa huduma za usafiri.

Baraza hilo pamoja na SUMATRA waliwagomea wamiliki wa daladala kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu hizo ni pamoja na Mosi; wamiliki wa daladala walishindwa kuwasilisha taarifa za kifedha za biashara zao.(Approved financial statements) Pili sababu walizozitoa kuhusu kupanda gharama walidai (exagrated) zilikuzwa mno na kukosa ushahidi wa bei katika soko. Baada ya kufuatilia mnyukano ule niliwahurumia sana wamiliki wa daladala kwa sababu wenye rungu la kuwasaidia hawajui viatu vya umiliki wa daladala vinavyobana na kuumiza.

Nimetafiti biashara hii katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Dodoma huku Iringa nikiwa nimeifanya kwa vitendo. Sehemu karibu zote changamoto zinafafanana ingawa kuna tofauti ndogo ndogo kutegemea na tamaduni za kimaeneo. Sehemu hizi zote viwango vya fedha inayolazwa ni shilingi kati ya elfu thelethini (30,000) na elfu arobaini (40,000) kwa siku kwa mabasi madogo (Hiace Super Roof). Kwa mabasi ya kati (Coaster) kiwango kwa siku ni kati ya elfu hamsini (50,000) hadi elfu themanini (80,000) kwa siku. Sasa twende kimizania ya uhasibu hapa.

Bei ya kununua basi dogo (Toyota Hiace Super Roof) pamoja na kusajili leseni, njia, na taratibu zote ili ianze biashara ni kati ya shilingi milioni ishirini hadi milioni ishirini na tano (20M-25M). Bei ya kununua basi la kati (Coaster) ni kati ya milioni thelathini na tano hadi milioni arobaini na tano (35-45). Magari hayo yote ni yale yaliyotumika kule Japan (Used Cars) Tukokotoe mahesabu ya basi dogo.

Kwa upande wa mapato kama gari inalaza shilingi elfu 30 kwa siku ina maana kwa mwezi unakusanya shilingi 840,000 (laki nane na arobaini elfu). Hesabu hizi ni kwa siku ishirini na nane. Siku mbili kikawaida hutengwa kwa ajili ya kufanya service ya gari ambayo ina fanyika kwa mwezi mara mbili kila baada ya siku 14.

Tushuke kwenye matumizi. Galoni moja la kilainishi kizuri(oil) ni shilingi elfu 45, gharama ya kubadilisha sahani za breki ni shilingi 25, vifaa ambatanishi vya service ni karibu shilingi 20. Ukichanganya na ufundi na ikiwa unafanya service ya uhakika katika gari lako kila service moja unatumia shilingi laki moja kwa kadirio la chini.

Katika kipengele cha service kwa mwezi unatumia kama laki mbili. Mshahara wa dereva kwa mujibu wa sheria za SUMATRA zinazoambatana na masharti ya kupewa leseni yanakutaka mmiliki wa gari ulipe kuanzia kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi shilingi elfu themanini. Kodi za serikali ikiwemo leseni ya barabara, leseni ya njia, zima moto, mapato na ushuru wa manispaa/jiji ni wastani wa shilingi elfu sitini kadirio la chini.


Nyingi ya kodi hizi zinalipwa kwa mwaka lakini hapa nimezigawanya katika mafungu ya miezi 12. Mwisho tujumlishe mshahara wa wewe Mjasiriamali unayemiliki gari. Najua wajasiriamali wengi hawana utaratibu wa kutenga mishahara yao kwa biashara zao, lakini hata kama hutengi mshahara tukadirie kuwa unajilipa shilingi elfu themanini tu kwa mwezi.

Sasa ukichukua mishahara ukajumlisha na kodi ukajumlisha na gaharama za matengenezo (service) unapata matumizi ya shilingi laki nne na ishirini elfu (420,000). Kiharaka haraka unaweza ukadhani faida inayobaki ni shilingi laki nne na ishirini (420,000).

Hapa ndipo wafanyabiashara wengi wa magari ambapo hufilisikia kwa kusahau jambo la muhimu kuliko yote. Jambo hili la muhimu ni gharama ya uchakavu wa gari (depreciation cost). Gharama hii kitaalamu hutakiwa kujumuishwa kwenye kipengele cha matumizi.

Tunaposema gharama ya uchakavu ni pale unapoelewa kuwa ikiwa gari inatembea basi tairi zinazidi kuisha, vyuma vinasagika na bodi linachakaa. Kinachoamua kiwango cha gharama ya uchakavu ni makadirio ya muda ambao gari lako litakaa kabla ya kuchakaa kabisa. Kuna njia kadhaa za kitaalamu lakini hapa nataka nitumie njia rahisi ya kijasiriamali ili tuelewe vema.

Mathalani kama gari yako inapita kwenye barabara nzuri unaweza kukadiria kuwa uhai wa gari lako utakuwa ni miaka mitano. Unachofanya unachukua thamani ya kununulia hadi kusajili gari ianze biashara kisha unagawanya kwa miaka mitano. Twende pole pole hapa.

Tumesema wastani wa chini wa basi dogo ni shilingi milioni 20 hadi ianze biashara. Ukichukua milioni 20 ukagawanya kwa miaka mitano unapata shilingi milionI 4 ambayo ndio gharama ya uchakavu kwa mwaka. Sasa chukua milioni hii 4 kisha gawanya kwa miezi kumi na mbili unapata wastani wa shilingi 333,000 (laki tatu na thelathini na tatu elfu). Hii fedha tunaiingiza kwenye sehemu ya matumizi.

Kwa maana hiyo jumla kuu ya matumizi yetu kwa mwezi inakuwa ni shilingi 753,000/=(laki saba na hamsini na tatu elfu). Ili uelewe faida HALISI unayozalisha kwa mwezi chukua mapato ya mwezi (840,000) kisha utoe na matumizi ya mwezi (753,000). Ukikokotoa hapo utaona faida HALISI ya biashara ya daladala ikiwa una basi dogo kwa mwezi ni shilingi elfu themanini na saba (87,000/=) tu! Najua mahesabu haya yatawastua wengi na wengi wanaweza wasiyaelewe na kwa kutoyaelewa wanaweza wasiyakubali. Bahati nzuri ni kuwa nimeshafanya biashara hii huku nikiwa na digrii ya biashara kutoka chuo kikuu hivyo naelewa ninachokisema hapa. Labda nitafsiri maana ya mahesabu hayo hapo juu kwa lugha nyepesi na ya picha.

Iko hivi; ukinunua gari la milioni 20 leo, baada ya miaka 5 linaweza kuwa limeshachakaa kabisa. Wakati huo gari litakapochakaa unatakiwa uwe na fedha mkononi za kununua gari jingine kutoka katika biashara hiyo hiyo na ubakiwe na fedha nyingine ambayo ndiyo tutaiita FAIDA. Ile hela utakayorudishia gari lililochakaa ni mtaji ulioanza nao. Kwa mahesabu hayo hapo juu ambapo tumeona faida HALISI ya daladala ikiwa unamiliki Hiace Super Roof ni shilingi elfu themanini na saba kwa mwezi.

Kwa faida hiyo (@87,000/=) itakuchukua Mjasiriamali miaka 19 ili afanikiwe kununua gari jingine la pili! Mliowahi kufanya biashara ya daladala mtakubaliana nami kuwa; ukiona mtu ameongeza daladala ya pili ndani ya mwaka mmoja ama miwili basi uwe na uhakika kuwa fedha ya kununulia gari ya pili hajaitoa kwenye gari ya kwanza kwa asilimia mia moja.

Ni ama amechukua mkopo au fedha ameongezea kutoka vyanzo vingine. Naomba nieleweke vema hapa. Sisemi kuwa biashara ya daladala hailipi, la hasha! Lakini faida HALISI iliyopo kwenye daladala ipo tofauti sana na vile SUMATRA na abiria wanavyoitazama ama kuifikiria.

Mtazamo na mawazo ya wadau hawa ndio yamekuwa yakisababisha kuwakatalia wenye daladala ama kuwakubalia kwa mbinde kila wanapotaka kuidhinishiwa kupanda kwa nauli. Mathalani, kilainishi (oil) ambacho mwaka 2006 kilikuwa kikiuzwa shilingi 19,000/= leo kinauzwa 45,000/=. Tairi ambalo wakati huo liliuzwa kwa shilingi 85,000/= leo linauzwa 165,000/=. Gari lililokuwa linauzwa milioni 12M mwaka 2006 leo linauzwa milioni 22M (Toyota Hiace Super Roof).

Kwa mabadiliko hayo nauli za daladala zilitakiwa zipande kwa asilimia 236% kutoka mwaka 2006 hadi leo. Lakini hali ni kinyume, kwani maeneo mengi nauli ya daladala imeongezeka kwa kati ya shilingi 50 hadi 100 ongezeko la kati ya asilimia 25% hadi 50% tu.

Ndio maana SUMATRA na baraza la watumiaji walipowagaragaza wamiliki wa daladala kwa kufutilia mbali madai yao ya kupandisha nauli, nilijichekea na kusikitika tu. Hata hivyo sina neno na wala sina lawama kwa SUMATRA wala baraza la watumiaji; kwa sababu wenye daladala wenyewe walishindwa kujitetea utetezi wenye nguvu za hoja.

S
ource: suleimanmagoma.blogspot.com
Hii comment ya moto
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Back
Top Bottom