Ukistaajabu ya Musa....watoto wasio na baba

Ukistaajabu ya Musa....watoto wasio na baba

Mpitagwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2012
Posts
2,338
Reaction score
1,127
WanaJF, leo nimeonana na dada mmoja tuliyesoma nae chuo kimoja. Wakati wa chuo dada alikuwa na rafiki yake wa kiume lakini kama yalivyo mapenzi mengi ya vyuoni na la kwake liliisha baada ya kumaliza chuo. sijaonana nae yapata miaka mitano. Leo naonana naye tukasalimiana vizuri na kama ilivyo desturi ya kiiafrika tukaanzia kujuliana hali za familia zetu.
Amenishangaza kwa kuniambia kuwa kwasasa anawatoto wawili, nikamuuliza baba yao hajambo, akasema baba yao ni Yesu. Nikawa simwelewi, tumeongea ongea baadaye akaniambi, alifunga na kuomba mungu wake alimruhusu kwenda kununua hospital kwa kuchomwa sindano za kupewa uja uzito. Na amesema watoto wake wanaendelea vizuri.

Na amesema yeye hataki mahusiano na mwanaume yeyote yule zaidi ya yesu. Nimekuwa mdogo kama piriton nimeshindwa hata kuendelea kuongelea hilo nikabadili topic.

Wanajf hili mnalionaje? Na kwa wale wenye imani, dini zenu zinasemaje juu ya hili?
 
Unachoshangaa ni nini?

Kwamba mwanamke hawezi kufanya IVF na kupata watoto bila mwanamme?

Au kwamba mwanamke wa Kitanzania kakwambia kwamba kafanya hivyo?

Je unaamini kwamba Yesu alizaliwa kwa "immaculate conception"?
 
hakuna mtoto asiye na baba.... Sperm donor ndo baba wa hzo watoto.... Anyway unashangaa nini? Dada wa qatu kaona nyie wanaume nk vichomi kaamua kufanya IVF....ndo mjue soko lenu linashuka thamani ka shilingi ya tanzania
 
Kwanini awaite watoto wa Yesu...maana hakuzaa bana wala hakuweka sperms zake hospitalini. Asihusishe maamuzi yake kwa kupitia yesu
 
hakuna mtoto asiye na baba.... Sperm donor ndo baba wa hzo watoto.... Anyway unashangaa nini? Dada wa qatu kaona nyie wanaume nk vichomi kaamua kufanya IVF....ndo mjue soko lenu linashuka thamani ka shilingi ya tanzania

ah wapi...utamu wa duahelele upo pale pale so thamani yetu ipo bwana haishuki
 
haswaaaaa maana wanazingua sana

Ukisema "wa nini"? wenzio wanasema "ntampata lini"?.

Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.

Same sex marriage zinakuja pia kama wanawazingua zaidi, options zitajaa kedekede, si lazima kendekende.
 
Kwa kumsaidia huyo rafiki yako ungempeleka hospitali akapimwe akili.
Akikubishia mwambie umetumwa na Yesu.
 
Mwokozi kabambikiwa watoto au, au alidoneti baada ya makubaliano kupitia maombi mazito?!
 
hakuna mtoto asiye na baba.... Sperm donor ndo baba wa hzo watoto.... Anyway unashangaa nini? Dada wa qatu kaona nyie wanaume nk vichomi kaamua kufanya IVF....ndo mjue soko lenu linashuka thamani ka shilingi ya tanzania

There is no substitute to that...tatizo these days serikali inaruhusu tunaishi na VICHAA huku mitaani ni hatari sana....
 
Mmh! Naona watu wamechoka kumsingizia SHETANI now wamemuingilia YESU... Sasa kabaki MUNGU tu kusingiziwa.
Hiyo njia aliyotumia kupata watoto haingiliani kabisa na masuala ya imani za kidini, iweje ambambikizie huyu mwokozi watoto?
 
hakuna mtoto asiye na baba.... Sperm donor ndo baba wa hzo watoto.... Anyway unashangaa nini? Dada wa qatu kaona nyie wanaume nk vichomi kaamua kufanya IVF....ndo mjue soko lenu linashuka thamani ka shilingi ya tanzania
Hapo natofautiana na wewe bibie......
 
Back
Top Bottom