Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Mkwamo wa Tanzania tangu kuanzishwa kwake umetokana na sababu kuu mbili.
1. Kuwapa kipaumbele zaidi wajinga na ujinga kuliko akili na wenye akili.
2. Rushwa na Ubinafsi.
Kuhusu kuwapa kipaumbele wajinga na ujinga kuliko akili na wenye akili.
Kabla ya kifo chake. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mzee Mark Bomani alikuwa rafiki yangu sana. Mara nyingi nikitoka kwenye kazi zangu mitaa ya kisutu, Posta nilikuwa napitia zilipokuwepo Ofisi zake, nakaa nae na ananielezea mengi sana kuhusu historia ya Taifa letu.
Mark Bomani aliyepata kuwa DPP na baadae Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria wakati wa Nyerere alinihadithia kisa cha ugomvi wa Nyerere na Oscar Kambona vizuri sana.
Kwa mujibu wa Marehemu Mark Bomani, Kambona alitofautiana na Nyerere kuhusu namna ya kutekeleza sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Kwa mawazo yake aliona sio sawa kuwanyang'anya watu mali zao kama mashamba, matrekta, nyumba na kuwalazimisha kwenda kuishi vijiji vya ujamaa kulipokuwa hakuna chochote. Kambona aliona ile kama dalili ya kwanza ya udikteta na kijiua kiuchumi ( Economical suicide).
Kwa mawazo ya Kambona hatua ile ilikuwa ni kuharibu uchumi wa Taifa uliokuwa unaendelea vizuri sana ikumbukwe kabla ya sera ya Ujamaa na Kujitegemea Tanganyika na baadae Tanzania ilikuwa na uzalishaji mkubwa sana wa chakula uliokuwa ukifanywa na Wazawa pamoja na wakulima wachache wa kigeni. Wakulima hawa walikuwa wanazalisha chakula kwa wingi sana mikoa ya Mbeya, Iringa, Tanga, Morogoro, Lindi, Kilimanjaro, Arusha, Mara, Mwanza na Dodoma. Mawazo ya Kambona ilikuwa akili kubwa.
Kambona hakukubaliana na kuwanyang'anya watu uwezo wao na nguvu kazi zao. Matokeo yake alikuja kutangazwa kuwa Mhaini ila ukweli ulibaki palepale kuwa Sera ya Ujamaa na Kujitegemea hasa vijiji vya Ujamaa ilikuja kuzalisha umaskini wa kutisha kwa Watanzania hadi kuleta mabalaa ya Njaa hadi kusababisha kuletewa vyakula vya msaada.
Sio hivyo tu Sera hii ilikuja kusababisha kuanguka kwa uchumi wa nchi hadi kupelekea wananchi kuvaa nguo zenye viraka.
Kwa upande wa Mzee Warioba huyu uzuri historia yake wengi tunaifahamu.
Inasemwa tangu alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa na misimamo thabiti yenye akili na wakati mwingi aliweza kutofautiana hadi na Waziri Mkuu Edward Sokoine na kutishia kujiuzuru. Siku zote amekuwa mtetezi mkubwa wa mifumo imara, utawala wa sheria na haki.
Kwenye moja ya visa vinavyosemwa sana inasemwa Sokoine kwenye kutekeleza Sera ya Uhujumu Uchumi alilazimisha kutungwa kwa Sheria zinazolazimisha watu kuadhibiwa nje ya utaratibu wa Kimahakama na Warioba alipingana nae waziwazi kuwa hatuwezi kutunga Sheria ya namna hiyo. Suala hili lilifanya Warioba atake kujiuzuru hadi Nyerere akaingilia kati na kusema vifungu hivyo visiwekwe kwenye Sheria.
Sio hivyo tu. Inasemwa akiwa Waziri Mkuu alipingana na Rais Mwinyi mara kadhaa wakati Mwinyi alipotaka kufanya mambo kinyume na utaratibu wa Kisheria hadi kumlazimisha Mwinyi kuvunja Baraza la Mawaziri na Warioba akaishia kutupwa nje ya Baraza la Mawaziri.
Akiwa Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Warioba aliongoza mchakato wa Katiba Mpya iliyopendekezwa kupunguza madaraka ya Rais na kutengeneza mifumo imara kwa uimara wa Taifa.
Ukiangalia kwa umakini namna Kambona na Warioba walivyotendewa na Serikali ya CCM kusema kweli lazima utaelewa tu kuwa kansa kuu inayoliangamiza Taifa letu ni namna Serikali ya CCM wasivyopenda watu wenye akili na matumizi sahihi ya akili kwa maendeleo ya binadamu hasa Watanzania.
Kote duniani, Mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea vizuri ni yale yanayojali matumizi sahihi ya akili kwa maendeleo ya binadamu. Akili ni pamoja na kusema ukweli, kushauri ukweli na kuupa ukweli huo kipaumbele katika kutatua matatizo yanayokukabili.
Kutopenda matumizi sahihi ya akili ndipo kumekuja kusababisha kutokuwepo kwa mifumo imara ya kuliendesha Taifa letu na hatimaye Rushwa imekuja kushamiri na kuliimarisha zaidi kundi la Watu wachache wanaoishi kwa kutumia vibaya kodi na rasilimali zetu huku wakitukandamiza kwa nguvu kwa mtutu wa bunduki.