Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,280
Swaiba alipata kiwanja Kigamboni, enzi zile bado mapori mengi. Kwa kifupi aliuziwa shamba la ekari mbili. Kwakua haishi Tanzania aliamua kujenga ili asipoteze kiwanja. Alijenga nyumba yake nzuri na swimming pool. Kwakua kiwanja ni kikubwa alijenga na guest wing ya vyumba vitatu yenye master’s bedroom.
Alizingusha uzio na kuweka gate. Furniture ya ndani na kila kitu nyumba ilikamilika. Alimuweka binamu yake kule kwenye guest wingi na nyumba yake alifunga ila mara moja kwa mwezi kuna mtu anafanya usafi, anafungua madirisha asubuhi na kuyaacha wazi mpaka jioni ili hewa iingie.
Binamu alipokabidhiwa nyumba alikua bwana mdogo ndiyo amemaliza chuo. Alitafuta kazi mpaka anaoa yuko katika nyumba ile. Halipi chochote zaidi ya kulipaia umeme, na gas anayotumia maji jamaa alichimba kisima wakati anajenga.
Katika mazungumzo siku moja aliniambia, mtoto wa binamu yake ambae amezaliwa pale amemaliza form six, kama utani alisema hawa watoto watajua nyumba ile ni ya kwao maana maisha yao yote wameishi pale. Tulicheka lakini swaiba alidhamiria. Alimpa notice binamu.
Hata hivyo alipata shirika linataka nyumba zote mbili kwa wafanya kazi wao. Tangu ametoa notice sasa amekua adui wa familia, shangazi yake ambae ni mama wa binamu analalamika wanaua undugu atamtoaje ndugu yake kwenye nyumba ilhali hata yeye akienda Dar kwa matibabu anafikia hapo.
Shangazi haoni kabisa kuwa kwa miaka zaidi ya 15 mtoto wake alipaswa kuwa na nyumba hata kama alipenda kukaa pale basi yake angepangisha. Binamu alipaswa ajiongeze kimaisha.