1. Siku ya ibada, Sabato.
Hili wengi wanaliona kama fundisho kuu. Kutokana ndio utambulisho wa kanisa. Sio ajabu kanisa linaitwa SDA yaani seventh day Adventist church yaani kanisa la Sabato la marejeo ya kristo.
2. Marejeo ya kristo (kurudi mara ya pili kwa Yesu)
Hili ni fundisho la pili. Na linalotiliwa mkazo.
3. Amri za Mungu.
Hapa zipo Amri nyingi sana ambazo wasabato wanazihubiri. Lakini inayojitokeza mara kwa mara ni amri ya nne. Kuheshimu na kuitunza Sabato.
Amri hii inapohubiriwa ndipo unaona Wanaotunza jumapili wakitajwa kwani lazima watu wafundishwe Sabato ya kweli ni ipi katika zile siku saba za juma.
Amri zingine ni kama amri za vyakula, hapo ndipo Nguruwe anapopata umaarufu.
4. Ubatizo wa Maji mengi.
Hapo pia lazima Wakatoliki watajwe kwa sababu wanatofautiana na wasabato. Na wapo kinyume na Biblia.
5. Fundisho la utatu.
Hili linawaunganisha Wakristo wengi. Wasabato na Wakatoliki hapa wanakuwa kitu kimoja.
Ingawaje mimi Mtibeli naliona kama fundisho la kikafiri(kipagani)
6. Fundisho la Maisha baada ya kifo.
Wasabato hapa wanapishana na Wakatoliki. Wasabato wanafuata fundisho la biblia kwamba mtu akifa amekufa anarudi udongoni.
Wakatoliki wao wanaamini kuzimu maisha yanaendelea huku kukiwa na adhabu kwa watakatifu ili kuwatakasa.
7. Fundisho la ndoa, na Kaya na familia.
Hili pia ni fundisho kuu ambalo utalisikia kwa wasabato.
Hapa msingi mkuu wa maisha ya kiroho unaanzia kwenye familia.
Wasabato wanaamini kwenye Mke, mume mmoja. Wanaungana na Wakatoliki
8. Fundisho la uwakili.
Hili ni fundisho kubwa lililosheheni mambo mengi. Hapa utafundishwa kwamba sisi wote ni mawakili wa Mungu. Tunamwakilisha kwa kila kitu alichotupa kama Baraka.
Wakili wa muda, wakili wa mali na kipato, wakili wa kila jambo.
Na mafundisho mengine