Inaweza kuwa sawa lkn umeiangalia in negative way peke yake,kwa nini nasema hivyo kwanza sababu walizotoa ni za msingi,hivi wewe unafurahia mambo yanayoendelea Zanzibar ? Pili wewe unaona ni sawa kwa hizi sheria za cyber crime? Tuache unafki mkuua, misaaada ya masharti sisi hatuitaki.Leo wanakupa sharyi la zbar, kesho watakwambia habari za ndoa ya jinsia moja.
Ni toka kwenye nukuu ya Mwl nyerere aliposema kuwa siku akiona wazungu wanampenda(hasa wamarekani) atajua kuna mahala kaanza kukosea...........sasa kwa hili la misaada kuzuia eti kisa zanzibar.....na kukaa kimya kwa marekani bila kutoa pongezi kwa magufuli jinsi alivyoanza ingawa benki ya dunia imepongeza na kutoa pesa kwa ajili ya mirad mbalimbali...........mabepari wameuchuna sababu wanaona zile enzi za kijamaa zinarud...zile enzi za rais kuwapenda wa tz kwa dhat kabisa, enzi za kushughurika na mambo ya wanachi bila kujipendekeza kwa wazungu.....enzi ya tanzania kuwa nchi yenye heshima........enzi ya tanzania kuanza kurudi kule ambapo wamarekani walikuwa wanakuogopa miaka yote.........kamwe marekani haijawahi wala haitawahi kuitakia mema nchinyingine....hasa afrika....zaidi ya kujali interest zake.........kwa historia ya tz tangu mwanzo na haya ya magufuli kwa sasa.....ni dhahili kuwa wamarekani wana hof ns tz ijayo na wenye akili hawashangai kwa lililotokea na tujiandae kwa mengine menhi zaid......hii ni vita ya ki itikadi sababu zingine ni mbwembwe tu!............Tusiogope dunia kwa sasa imebadilika sana...hao wamarekani hawana chao kwa sasa na kamwe hawatafanikiwa katika hii vita na tz.....magufuli upo sahihi na kamwe usirudi nyuma......"mbele kwa mbele"
Waafrika hatufikiri sawa sawa.
Hapo Wamarekani wana kosa gani?
Wameona mbali sana.
Angalia Burundi wanavyouana utasema ni Marekani au ni upuuzi tu wa kikundi cha watu kung'ang'ania atawale kiongozi kwa maslahi binafsi.
Wenzetu tukubali tu kuwa wana mipango mizuri kwa ajili ya mataifa yao na wanaisimamia.
Hivi kuna faida gani ya kukosa pesa za mcc kwa sababu tu ya kumng'ang'ania Shein ndio awe rais?
Hivi watanzania wa kawaida wanafaidika nini Shein akiwa rais wakati hawana maji,umeme,madawa na elimu bora?
Ni kwa nini tukubali ujinga wa Jecha usio na manufaa kwa maendeleo ya watanzania hasa wa bara halafu tujifanye kuiona misimamo ya marekani yenye faida kwa maendeleo yetu wenyewe kuwa ni kuingilia mambo yetu?
Hivi waliomtuma Jecha kufanya utumbo alioufanya wanatoa fedha kiasi gani kutoka mifukoni mwao kusaidia maendeleo ya nchi mbali na kumtumia Sheini
na nembo ya ccm kutumbu mijihela wanapokua madarakani?
Kama sio matumizi mabaya ya akili hebu tujiulize kwa nini Maalim Seif ambaye ni Mzanzibar asitangazwe na kuwa rais na Dr. Shein ambaye pia ni mzanzibar akawa Makamu wa Kwanza wa Rais kama wananchi wengi walivyoamua kwenye sanduku la kura kisha tukasonga mbele na pesa za mcc tukachukua na kujenga taifa?Badala yake tunaingia gharama ya kurudia uchaguzi utakao kuwa kiini nacho kwani ni dhahiri kuwa lengo la CCM kuifuta serikali ya umoja wa kitaifa litatimia kwani CUF hawatashiriki hivyo ccm kushinda kwa 100%.
Je,sisi watanzania hatuoni kitakachotokea Zanzibar baada ya kumrudisha Shein kwa ushindi wa 100% wakati alikua ameshindwa kwa uchaguzi huru uliofanyika kwa gharama kubwa?
Hatuoni hasara ya uchumi kudorora kwa miaka mitano ijayo na Waislam na wananchi wa kawaida wa Zanzibar kuishi maisha ya hofu na uhasama huku serikali ikiingia gharama kubwa za kupeleka majeshi kule Zanzibar badala ya kununua dawa hospitalini?
Wakati mamilioni ya watanzania wakiendelea kutaabika Jecha atakua anapongezwa na kusifiwa na wale waliomtuma. Eti huu ndio ujanja wa wa Kumshauri Magufuli asimsikilize Obama. Hawa wanaopinga tamko la Marekani hawana nia njema kwa maendeleo ya watu wa chini?
Wazanzibar walishaamua kumchagua Seif ili awavushe walipo, Shein wamemkataa kwani haendani na Kasi ya Magufuli.