Mtu huyo Lazima atakuwa na tabia za Kichadema, Tabia za kutaka Taifa liharibikiwe tu, kutaka Serikali iliyoko madarakani iharibikiwe, kutaka CCM iharibikiwe, Mijitu hii ni Rahisi mno kuijua. Kwa kupitia comments mitandaoni
Tutamtetea CAG na mtu yeyote hata angekua ni Msemaji wa Chama kama Polepole endapo tu anapotetea Fedha za umma zinazotumika pia kuwalipa Mishahara Wazalendo halisi Wafuatao ambao hawana Vyama na hawaruhusiwi Kikatiba kuwa na vyama :-
(1)Majaji wasio na vyama ambao wasikiliza kesi za watu wa vyama vyote bila kujali vyama vyao.
(2)Wanajeshi wetu wapendwa (JWTZ) wasio na vyama wanaotujengea mpaka Ukuta na nyumba za umma na kulinda mipaka ya nchi sio mipaka wala mapaka ya vyama.
(3) Polisi Wetu wasio na vyama wanaotulinda usiku na mchana tunafurahi na kutembea vifua mbele na kufanya mambo yetu kwa amani.
(4) Askari wetu wa Magereza wasio na vyama ambao wanawalinda hata watuhumiwa na wafungwa wote bila kujali vyama vyao.
(5)Askari wa Uhamiaji wasio na vyama na ambao wanafuatilia kwa karibu wahamiaji na wale wanaoingia kiholela nchini kwetu bila vibali.
(6) Askari wetu wa Zima Moto na uokoaji wanaojitolea kuingia kwenye Moto na kwenye majanga ya mafuriko na maji n.k kusaidia kunusuru watu wasipate madhara makubwa au majengo yasiteketee kwa moto.
..Pia Tutamtetea na kumpigania CAG wetu Mpendwa sana Mchamungu na Mwenzetu ,Raia Mwema na Mzalendo wa kweli ,Mwadilifu, asiyejali maslahi yake binafsi ,aliyejitolea kwa vitendo Konyesha mianya ya Mafisadi na majizi ya kula fedha za umma bila huruma ndani ya Vyama vya siasa , bunge na serikali , muumini mwenye kumuhofu Mungu na kuamini kuwa kuna Siku ya Kiama ambapo ataulizwa juu ya aliyoyafanya kwa ajili kunusuru pesa za umma na sio kushirikiana na wanaozimaliza kama wanavyofanya CCM na Chadema, ambao Bungeni CCM inamtumia Spika na wabunge wake kumlazimisha Mh. Rais aingie kwenye mtego wa kumfukuza Mwana wa Wanyonge wa Tanzania Bara na Visiwani na dunia kwa ujumla wakati nje ya Bunge Chadema wanamwandama baada ya kuwaumbua kuwa Chama kimegeuka kuwa Kikoba cha kukopeshana Magari ,sio Mwingine ni CAG ,Alhaj Prof. Assad.
Mungu ampe Uzima na Maisha Marefu ili aishuhudie Tanzania mpya yenye Wapinga wizi wa fedha za umma bila kujali vyama.
Tunapenda CAG huyu muadilifu kama tunavyopenda Pesa halali.
Wale walioshiba na kuvimbiwa Pesa haramu hawaoni umuhimu wa kuwa na CAG muadilifu .
Tutamlinda CAG wetu muadilifu kama tunavyolinda pesa zetu halali.
Tutampigania CAG wetu kama tunavyopigania Pesa zetu za vipato vyetu halali zinapojaribu kuporwa na vibaka.
Tumechoka kuitwa Dhaifu kutokana na umaskini wetu wakati wenzetu wakijiona wenye nguvu kutokana na mapesa ya wizi na ufisadi.
KIBWAGIZO:
CAG sema , sema usiogope sema , sisi Wazalendo wa kweli, hatuogopi Mafisadi Sema x 2.