Ni wakati wa kuyashitaki makampuni manne ya simu

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,027
Reaction score
20,413
NI WAKATI WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Niwakati Sasa wakuyashitaki Makampuni ya simu Tigo, Airtel, Vodacom na Halotel. Kwa mujibu ya Sheria Namba 12/2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mashtaka ya aina hii yanatakiwa kuaandikiwa makampuni hayo taarifa kuyataka yarekebishe ndani ya siku 30 ninachokilalamikia.

Nitaomba mambo sita nikifungua kesi hii.

JAMBO LA KWANZA,
Vifurushi vyote havipaswi kuexpire. Kitu pekee ambacho kinapaswa kumaliza kifurushi inatakiwa iwe ni wewe kuongea hadi dakika zako zikaisha.

Si haki kukata kifurushi cha mtu ambaye dakika zake za kuongea,za data, au sms bado zipo kwa kigezo cha kuexpire au muda wake wa wiki, masaa12, nk kuisha. Lazima kitu hiki kiondoke.

Mathalan, umejiunga kifurushi cha 1000 na umepewa dakika 10 ndani ya masaa 12. Umetumia dakika 3 tu ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 300, na masaa 12 yameisha. Maana yake kwenye 1000 yako zilibaki dakika 7 ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 700, ambazo hizo sasa shilingi 700 kampuni ya simu inajirudishia kwa kigezo cha muda kuexpire. Nachelea kuiita huu wizi lakini initoshe kusema hii haiwezi kuwa haki na haikubaliki.

Lakini pia ninapolipa 500 na wewe ukaniuzia kifurushi si nimekulipa hela yako yote na wewe hunidai. Sasa kwanini tena unachukua kilekile nilichonunua kwako na hela yako yote nimeshakulipa.

Ni hivi,unaponunua kifurushi ni sawa na umenunua bidhaa, na ukishanunua bidhaa hakuna mtu mwingine yeyote, akiwemo aliyekuuzia bidhaa hiyo, mwenye haki ya kuichukua tena bidhaa hiyo yote au sehemu yake isipokuwa wewe uitumie mpaka iishe.

Tizama Tanesco na LUKU. Tanesco ikishakuuzia umeme/units ukamlipa basi hatma ya units zako ni utumie mpaka umalize.Hawezi kuikata na kujirudishia kwasababu anajua alikuuzia bidhaa na wewe ukamlipa na hivyo una haki ya kutumia bidhaa yako mpaka umalize. Hii ndiyo HAKI.

Kinachofanywa na makampuni ya simu ni sawa ununue soda dukani na mwenye duka umlipe hela yake yote. Halafu mwenye duka huyohuyo akwambie kwamba usipoinywa soda yote kufikia jioni au ndani wiki au mwezi nitakuja tena kuichukua nyumbani kwako, na aje kweli aichukue iwe mali yake tena kwa mara ya pili.

Zaidi ya hayo,ukweli halisi ni kuwa kifurushi kwa muundo wake si bidhaa inayoexpire. Ukinunua soda ikiexpire utauona, utaona kabisa kwa macho kadhalika bidhaa nyingine zenye sifa ya kuexpire. Lakini kifurushi kwa uhalisi wake si bidhaa inayoexpire au yenye sifa ya kuexpire.

Hili neno kuexpire limetengezwa ili kuficha neno kupora au uporaji. Ukweli ni kwamba kifurushi kinaporwa makusudi kwa kigezo hovyo kabisa na dhahania cha kuexpire, sijui masaa yako 12, sijui wiki yako, sijui mwezi wako umeisha nk. Kifurushi kinaishaje kabla dakika zangu nilizolipia kwa ukamilifu sijazitumia zikaisha?

Yapo haya nayo lazima yaeleweke, mtu amejiunga lakini yuko safarini hawezi kutumia mda wake , mwingine alipo hakuna network, mwingine hajatumia mda wake alikuwa bize na kazi zake, mwingine simu haikuwa na chaji siku nzima, mwingine umeme ulikatika alikosa mawasiliano nk nk, hawa wote pesa zao walizolipia na hawajazitumia au wametumia kidogo zinakatwa na makampuni ya simu yanajirudishia pesa hizo bila kujali.

Ninataka nifunguwe kesi kuondoa unyonyaji huu .Hatuwezi kuendelea kuwa viwanda vya kutengeneza ukwasi wa makampuni ya simu.

JAMBO LA PILI
Haki ya kutochanganyiwa kifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ridhaa.

Nitatoa mfano, unakuta mtu ameweka shilingi 1000 kwenye simu ambapo anajiunga 500 na 500 inabaki kama muda wa maongezi wa kawaida. Wakati anapokuwa akizungumza au akitumia data kupitia ule muda aliojiunga na ukaisha basi simu haikatiki bali inaunganisha moja kwa moja na ile 500 ya muda wa maongezi wa kawaida ambayo alikuwa hajajiunga.

Hii si sawa hata kidogo na ni vitu ambavyo vinatengenezwa maksudi ili kujipatia fedha bila kujali mtumiaji anaumia kiasi gani. Ni hivi, mtu anapoamua kujiunga 500 na akabakisha 500 bila kuiunga ana maana yake kubwa tu.Hakushindwa kuunganisha 1000 yote.Amechagua 500 kwa maksudi maalum. Sasa iweje unamlazimisha kutumia akiba yake ya 500 hata bila ridhaa yake.

Inatakiwa kuwe na chaguo (option) iwapo mtu anahitaji huduma ya aina hiyo au hapana. Au inatakiwa muda wa kifurushi ukiisha simu ikate halafu kama anataka kuendelea kutumia muda wa kawaida achague mwenyewe kuendelea kuutumia na sio kampuni ya simu kumchagulia.

Au kama anataka kujiunga na hiyo 500 iliyobaki basi ajiunge. Isiwe biashara ya kuviziana kama ilivyo sasa. Hili nalo lazima waliondoe.

JAMBO LA TATU, Haki ya kujua matumizi ya kifurushi. Malalamiko ya vifurushi vya watu kuliwa isivyo kawaida ni mengi mno.

Unanunua dakika 20 unaongea 10 unaambiwa kifurushi kimeisha, unabaki kushangaa. Ni lazima waweke mfumo wenye kutoa taarifa sahihi na za wazi(transparency) ili kumwezesha mtumiaji kumonita matumizi ya kifurushi chake.

Malalamiko ya watu ya kutumia vifurushi chini ya kile walichonunua yanaongezeka siku hadi siku. Kuwaachia makampuni ya simu wao wawe ndio wauzaji wa vifurushi, na wao hao hao ndio wakueleze umetumia nini,kama umemaliza au hujamaliza, huku wewe mteja ukiwa kipofu/gizani ukisubiri kupokea lolote wanalolisema wao, kupigwa hakuwezi kukwepeka.

Waweke mfumo ambao wao pamoja na mteja watamonita matumizi ili mteja aweze kuhoji. Teknolojia imekua hili ni dogo sana.

JAMBO LA NNE Haki ya kuhamisha kifurushi.

Nimesema hapo juu kifurushi ni mali yako na ndo maana unailipia pesa na hivyo kuwa na haki ya kuitumia kwa uhuru.

Kwa msingi huu makampuni ya simu ni lazima yaweke mfumo unaomwezesha mtu kumhamishia mtu mwingine kifurushi kama ilivyo kwenye muda wa kawaida wa maongezi. Maana yake nikinunua kifurushi cha 1000 labda dakika 10 za maongezi, Mb 100, na sms 50.

Niwe na uwezo wa kumgawia yeyote ninayemtaka kiasi cha muda wangu wa maongezi,sms au Mb. Na hii ninaamini inawezekana kabisa kugawiana watu wa mtandao mmoja.Tunahitaji uhuru huu kwetu.

JAMBO LA TANO.Haki ya kupewa tahadhari kuhusu kifurushi au muda wa hewani unapokaribia kuisha. Kuna makampuni wana huduma hii lakini wanaitoa kwa hiari sana na wengine wameacha kabisa. Wengine wanatoa tahadhari muda unapoisha na sio unapokaribia.

Tunataka watoe unapokaribia ili mtu ajipange. Ni haki mtu kupewa tahadhari wakati akizungumza,akiwa kwenye mtandao, au sms, kuhusu dakika zake kukaribia kuisha. Sio sahihi wala ustaarabu simu kukatika ghafla bila tahadhari.

Na wanafanya hivyo maksudi wakijua unapokatakiwa na mawasiliano ghafla ni lazima tu utakuwa hujamaliza haja yako na hivyo utalazimika kuongeza vocha ili umalizie na wao wapate mauzo zaidi.

Wanajua ukipewa tahadhari unaweza tu kufupisha mazungumzo yako na wakati simu inakatika ukawa tayari umemaliza na hivyo usihitaji tena kuongeza vocha. Tabia za hovyo kabisa za kuviziana.

Unawezaje kunipa tahadhari ya muda kuisha ukashindwa kunipa ya muda kukaribia kuisha. Hili nalo tunataka lifanyiwe kazi.

Sita: unakuta umenunua kifurushi labda Cha siku au wiki halafu unakuta kunatatizo la mtandao na tatizo nilao unakuta mtu anapoteza kifurushi chake na hafidishiwi mtumiaji anakuwa amepoteza huku kampuni ikinufaika hili nalo lazima likome

SHERIA ya Mambo haya kwa ujumla wake ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 18( c ) inayotaka uwepo wa mawasiliano bila kuingiliwa, lakini yanakiuka Kanuni za Kielektroniki na Mawasilano ya Posta kuhusu viwango vya Tozo GN. No 22/2018 hasa Kanuni ya 4 ( 1na 2) inayotaka viwango vyote vya tozo za simu kuwa vya haki na kadri(just and reasonable), yanakiuka Kanuni ya 4 ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inayotaka mlaji kupewa taarifa kwa usahihi ya matumizi ya huduma muda wote, yanakiuka Sheria ya Ushindani namba 8/2003 inayotaka mtoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia zaidi maslahi ya watu wa hali ya chini, na sheria nyingine nyingi zimekiukwa.

Na tuelewane vizuri hapa, hakuna kitu kinaitwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA. Sheria iko wazi kuwa neno,maneno,sentensi au msemo wowote wenye lengo la kusigina haki ya mtu/watu ni batili.

Basi nitaviomba vyombo vya maamuzi vitusaidie kuyaweka sawa haya sita.nawasiliana na wana sheria wangu wa LIS Low chembers kwa ushauri zaidi ili haki iten deke.

Naomba tushirikiane kutetea haki ya wanyoge.
 
Kuna mtu humu amewahi kuleta hoja hizi za msngi aliishia wap kwan...nmewahi kuwajaribu wazee wa power for u..wakasema ku expire bando sio huduma wao wanauza vocha ambayo hai expire hata usipotomia
Waongo hao mbona vocha zina expire date?
 
Mkuu...sidhani kama umefanya homework yako vizuri kwenye hilo.

Kifupi ni kwamba ukiwaambia bando lisiexpire watakuuzia mb 50 kwa 1000 utakaa nayo muda gani? ref halichachi inavyo apply.

Halafu kujiunga ni option na ni kama promotion tu bt unaweza tumia muda wako wa maongezi tu kupiga simu,kutuma msg na kusurf bila ku expire,unless una hoja nyingine Ila kwa hizo huna locus stand.
 
Mkuu...sidhani kama umefanya homework yako vizuri kwenye hilo...
Aisee..nahisi wewe utakuwa mnufaika wa hio so called mitandao ya simu...ninyi ni majifi kabisa....maana pamoja na hio option unaosema hapo ya halichachi nayo inamuda wake wa kuisha..huu ni wizi na udhalimu wa Hali ya juu.

Mtoa mada heko kwa kuweka hapa hizo hoja..Kama utachelewa wewe Mimi nafikiria kwenda mahakam kidai fidia na mabadiliko ya hizo huduma kwa kutumia hoja zako
 
Aisee..nahisi wewe utakuwa mnufaika wa hio so called mitandao ya simu...ninyi ni majifi kabisa....maana pamoja na hio option unaosema hapo ya halichachi nayo inamuda wake wa kuisha..huu ni wizi na udhalimu wa Hali ya juu.

Mtoa mada heko kwa kuweka hapa hizo hoja..Kama utachelewa wewe Mimi nafikiria kwenda mahakam kidai fidia na mabadiliko ya hizo huduma kwa kut
Nimekupa fact jibu fact...sasa habari za mimi kunufaika na mitandao zinahusiana vipi hapa?
Pia kuna kampuni zina halichachi zenye expiry date na ambazo hazina...kwa wale wenye expiry date watakupiga mahakamani kwa maana hiyo waliyoweka hapo ni invitation to treaty na siyo offer,do your homework on that...penda kujifunza vitu na siyo kukalia ubishi tu usio na maana.
 
Wizara, mamlaka tcra, na wamiliki wa mitandao na wadau wana mkutano wa pamoja kujadili hizo changamoto, usikose hilo beba na mwanasheria wako ukalipue bomu
 
Kuna mtu humu amewahi kuleta hoja hizi za msngi aliishia wap kwan...nmewahi kuwajaribu wazee wa power for u..wakasema ku expire bando sio huduma wao wanauza vocha ambayo hai expire hata usipotomia
Fursa mkuu
Fursa kila kona
 
Mkuu...sidhani kama umefanya homework yako vizuri kwenye hilo.

Kifupi ni kwamba ukiwaambia bando lisiexpire watakuuzia mb 50 kwa 1000 utakaa nayo muda gani? ref halichachi inavyo apply.

Halafu kujiunga ni option na ni kama promotion tu bt unaweza tumia muda wako wa maongezi tu kupiga simu,kutuma msg na kusurf bila ku expire,unless una hoja nyingine Ila kwa hizo huna locus stand.
Inatakiwa wakitoa Mb500 kwa sh500 waniache nitumie wasikate eti kisa mda umeisha
 
Wizara, mamlaka tcra, na wamiliki wa mitandao na wadau wana mkutano wa pamoja kujadili hizo changamoto, usikose hilo beba na mwanasheria wako ukalipue bomu
Shukurani mkuu
 
NI WAKATI WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Niwakati Sasa wakuyashitaki Makampuni ya simu Tigo, Airtel, Vodacom na Halotel. Kwa mujibu ya Sheria Namba 12/2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mashtaka ya aina hii yanatakiwa kuaandikiwa makampuni hayo taarifa kuyataka yarekebishe ndani ya siku 30 ninachokilalamikia.

Nitaomba mambo sita nikifungua kesi hii.

JAMBO LA KWANZA, Vifurushi vyote havipaswi kuexpire. Kitu pekee ambacho kinapaswa kumaliza kifurushi inatakiwa iwe ni wewe kuongea hadi dakika zako zikaisha.

Si haki kukata kifurushi cha mtu ambaye dakika zake za kuongea,za data, au sms bado zipo kwa kigezo cha kuexpire au muda wake wa wiki, masaa12, nk kuisha. Lazima kitu hiki kiondoke.

Mathalan, umejiunga kifurushi cha 1000 na umepewa dakika 10 ndani ya masaa 12. Umetumia dakika 3 tu ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 300, na masaa 12 yameisha. Maana yake kwenye 1000 yako zilibaki dakika 7 ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 700, ambazo hizo sasa shilingi 700 kampuni ya simu inajirudishia kwa kigezo cha muda kuexpire. Nachelea kuiita huu wizi lakini initoshe kusema hii haiwezi kuwa haki na haikubaliki.

Lakini pia ninapolipa 500 na wewe ukaniuzia kifurushi si nimekulipa hela yako yote na wewe hunidai. Sasa kwanini tena unachukua kilekile nilichonunua kwako na hela yako yote nimeshakulipa.

Ni hivi,unaponunua kifurushi ni sawa na umenunua bidhaa, na ukishanunua bidhaa hakuna mtu mwingine yeyote, akiwemo aliyekuuzia bidhaa hiyo, mwenye haki ya kuichukua tena bidhaa hiyo yote au sehemu yake isipokuwa wewe uitumie mpaka iishe.

Tizama Tanesco na LUKU. Tanesco ikishakuuzia umeme/units ukamlipa basi hatma ya units zako ni utumie mpaka umalize.Hawezi kuikata na kujirudishia kwasababu anajua alikuuzia bidhaa na wewe ukamlipa na hivyo una haki ya kutumia bidhaa yako mpaka umalize. Hii ndiyo HAKI.

Kinachofanywa na makampuni ya simu ni sawa ununue soda dukani na mwenye duka umlipe hela yake yote. Halafu mwenye duka huyohuyo akwambie kwamba usipoinywa soda yote kufikia jioni au ndani wiki au mwezi nitakuja tena kuichukua nyumbani kwako, na aje kweli aichukue iwe mali yake tena kwa mara ya pili.

Zaidi ya hayo,ukweli halisi ni kuwa kifurushi kwa muundo wake si bidhaa inayoexpire. Ukinunua soda ikiexpire utauona, utaona kabisa kwa macho kadhalika bidhaa nyingine zenye sifa ya kuexpire. Lakini kifurushi kwa uhalisi wake si bidhaa inayoexpire au yenye sifa ya kuexpire.

Hili neno kuexpire limetengezwa ili kuficha neno kupora au uporaji. Ukweli ni kwamba kifurushi kinaporwa makusudi kwa kigezo hovyo kabisa na dhahania cha kuexpire, sijui masaa yako 12, sijui wiki yako, sijui mwezi wako umeisha nk. Kifurushi kinaishaje kabla dakika zangu nilizolipia kwa ukamilifu sijazitumia zikaisha?

Yapo haya nayo lazima yaeleweke, mtu amejiunga lakini yuko safarini hawezi kutumia mda wake , mwingine alipo hakuna network, mwingine hajatumia mda wake alikuwa bize na kazi zake, mwingine simu haikuwa na chaji siku nzima, mwingine umeme ulikatika alikosa mawasiliano nk nk, hawa wote pesa zao walizolipia na hawajazitumia au wametumia kidogo zinakatwa na makampuni ya simu yanajirudishia pesa hizo bila kujali.

Ninataka nifunguwe kesi kuondoa unyonyaji huu .Hatuwezi kuendelea kuwa viwanda vya kutengeneza ukwasi wa makampuni ya simu.

JAMBO LA PILI Haki ya kutochanganyiwa kifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ridhaa.

Nitatoa mfano, unakuta mtu ameweka shilingi 1000 kwenye simu ambapo anajiunga 500 na 500 inabaki kama muda wa maongezi wa kawaida. Wakati anapokuwa akizungumza au akitumia data kupitia ule muda aliojiunga na ukaisha basi simu haikatiki bali inaunganisha moja kwa moja na ile 500 ya muda wa maongezi wa kawaida ambayo alikuwa hajajiunga.

Hii si sawa hata kidogo na ni vitu ambavyo vinatengenezwa maksudi ili kujipatia fedha bila kujali mtumiaji anaumia kiasi gani. Ni hivi, mtu anapoamua kujiunga 500 na akabakisha 500 bila kuiunga ana maana yake kubwa tu.Hakushindwa kuunganisha 1000 yote.Amechagua 500 kwa maksudi maalum. Sasa iweje unamlazimisha kutumia akiba yake ya 500 hata bila ridhaa yake.

Inatakiwa kuwe na chaguo (option) iwapo mtu anahitaji huduma ya aina hiyo au hapana. Au inatakiwa muda wa kifurushi ukiisha simu ikate halafu kama anataka kuendelea kutumia muda wa kawaida achague mwenyewe kuendelea kuutumia na sio kampuni ya simu kumchagulia.

Au kama anataka kujiunga na hiyo 500 iliyobaki basi ajiunge. Isiwe biashara ya kuviziana kama ilivyo sasa. Hili nalo lazima waliondoe.

JAMBO LA TATU, Haki ya kujua matumizi ya kifurushi. Malalamiko ya vifurushi vya watu kuliwa isivyo kawaida ni mengi mno.

Unanunua dakika 20 unaongea 10 unaambiwa kifurushi kimeisha, unabaki kushangaa. Ni lazima waweke mfumo wenye kutoa taarifa sahihi na za wazi(transparency) ili kumwezesha mtumiaji kumonita matumizi ya kifurushi chake.

Malalamiko ya watu ya kutumia vifurushi chini ya kile walichonunua yanaongezeka siku hadi siku. Kuwaachia makampuni ya simu wao wawe ndio wauzaji wa vifurushi, na wao hao hao ndio wakueleze umetumia nini,kama umemaliza au hujamaliza, huku wewe mteja ukiwa kipofu/gizani ukisubiri kupokea lolote wanalolisema wao, kupigwa hakuwezi kukwepeka.

Waweke mfumo ambao wao pamoja na mteja watamonita matumizi ili mteja aweze kuhoji. Teknolojia imekua hili ni dogo sana.

JAMBO LA NNE Haki ya kuhamisha kifurushi.

Nimesema hapo juu kifurushi ni mali yako na ndo maana unailipia pesa na hivyo kuwa na haki ya kuitumia kwa uhuru.

Kwa msingi huu makampuni ya simu ni lazima yaweke mfumo unaomwezesha mtu kumhamishia mtu mwingine kifurushi kama ilivyo kwenye muda wa kawaida wa maongezi. Maana yake nikinunua kifurushi cha 1000 labda dakika 10 za maongezi, Mb 100, na sms 50.

Niwe na uwezo wa kumgawia yeyote ninayemtaka kiasi cha muda wangu wa maongezi,sms au Mb. Na hii ninaamini inawezekana kabisa kugawiana watu wa mtandao mmoja.Tunahitaji uhuru huu kwetu.

JAMBO LA TANO.Haki ya kupewa tahadhari kuhusu kifurushi au muda wa hewani unapokaribia kuisha. Kuna makampuni wana huduma hii lakini wanaitoa kwa hiari sana na wengine wameacha kabisa. Wengine wanatoa tahadhari muda unapoisha na sio unapokaribia.

Tunataka watoe unapokaribia ili mtu ajipange. Ni haki mtu kupewa tahadhari wakati akizungumza,akiwa kwenye mtandao, au sms, kuhusu dakika zake kukaribia kuisha. Sio sahihi wala ustaarabu simu kukatika ghafla bila tahadhari.

Na wanafanya hivyo maksudi wakijua unapokatakiwa na mawasiliano ghafla ni lazima tu utakuwa hujamaliza haja yako na hivyo utalazimika kuongeza vocha ili umalizie na wao wapate mauzo zaidi.

Wanajua ukipewa tahadhari unaweza tu kufupisha mazungumzo yako na wakati simu inakatika ukawa tayari umemaliza na hivyo usihitaji tena kuongeza vocha. Tabia za hovyo kabisa za kuviziana.

Unawezaje kunipa tahadhari ya muda kuisha ukashindwa kunipa ya muda kukaribia kuisha. Hili nalo tunataka lifanyiwe kazi.

Sita: unakuta umenunua kifurushi labda Cha siku au wiki halafu unakuta kunatatizo la mtandao na tatizo nilao unakuta mtu anapoteza kifurushi chake na hafidishiwi mtumiaji anakuwa amepoteza huku kampuni ikinufaika hili nalo lazima likome

SHERIA ya Mambo haya kwa ujumla wake ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 18( c ) inayotaka uwepo wa mawasiliano bila kuingiliwa, lakini yanakiuka Kanuni za Kielektroniki na Mawasilano ya Posta kuhusu viwango vya Tozo GN. No 22/2018 hasa Kanuni ya 4 ( 1na 2) inayotaka viwango vyote vya tozo za simu kuwa vya haki na kadri(just and reasonable), yanakiuka Kanuni ya 4 ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inayotaka mlaji kupewa taarifa kwa usahihi ya matumizi ya huduma muda wote, yanakiuka Sheria ya Ushindani namba 8/2003 inayotaka mtoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia zaidi maslahi ya watu wa hali ya chini, na sheria nyingine nyingi zimekiukwa.

Na tuelewane vizuri hapa, hakuna kitu kinaitwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA. Sheria iko wazi kuwa neno,maneno,sentensi au msemo wowote wenye lengo la kusigina haki ya mtu/watu ni batili.

Basi nitaviomba vyombo vya maamuzi vitusaidie kuyaweka sawa haya sita.nawasiliana na wana sheria wangu wa LIS Low chembers kwa ushauri zaidi ili haki iten deke.

Naomba tushirikiane kutetea haki ya wanyoge.
Vodacom Tanzania
 
Back
Top Bottom