Mwenyezi Mungu amemjalia Rais Samia Kifua cha Uongozi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Rais wetu Jemedari wa Vita, Dereva makini, Nahodha maridadi na Hodari, komandoo wa Vita, Rubani wa uchumi, Jasiri muongoza njia, imara na madhubuti, mama wa shoka, chuma cha reli Mh. mama Samia suluhu Hassani amejaliwa na kubarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na kifua cha uongozi na uwezo mkubwa wa kiuongozi.

Ndio maana wakati wote Rais wetu amekuwa hayumbi Wala kuyumbishwa, ndio maana Rais wetu amekuwa akilipeleka mbele Taifa letu katika muelekeo unaoeleweka na kuleta matumaini kwa watanzania, ndio maana amekuwa na uwezo na masikio ya kusikiliza sauti zote, kutazama na kumtazama kila mtu kwa jicho la kiuongozi.

Rais Samia anatambua kuwa katika uongozi Kuna kutofautiana kimtizamo, anatambua kuwa katika uongozi kuna wale wanaiona na kutazama leo bila kuwa na uwezo wa kupenya kesho, anatambua kuwa katika uongozi kuna wanaolipuka mioyo yao na kutoa maneno ya karaha na lugha za kuudhi.

Kama kiongozi anatambua kuwa hao wote ni watu wake, ni wananchi wake, ni Raia wake na ni Watanzania na hivyo inahitajika busara na kifua cha hali ya juu sana katika kuwavumilia, kuwasikiliza na wakati mwingine kuwasamehe pale wanapokuwa wanazungumza mambo pasipo kuwa na uelewa wa kutosha na undani wa Taarifa juu ya Jambo fulani.

Pamoja na ukweli kwamba Rais Samia ni mwanadamu mwenye moyo wa nyama, mwenye Damu ya binadamu, mwenye hisia za maumivu, mwenye mume, watoto, wajukuu, wakwe, ndugu, jamaa, rafiki, mawifi na mashemeji lakini ameendelea kuwa mvumilivu na mwenye unyenyekevu wa hali ya juu sana hata pale anaposhambuliwa bila sababu ya msingi.

Rais Samia ameendelea kuongoza na kuwa mbele kama kiongozi katika kuwatumikia na kuwahudumia watanzania bila ubaguzi wala chuki kwa mtu au kundi fulani, anatambua kama Rais na mkuu wa nchi na serikali ni kiongozi wa wote.

Ni mtumishi wa Watanzania wote, ni mama na mlezi wa wote anayepaswa kuwasikiliza watu wote bila kuzima sauti ya mtu yeyote yule kwa njia ya aina yoyote Ile. Ndio maana ameendelea kuimarisha demokrasia na Uhuru wa habari hapa nchini, ndio maana watu wapo huru kuzungumza bila hofu wala wasiwasi.

Ndio maana vifua na mioyo ya Watanzania ni myeupe isiyo na kinyongo wala chuki kwa kuwa kila mtu anapata nafasi ya kuzungumza hisia zake bila hofu au kulimbikiza sumu moyoni.

Rai yangu kwa Watanzania ni kutaka kuwaambia ya kuwa Rais wetu ni mwanadamu mwenye moyo wa nyama kama tulivyo sote, ni Rais wetu, ni mkuu wa nchi na serikali na ni Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama.

Ni lazima Rais wetu aheshimiwe, ni lazima kiti chake kiheshimiwe na kulindwa kwa wivu wa hali ya juu sana. Rais ndio nembo yetu, ndio taswira yetu kama Taifa. Tumheshimu sana Rais wetu, mwenye kuona dosari mahali basi aeleze kwa lugha za staha, heshima, busara na uungwana pasipo kumshambulia Rais wetu.

Kifua cha Rais wetu ni viongozi wachache sana au hawapo kabisa kama Rais Samia kwa sasa barani Afrika. Ndio maana utaona huko kwingineko wakikimbizana mahakamani na kuviziana na wapinzani wao, huko utaona wakifungana pingu na kudhalilisha wapinzani wao wa kimawazo na kifikira.

Huko utakuta sheria kali zikitungwa kila jua likichomoza kumlinda Rais na watu wake, huko utakuta magari ya polisi yakipiga doria na maslaha ya kivita begani na vifuani kwenye ofisi na Kaya za wapinzani wao, huko utakuta watu wakikimbia nchi zao kila siku.

Lakini hapa Tanzania chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassani unaona amani, utulivu, upendo, umoja na mshikamano vikiwa vimetamalaki miongoni mwa Watanzania.

Huku unaona watu wakijivunia kuzaliwa na kuishi Tanzania, huku unaona watu wakifurahia kuwa nchini na kufanyia shughuli zao za kiuchumi nchini, huku unaona watu wakiona fursa hapa hapa nchini na siyo nje ya nchi.

Hii yote ni kutokana na mazingira bora yaliyojengwa na Rais Samia, hii yote ni kutokana na Rais Samia kuamua kuwapa nafasi Watanzania kujivunia uUtanzania wao na kuiweka serikali mikononi mwa Watanzania.

Hii yote ni kwa kuwa Rais Samia ameamua kuendesha nchi kwa maslahi mapana ya Taifa letu, ndio maana kila Mtanzania anayo furaha, amani, matumaini na tabasamu moyoni mwake.

Ipo siku miaka ya mbele panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu Watanzania tutakuja kutambua umuhimu na upekee wa Rais Samia, tutakuja kupiga magoti kumuomba msamaha kwa wale wanaomshambulia bila staha, tutakuja kusema tulimkosea na kumvunjia heshima mama huyu mpole, mkarimu, mnyenyekevu, mzalendo, mwenye upendo wa dhati na moyo wa huruma kwa watu wote. Tutakuja kufahamu kuwa Rais Samia alizaliwa kama zawadi kwetu Watanzania.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Back
Top Bottom