Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,070
- 136,458
Labda ni mimi tu. Labda mimi ndo tatizo. Labda nina uwezo mdogo wa kuelewa mambo.
Labda ni hivi au labda ni vile.
Labda nategemea mambo flani flani toka kwa watu ambao sipaswi kutegemea chochote au lolote toka kwao.
Kuna ukimya wa ajabu sana kutoka kwa baadhi ya watu na taasisi ambazo mtu ungedhani ziko mstari wa mbele katika kutetea haki za kibinadamu.
Kwa uwazi tu, sitegemei chochote toka kwa muuaji na kiongozi haramu.
Ataanzia wapi kukemea kilichotokea na kutoa pole kwa wahanga?
Lakini wengine nao je?
Wako wapi wale viongozi wa dini ambao huwa wanakemea utekaji?
Wako wapi wale viongozi wa zamani ambao wamestaafu kukemea kilichotokea?
Watu wamejikausha tu kama vile hakuna chochote kilichotokea!
Kuna mambo mtu mwenye akili timamu hupaswi kuyakalia kimya.
Zaidi ya wiki sasa na watu hawasemi chochote.
Ukimya mbele ya ukiukwaji wa makusudi wa haki za kibinadamu ni usaliti.
Waendelee kupumzika kwa amani wazalendo wote waliopoteza maisha yao na wale walioumizwa.
Kwa nyie wasaliti, kama mnadhani kila kitu ni upepo tu na lililotokea nalo litapita tu kama upepo, subirini muone.