Ukimwi na Mapenzi

PROF. ENG

Senior Member
Nov 15, 2011
122
34
Mume wangu nakupenda sana, ujilinde, mimi siwezi kukulinda au kukuchunga kila uendapo, unaweza ukawa kuna mambo unayafanya ambayo mimi hutaki niyajue na wala sitaki nijue, Tafadhali sana lolote lile utakalofanya jua kuna ukimwi, Angalau ukumbuke kutumia kinga, kwakweli sitakusamehe wala kukuhudumia siku ukipatwa na ukimwi. Hayo ni maneno ambayo mke alikuwa anamwambia mumewe. Lakini baada ya miaka kadhaa ya ndoa kama nane hivi mke ikajulikana yeye ndio amepata ukimwi bahati nzuri mume alipoenda kucheki yeye alikuwa bado hajaathirika. Mbaya zaidi jamaa hajawahi kusikia wala kuhisi kama mkewe anatoka nje ya ndoa mpaka alipogundua dalili za ukimwi kwa mkewe.

Kweli ndoa ngumu. Kupata mtu muaminifu ni ndoto.
 
hiyo ndio life in the flesh

na sifa kuu ya ndoa pia ni surprises kama hizo

inauma sana, lakini labda yapo yaliyochangia huyo mama kupata HIV ambayo angepewa nafasi ya kuelezea (kama atakubali) basi wote twaweza kumuonea huruma
 
Aliwazalo mjinga ndo litalomtokea..
Huyo mke alikuwa ni mwizi ndo maana alikuwa akihisi kuwa mumewe pia ni mdanganyifu kama alivyo yeye.
Mwisho wa siku ameumbuka kwa tabia yake.
 
hatujui upande wa pilli wa hii hadithi...nachelea kumuhukumu huyu mama coz hatujui nini kilimsibu....all in all uaminifu unajengwa na vitu vingi sana...
 
kwa nini mnakimbilia maambukizi kwene mapaja peke yake? huwenda aliambukizwa kwa kumuuguza mtu mwingine wa kifamilia hata hivyo hastahili kuhukumiwa anahitaji huruma na kitiwa moyo.
 
kwa nini mnakimbilia maambukizi kwene mapaja peke yake? huwenda aliambukizwa kwa kumuuguza mtu mwingine wa kifamilia hata hivyo hastahili kuhukumiwa anahitaji huruma na kitiwa moyo.

Mke baada ya kujulikana kama ana ukimwi, alitubu, akawataja watu wake wawili ambao ndio alikuwa anakutana nao, mmoja ameshatangulia mbele za haki, anahisi huyo ndio alimuambukiza. ni mfanyakazi mwenzie ofisini anapofanyia. Mume alimkumbusha hayo maneno mkewe aliyomwambia miaka kama nane iliyopita. Mke ni kilio tu hajui aseme nini. Anafikiria hata kujiua.
 
majuto ni mjukuu huyo dada atalaumu sana wizi wake na tamaa zake anazokuwa anazifanya na adhabu inaanzia hapa hapa duniani then ahera
 
hata akijiua bado ni vile so muhimu aendelee na maisha kwani ukimwi si tishio kivile
 
ka ujumbe flani katamu na kanahudhunisha vilevile.
Tusali sana.
 
Mambo ya discordant couples hayo,jamaa amshukuru mola wake na kikubwa zaidi amtunze mkewe na ammpe moyo,waishi watunze watoto,kulaumiana haisadii,wakubali tu hali halisi.
 
Mke baada ya kujulikana kama ana ukimwi, alitubu, akawataja watu wake wawili ambao ndio alikuwa anakutana nao, mmoja ameshatangulia mbele za haki, anahisi huyo ndio alimuambukiza. ni mfanyakazi mwenzie ofisini anapofanyia. Mume alimkumbusha hayo maneno mkewe aliyomwambia miaka kama nane iliyopita. Mke ni kilio tu hajui aseme nini. Anafikiria hata kujiua.
Katika mahusiano, ndoa au urafiki ukiona mwenzako bila wivu anakuambia wewe nenda tu nje ya uhusiano ila nisijue, jua kuwa yeye anatembea nje ya uhusiano,na guilt conscious inamtesa ndo maana anataka na wewe utoke ili muwe sawa.Kama mwanamke au mwanamume ni mwaminifu hata siku moja hawezi kukubali kusikia mwenzake anatembea nje!
 
I concur with you aisee..
 
Mume wangu nakupenda
sana, ujilinde, mimi siwezi kukulinda au kukuchunga kila uendapo,
unaweza ukawa kuna mambo unayafanya ambayo mimi hutaki niyajue na wala
sitaki nijue, Tafadhali sana lolote lile utakalofanya jua kuna ukimwi,
Angalau ukumbuke kutumia kinga, kwakweli sitakusamehe wala kukuhudumia
siku ukipatwa na ukimwi. Hayo ni maneno ambayo mke alikuwa anamwambia
mumewe. Lakini baada ya miaka kadhaa ya ndoa kama nane hivi mke
ikajulikana yeye ndio amepata ukimwi bahati nzuri mume alipoenda kucheki
yeye alikuwa bado hajaathirika. Mbaya zaidi jamaa hajawahi kusikia wala
kuhisi kama mkewe anatoka nje ya ndoa mpaka alipogundua dalili za
ukimwi kwa mkewe.

Kweli ndoa ngumu. Kupata mtu muaminifu ni
ndoto.

waaminifu wapo kibao
 
hatujui upande wa pilli wa hii hadithi...nachelea kumuhukumu huyu mama coz hatujui nini kilimsibu....all in all uaminifu unajengwa na vitu vingi sana...

Me too!
Ila kwa kauli yake ya kutomuhudumia mumewe, sijui na mume afanye hivyo pia???
 
Inamaana hawakuwa na mahusiano ya kinyumba? Hili swala la mke/mume kuwa na virusi lakini mwenzake akakosa linanitatiza sana.

The only explanation ni kama hawakutani kimwili, lakini kama wanakutana kimwili regularly inashangaza.
 
Back
Top Bottom